Speed of light
JF-Expert Member
- Nov 8, 2014
- 313
- 284
Nimeikuta mahali hii
Uongo ni tamko lisilo kweli lanalotolewa kwa makusudi. Mtu anayesema uwongo anajua au anahisi ya kwamba maneno yake si ya kweli lakini anataka msikilizaji wa maneno yake (au mpokeaji wa ujumbe wake) ayaamini kuwa kweli.
Mara nyingi uwongo hutumiwa kwa kusudi la kuficha kosa , aibu au tendo
haramu. Kusudi lingine ni kujipatia
faida au kuzuia hasara .
Uwongo hutazamwa kuwa tofauti na maneno yasiyo kweli lakini msemaji hajui kwamba si kweli au alikosea mwenyewe.
Aina za uwongo
Augustino wa Hippo alikuwa kati ya wataalamu wa kwanza waliofanyia uwongo utafiti . Katika kitabu chake "Kuhusu uwongo" ("De Mendacio") aliorodhesha aina nane za uwongo kama vile
Uwongo kuhusu mafundisho ya dini
Uwongo unaoleta hasara kwa mtu bila kumsaidia yeyote
Uwongo unaosababisha hasara kwa watu kadhaa na kuwasaidia wengine
Uwongo unaosimuliwa kwa furaha ya uwongo au kama mzaha
Uwongo unaotolewa kwa kumfurahisha mtu wakati wa maongezi
Uwongo usiomwudhi mtu lakini unaokoa uhai wa mtu
Uwongo usiomwudhi mtu na unaokoa heshima ya mtu
Uwongo usiomwudhi mtu na kumsaidia mtu
Kwa uchanganuzi huo je uongo ni sehemu muhimu ya maisha....? na je kuna mtu anaweza kuishi bila ya kutumia uongo kwenye maisha yote duniani....? ingawa kunasemwa uongo ni dhambi na ukweli ni haki na haiwezi kupotezwa na aina yoyote ya uongo
swali langu ni je kuna mtu yoyote (isipokuwa mitume wa mungu) akakiri kuwa hajawahi sema uongo maisha yake yote...? na kama hakuna ni kwanini tunapogundua tumedanganywa huwa tunachukia na kuwa na hasira na viapizo vya kulipa kisasi....?