Uozo Ndani ya Polisi: Wanachi wamechoka; Jisomee huu Mkasa

Ni watanzania wangapi wanajua haki na wajibu wao ndani na nje ya nchi yao?ndo maana wanaojua sheria kama akina chenge wanatanua kila mahala.
 
Ni watanzania wangapi wanajua haki na wajibu wao ndani na nje ya nchi yao?ndo maana wanaojua sheria kama akina chenge wanatanua kila mahala.

Freedom is coming tomorrow.....Matemate ndo jina la huyo polisi aliyepachika kesi feki
 
He! Mkasa huo mbona cha mtoto,c bora huyo mama anakaa mjini,watu kama kova na huyo bw wa takukuru wanapata hata taarifa...chukua huu mkasa nilioukuta mkoani morogoro,wilaya ya ulanga,tarafa ya malinyi,kijiji cha biro...kuna bw m1,msukuma kwa kabila,alifiwa na mtoto wake wa umri wa miaka 2, (niseme tu kwanza hawa wasukuma wanaogopa polisi kuliko simba) kwa mujibu wa mtoa habari wangu kifo cha mtoto huyo kilisababishwa na ugonjwa wa kuharisha na kutapika. Na ukichukulia hawa mabwana wanaishi mbali mashambani. Kuna polisi m1 akasikia jamaa kafiwa akaenda kwa yule mfiwa na kumtetemesha kwa kumwambia yeye ndo kasababisha kifo cha yuke mtoto kwa uzembe wa kutompeleka mwanae haspitali,...basi,akamtaka jamaa ampatie Tsh milioni 2 la sivyo atamfungulia kesi ya mauaji. Msukuma wa watu akapiga hesabu akaomba apewe wiki 1,akauza mazao yake na ng'ombe akampatia polisi yule mshenzi tsh 2ml akatokomea zake. Mtoa habari wangu anadai hata OSS hajui hiyo deal. Imagine ndo wewe mwanao amekufa wanakuja wahuni wanakuchukulia na pesa ...matukio ni mengi!
huyo msukuma inawezekana ni kweli aliua mwanae,ujinga wa aina gani wa kutoa amount yote hiyo bila kosa lolote.wajinga ndiyo waliwao.
 
Polisi ni uozo uliokithiri, wanalazimisha hadi rushwa ya shs elfu moja!sijui hii ni njaa au tabia na kamfumo ka kila mtu kufanya anavyoweza chini ya manifesto ya ccm, make haka kautaratibu kamezoeleka!dawa ni kubadilisha uongozi na kuwa na viongozi walio serious sio hawa ambao wameshindwa kwa kila kitu!najisikia vibaya kuitwa mtanzania wa sasa!!!!!!!!!!!!!
 
Wananachi nao waache ujuha. Kwanini wasiwachome moto vibaka hawa waliovaa magwanda. Hiyo ndiyo suluhu ya ujambazi huu ambapo kila mwenye nafasi yake anaitumia kuwanyonya na kuwanyanyasa wananchi. Hapa tatizo ni wananchi wenyewe. Mbona kule Mwanza wananchi walipoanza kuchoma moto vituo ya polisi unyanyasaji umepungua. Ni suala la kuamua maana hii nchi ni yetu sote na hawa majambazi wachache wanalipwa mishahara kwa kodi yetu kutulinda na si kutunyanyasa wala vinginevyo.
 
You should have abridged your story. Some find it boring to peruse such lengthy essays.

Acha uvivu wa kusoma mkuu. Huu uvivu ndo unawafanya watu wa aina yako kushindwa kuelewa mambo madogo na kutoa pumba humu. Jifunze kusoma mkubwa sasa wewe acha utoto
 
tena mjihadhari kweli na traffic wa ubungo, ukikataa kuwapa pesa na wakiogopa personality yako wanakupa kesi. Mazingira ya mtoa mada yanafanana kabisa na yaliyonikuta walinipa kesi ya kumteka askari na wanakuweka celo ndio mchezo wao.
Tukichukua nchi 2015 ni kulibomoa lote na kuwapa kazi wajeda, simu lazima wakuzuie wakikuogopa.
 
