"UONGO" ni sehemu muhimu katika maisha....?

Speed of light

JF-Expert Member
Nov 8, 2014
313
284
Nimeikuta mahali hii

Uongo ni tamko lisilo kweli lanalotolewa kwa makusudi. Mtu anayesema uwongo anajua au anahisi ya kwamba maneno yake si ya kweli lakini anataka msikilizaji wa maneno yake (au mpokeaji wa ujumbe wake) ayaamini kuwa kweli.
Mara nyingi uwongo hutumiwa kwa kusudi la kuficha kosa , aibu au tendo
haramu. Kusudi lingine ni kujipatia
faida au kuzuia hasara .
Uwongo hutazamwa kuwa tofauti na maneno yasiyo kweli lakini msemaji hajui kwamba si kweli au alikosea mwenyewe.
Aina za uwongo
Augustino wa Hippo alikuwa kati ya wataalamu wa kwanza waliofanyia uwongo utafiti . Katika kitabu chake "Kuhusu uwongo" ("De Mendacio") aliorodhesha aina nane za uwongo kama vile
Uwongo kuhusu mafundisho ya dini
Uwongo unaoleta hasara kwa mtu bila kumsaidia yeyote
Uwongo unaosababisha hasara kwa watu kadhaa na kuwasaidia wengine
Uwongo unaosimuliwa kwa furaha ya uwongo au kama mzaha
Uwongo unaotolewa kwa kumfurahisha mtu wakati wa maongezi
Uwongo usiomwudhi mtu lakini unaokoa uhai wa mtu
Uwongo usiomwudhi mtu na unaokoa heshima ya mtu
Uwongo usiomwudhi mtu na kumsaidia mtu

Kwa uchanganuzi huo je uongo ni sehemu muhimu ya maisha....? na je kuna mtu anaweza kuishi bila ya kutumia uongo kwenye maisha yote duniani....? ingawa kunasemwa uongo ni dhambi na ukweli ni haki na haiwezi kupotezwa na aina yoyote ya uongo

swali langu ni je kuna mtu yoyote (isipokuwa mitume wa mungu) akakiri kuwa hajawahi sema uongo maisha yake yote...? na kama hakuna ni kwanini tunapogundua tumedanganywa huwa tunachukia na kuwa na hasira na viapizo vya kulipa kisasi....?
 
Viongozi wanapokuwa waongo athari yake ni kubwa tofauti na mtu wa kaiwaida na hurudisha maendeleo ya taifa nyuma , Taifa lenye viongozi waongo ni hatari kwa maendeleo...
 
Ila uongo ni muhimu sana wakati mwingine mkiwa wengi mkaishiwa maneno kinachofata ni habari za uongo..uongo unaburudisha,uongo unafurahisha,uongo unaokoa,uongo unakarahakisha ila huwezi kuepuka uongo usipodanganywa utadanganya tunao uongo kila siku lakini kikubwa UONGO NI DHAMBI.. mtoa mada umenikumbusha rafiki yangu mmoja akikwambia maneno kumi la ukwel moja au hakuna kabisa ahahaah
 
Wanasema, ukiwa muongo usiwe msahaulifu....ni kanuni kuu ya utumiaji wa uongo , Wanasiasa wengi ni waongo wasahaulifu
 
Vipiuu uongowa sasa wa milioni kumi? Maana ule alio mzungumzia maMvi kwasasa anaupaka rangi. Au ndio tusahau deni letu la NHC. DJ bring back our money hatutaki porojo.
 
*Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.
*Penye ukweli uongo unakaa pembeni
*Uongo ni dalili ya mtu mnafiki
*Uongo unaleta chuki na ugomvi baadae
 
Nimeikuta mahali hii

Uongo ni tamko lisilo kweli lanalotolewa kwa makusudi. Mtu anayesema uwongo anajua au anahisi ya kwamba maneno yake si ya kweli lakini anataka msikilizaji wa maneno yake (au mpokeaji wa ujumbe wake) ayaamini kuwa kweli.
Mara nyingi uwongo hutumiwa kwa kusudi la kuficha kosa , aibu au tendo
haramu. Kusudi lingine ni kujipatia
faida au kuzuia hasara .
Uwongo hutazamwa kuwa tofauti na maneno yasiyo kweli lakini msemaji hajui kwamba si kweli au alikosea mwenyewe.
Aina za uwongo
Augustino wa Hippo alikuwa kati ya wataalamu wa kwanza waliofanyia uwongo utafiti . Katika kitabu chake "Kuhusu uwongo" ("De Mendacio") aliorodhesha aina nane za uwongo kama vile
Uwongo kuhusu mafundisho ya dini
Uwongo unaoleta hasara kwa mtu bila kumsaidia yeyote
Uwongo unaosababisha hasara kwa watu kadhaa na kuwasaidia wengine
Uwongo unaosimuliwa kwa furaha ya uwongo au kama mzaha
Uwongo unaotolewa kwa kumfurahisha mtu wakati wa maongezi
Uwongo usiomwudhi mtu lakini unaokoa uhai wa mtu
Uwongo usiomwudhi mtu na unaokoa heshima ya mtu
Uwongo usiomwudhi mtu na kumsaidia mtu

Kwa uchanganuzi huo je uongo ni sehemu muhimu ya maisha....? na je kuna mtu anaweza kuishi bila ya kutumia uongo kwenye maisha yote duniani....? ingawa kunasemwa uongo ni dhambi na ukweli ni haki na haiwezi kupotezwa na aina yoyote ya uongo

swali langu ni je kuna mtu yoyote (isipokuwa mitume wa mungu) akakiri kuwa hajawahi sema uongo maisha yake yote...? na kama hakuna ni kwanini tunapogundua tumedanganywa huwa tunachukia na kuwa na hasira na viapizo vya kulipa kisasi....?
Kweli uongo haufai. Nashukuru umenipa exposure kuhusu hicho kitabu hicho nimeshadownload naanza kesho kukisoma. Namwelewa sana St. Augustine of Hippo.
 
Shetani ndio muongo namba moja kwa mujibu wa vitabu vya Dini , na waongo wanaoudhi kwa udanganyifu wao ni haya makampuni ya mitandao ya simu za mkononi eti namba yako imechaguliwa kushinda milioni kadhaa tuma neno kwenda namba....! huo ni ulaghai wa kukuingiza kwenye matumaini ya uongo
 
Back
Top Bottom