Uongozi wa Chama Kipya Ukiingia; CCM kifutwe?

Mbona CCM kimejifuta chenyewe si unaona awaelewani ata kauli zao, kuanzia mtoto wa mkulima mpaka mkuu wa wilaya awaelewani, mm najua chama bongo kipo kimoja tuuu CDM, vingine ni magenge ya wauni na waganga njaa.
 
CCM iko ICUinapumulia mashine, hata Sharon amepumulia mashine miaka mingi. Acha kife tu, hatujui kitakachozaliwa kitakuwaje lakini yote mbele kwa mbele. Bora mchawi ajaye kuliko tumjuaye maana keshatung'ata mno.
 
CCM imekuwa ni sehemu ya Dola kiasi kuwa ni vigumu kufikiria kuwepo kwe CCM isiyokuwa na dola. Vyama vyote vya aina ya CCM, baada ya kupoteza madaraka vimejikuta katika hali isiyoeleweka na kusema kweli havijengeki tena. Nakubaliana na aliyesema kuwa CCM itakapoondoka madarakani haitahitaji kufutwa, kitakuwa tayari kimefutwa kwa kuondolewa madarakani.

Angalia fate ya KANU ya Kenyatta kule kenya, UNIP ya kaunda kule Zambia, UPC ya Obotte kule Uganda, Rwanda, Burundi na hata Congo. Ok baadhi ya nchi kama Uganda, Congo na Rwanda vyama tawala vya uhuru viliondolewa na mapambano ya vita. Lakini nchi zilizofanya uchaguzi na kuving'oa vyama tawala vya uhuru kwa kutumia kula kama Kenya, Zambia na Malawi vyama hivyo havioneshi kuwa vitakuja kuinuka tena. Tanzania CCM inavyoelekea itaondolewa kwa uchaguzi (kama si 2015 basi 2020) kama ilivyofanyika Malawi, Zambia na Kenya. Uchambuzi wa kilichotokea kwa hao majirani wote unaonesha kuwa siku ikiondolewa madarakani CCM, utakuwa ndo mwisho wake.

Ndiyo maana wako tayari kufanya chochote ku 'hang' on power ikiwa hata kulazimisha serikali ya umoja wa kitaifa. Watu wa CCM haya ninayoyaandika hapa wanayajua, ingawa mahali chama kilipokwisha kufikia hakirekebishiki tena na kushindwa kwenye uchaguzi ni jambo ambalo halizuiliki. Ni ama CCM ikubali kushindwa, iondoke madarakani na ife au ing'ang'anie madarakani nchi iingie kwenye matatizo ya vita ya wenyewe kwa wenyewe tuishie kama ilipo Somalia! Hakuna kitu cha kati katika haya mawili!

Mwenendo wa CCM katika siku za hivi karibuni unaonesha kuwa wako tayari kung'ang'ania madarakani na nchi iingie kwenye machafuko, kwani watatupia lawama kwa wale wanaotaka kuwang'oa madarakani! Inaonekana wana mawazo kama Ghadafi kuwa walibya wanampenda mno na wanaompinga ni wabwia unga na mawakala wa al-qaeda. CCM nao wanaonekana kuamini kuwa watanzania wanaipenda mno CCM na wanaoipinga CCM ni waleta vurugu na fujo kwa hiyo CCM iko tayari kutumia nguvu zote kupambana nao! Hayo kwa haraka haraka yanaonekana kuwa ni mawazo miongoni mwa viongozi wengi wa CCM.

Sasa hali ikiwa hivyo tujiandae. CCM hairekebishiki tena. Kufa kitakufa tu. Suala ni kitakufaje? Ni ama Kitakufa na nchi yote (pale kitakapokataa kutoka madarakani baada ya kushindwa kihalali) au kitakufa chenyewe pale kitakapokubali kuondoka madarakani. Kukataa kuondoka madarakani kwa CCM ni pamoja na kuzuia uwezekano wowote wa kuwa na uchaguzi huru na haki, ili kiendelee ku chakachua matokeo ya chaguzi zote zitakazofanyika. Na iwapo kutakuwa na uchaguzi ulio huru na haki, itakuwa ndo uchaguzi wa mwisho kwa CCM!

Mh mawazo yako na uandishi wako vimenikuna sana!!keep it up Sir kwa sababu uandishi ni kazi ngumu hasa utakuta mtu anaandika hoja yake lakini katikati au mwishoni anapoteza uelekeo,utakuta anaanza kuchanganya mada aua kutukana na au jazba!nadhani CCM na serikali yao wanona mawazo
yako na ninajua kama ni binadamu wa ukweli na sio mashetani kama ninavyoamini kwa sasa basi lazima yatakuwa yamewaingia akilini!Nakuomba ndugu uendelee na uchambuzi wako makini!nimesoma point by point hadi nimejisikia kulia kwa uchungu!
anyway TANZANIA WILL RISE AGAIN!!
 
Hakika wazo nzuri kwani ni kweli mali wazodai ni za ccm zilipatikana toka kwa watanzania wote leo kuna vyama vingi hivyo si halali kumilikiwa na chama kimoja(CCM).
 
wataingiaje madarakani kama cdm tunafanya vizuri?? wataingia madarakani km walioshika dola wanazembea kuleta ustawi wa jamii; na ndo maana ya ushindani wa vyama kisiasa!! kwa msingi huo, vyama vyote vitaendelea kuwepo kujiuza kwa wananchi ki sera na wananchi wataendelea kuchangua chama waonacho kinaweza waletea ustawi zaidi.

Hivi we unawajua vizuri CCM???2005 hawakuingia madarakani kwa kauli safi za ''Maisha bora kwa kila Mtz'', ''Ajira zaidi ya milioni 1 kwa vijana''...''nguvu mpya,ari mpya....'',kipo wapi sasa hivi?? wataleta hila ili kwa ku-critisize walio madakani ili kishike dola watafune tulichokianzisha...naomba unielewe, CCM hakifai hata kuwa chama pinzani, kifie mbali kule.
 
Ukifuta ccm inabidi uifute na vyama vifuatavyo maana wote wanashirikiana na hiyo ccm:
Cuf
tlp
nccr-mageuzi
chama cha dovutwa
udp
pona
tadea(hiki kinaniuma maana kambona angekuwepo asingevumilia ujinga unaofanywa na hao alowaachia) lkn futilia mbali
na vinginevyo vinavyoshirikiana na ccm
 
Kuelekea kwenye Katiba Mpya ninaamini ni lazima CCM ifutwe ili ianze upya kama cha cha siasa. Vyama vingine vyyote vilianzia moja kwa kutafuta usajili wa muda na baadaye wa kudumu kwa kupita na kuomba wanachama wapya isipokuwa CCM. Aidha kianze moja kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 na hivyo kwenda kwenye uchaguzi huo kama chama kipya au kisubiri kufutwa kama walivyofanyiwa Tunisia ili kukipa nafasi ya kuanza moja.


Yes kuanza moja ni vizuri lakini what about the political void. Nchi zetu za kiafrika hizi shida yetu ni kwamba bado hatujapiga hatua yakuweza kuwa na sustainable systems of governance and constitutional order governed by the Rule of Law. As Mwalimu rightly said, without rule of law people will not know what will happen tomorrow. Haiwezekani eti chama kishinde uchaguzi alafu kifute the former ruling party (unless there is major reasons like apartheid, genocide, war crimes, crimes against humanity, treasonable activities,).

Kwahiyo there would never be a legal basis for dissolution unless it was voluntary, something which is in the same order of possibility as a snow ball in hell. All I'm saying is constitutional precedence of that nature lays the foundation for despotic autocracies.

Such ideas as the one proposed in this thread are vestiges of the 19th and even more so 20th century. We ought to realize the world we live in and create a constitution that reflects our society but also upholds the universal basic human rights and tries to the utmost to protect and uphold the rule of law. And empowering this constitution, through advocacy and primary and secondary curriculum (watoto wajue misingi na maadili ya nchi). The aim being that the next generation of Tanzanians will uphold the institutions of the state and the values of the people defending rights both socio-economic and basic human nature. Kufuta CCM hakuto badili chochote maana ni watu wale wale. Mnasema CCM is corrupt, Tanzania is corrupt maana kila ofisi utayako enda utakuta hayo mambo yako pale pale.
 
Si kuifuta tu CCM, inabidi pia kusubiri miaka 120 mbele ili kizazi hiki chenye damu ya CCM kifutike ndipo reform ifanyike! Mkuu unakumbuka kosa lililofanyika miaka ile Tambaza Sec ilipofungwa na ile generation kusambazwa kwenye shule nyingine? Ilienda kumea taratibu kila ilipoanguka na matokeo yake ndio haya tunayoyaona hata kwenye ajira (kwa wanaojua kisa hiki watanielewa)...Baada ya kifo cha CCM kuwe na interval ya miaka 150 mathalan
 
Sasa hivi CCM hawafanyi kazi kama chama cha siasa, wanafanya kazi kama mhimili wa dola. Kwa tabia hiyo siku Chama kingine kikichukua nchi CCM itakufa yenyewe, viongozi wake wengi ni watu wasio kuwa na pa kushika zaidi ya kutegemea kuchukua posho za vikao na kufanya ufisadi ili waendeshe maisha.

Kadri ruzuku inavyopungua ndio na chama kinapokosa nguvu ya kiuchumi na waroho wa madaraka kukikimbia. Tujipange vizuri wananchi tuwe tayari kukitimua chama hiki kwa nguvu zetu wenyewe kwani hali ya maisha inazidi kuwa mbaya kila kukicha!

huu ni mtizamo maridhawa.. inaonekana wewe ni mchambuzii uliyewiva.. u see things broadly... true ccm itakufa automatic kama chama kingine kitakamata nchi.. naamini ni maslahi binafsi ya wakuu wachama ndo wanaofanya chama kiwepo..
 
Hili nadhani kweli ni kosa lililofanywa, tena hasa pale ambapo mali na uchumi uliojengwa na wananchi wote katika mfumo wa chama kimoja haukurudishwa serikalini au kugawanywa kwa usawa katika kila chama ambacho kingeanzishwa. Kwa sasa tunashuhudia CCM ikiwa inamiliki maeneo makubwa katika karibu kila kata lakini chimbuko haswa si uwezo wa CCM kama chama bali hali ya mfumo wa chama kimoja iliyosukuma hivyo.

Nadhani mjadala mpana hususan katika mali na vitega uchumi CCM inayo sasa unapaswa uangaliwe upya hivyo aidha virudishwe serikalini na kuwa vitega uchumi vya serikali au vigawanywe kwa kila chama cha siasa.

Kulipaswa kutoa mazingira sawa na mapana ya vyama vyote kukua
swadakta
 
Nilikuwa sijasoma post yako kabla ya ku post yangu-we are precisely in the same line of thinking...Huwezi kujipindua hata siku moja; lakini pia kama walivyogusia wengine ung'ang'anizi wao utasababisha watu kukosa uvumilivu na kuanza kuwatoa kwa nguvu...

Kama ningekuwa mimi CCM ingetafuta exit strategy nzuri kwa kuondoa mamluki wote wa chama then ku recruit serious people na huku wakiendelea kufanikisha smooth transition kwenye true multipartism...ninachoona CCM inazidiwa na wachache wenye maslahi ambao wanahofu kama wakikosa madaraka basi na maslahi yao yatakosa legitimacy na hivyo kuwa cost hao wachache so wengi wangependa transition but wachache hawako tayari na wana nguvu.

Cha kusikitisha hao wachache cost ya kuendelea kung'ang'ania ya weza kuwa kubwa kuliko kukubali ni bora wangeangalia jinsi ya kuleta smooth transition na huku wakiangalia kuweka maslahi yao independent na utawala....All in all hakuna kitakachorudisha nyuma changes maana wengi wamesha kuwa awere and unfortunately economy is not good enough to hold this pressure back!
Hujambo ndugu yetu? Nina kusoma, at long last your work is coming into image (featuring out clearly). Time is a good friend....God is sovereign!
 
Back
Top Bottom