Ndo maana yake, huko Nigeria ni mtutu wa bunduki+sangoma na mambo yanaenda. Isione watu wanchinjana kila siku ukadhani watu ni animatic- basically wamechoka.
Hapa Mungu peke yake hatoshi. cha msingi polisi wajirekebishe vyenginevyo....!
 
tena mjihadhari kweli na traffic wa ubungo, ukikataa kuwapa pesa na wakiogopa personality yako wanakupa kesi. Mazingira ya mtoa mada yanafanana kabisa na yaliyonikuta walinipa kesi ya kumteka askari na wanakuweka celo ndio mchezo wao.
Tukichukua nchi 2015 ni kulibomoa lote na kuwapa kazi wajeda, simu lazima wakuzuie wakikuogopa.
Hapa sasa naanza kuelewa kwanini baadhi ya maeneo
vituo vya polisi vinavamiwa POLISI ni majambazi!
 
Nampa pole sana huyo mama. Pale ubungo ni kweli pananuka rushwa na tabia mbovu wa askari wa pale, mi mwenye yameshanikuta ya pale, ni story ndefu sana. Ila ni kweli kabisa kama hakuna hatua za haraka zitachukuliwa kwenye hiki kituo mengi yataendelea kutokea na kukosa haki zao za msingi. Lakini na wananchi hatuna budi kujua sheria zetu pamoja na kujiamini ili angalau uwe na uwezo wa kujitetea na kuchukua hatua unapoona unaonewa. maana hawa askari wana tabia ya kukusoma, wakikuona ni lele mama watakusumbua sana na kukutisha mambo kibao mara sijui mahakamani wakijaribu kutengeneza mazingira ili uwape rushwa kubwa. Hasa kwenye hili la kwenda mahakamani waTZ tupo waoga sana tukitishwa kwenda mahakani, lakini ukweli ni kwamba mtu kubali upelekwe huko, na hata kama ni kweli watakupeleka fine utakayolipa mwishowe kama kweli umekosa ni ndogo sana ukilinganisha na rushwa utakayoitoa.
 
Sasa hizo rushwa ni ndogo mimi nilipata kesi ya kusingiziwa tu nikashitakiwa na mtu anaeaminika kanunua police wote wa nchi hii. Kwa sababu sijuloikani nakaa wapi. Kwa kesi ya shilingi laki mbili na nusu. Nilitafutwa kwa gari 5 za kinondoni na gari mbili za kikosi maalumu cha tosi. Nikakamatwa kama jambazi lililo uwa kijiji kizima au kama jambazi lilitaka kufanya mapinduzi enzi za baba wa taifa???? Nikapelekwa ostabay police wakasema hii kesi iende central police, kufika pale nikasachiwa sikupatikana na silaha wala kitu chochote cha hatari. Wanirudisha kwenye magari ya kikosi maalumu magari mawili yanaongozana. Ndani ya gari nililo kuwamo askari wakaanza kuniuliza hivi huyu jamaa umemchukulia mke?? Nikasema hapana wakasema katoa pesa tukuwekee madawa ya kulevya ndio iwe kesi yako basi tukaenda maeneo ya kinondoni wakanunua drugs nikapelekwa kilwa road police post nikaacha huko nililala pale kwa siku sita bila kusikilizwa wala kuandikiwa maelezo au kujua kesi inayoniweka ndani, bahati nzuri hawakuandikisha madawa yale ya kulevya. Wakati nilipo kamatwa nilikuwa na mtu wa karibu anaenifahamu yeye alikuwa akifuatilia. Baada ya kujua kuwa hii kesi ni yakutengenezwa akaona kakuna kinachoweza kunitoa kule police bila kwenda ikulu kutafuta nguvu kubwa mungu saidia jamaa akaenda kuomba apointment na mkurugenzi wa usalama wa taifa hii ilikuwa ngumu sana akabahatisha kumuona katibu mkuu kiongozi, yeye akaandika kimemo kwa mkurugenzi wa usalama ndio simu ikapigwa nikaachiwa siku ya 14 bila shariti lolote. Sasa fikiria ni wangapi wamo magerezani bila makosa halali nchi hii. Yani akipatikana mtu akafadhili silaha nchi hii atapata watu karibia taifa zima. Kule vijijini kuna watu wakijiunga na upinzxani wanatengwa na kubambikiwa kesi za mauaji. Viongozi nyie kuleni kuku tu ila sikumoja vituo vyote vya police vitaswaka moto kama kile cha hedaru.
 
Hii tanzania ya watu wanaoishi kwa amani muda mfupi waitiwa wakachukue Tuzo ya Amani ya NOBEL kwa misingi hii mibovu ya Amani. Mwenyewe ninamikasa mingi mno yaliyonipata Vituo vya Polisi hapa Nchini, na hata ukienda Burundi ni hayahaya yanayotokea kwa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom