Unyama -unyamani!

pmwak

Member
Mar 13, 2013
26
3
Jamaa kamuaga mkewe kuwa anaenda semina Songea kwa wiki nzima kumbe hana lolote kahamia kwa mchuchu nyumba ya pili toka kwake. Kachukua taxi kazunguka mtaa akajitoma ndani ya nyumba ya jirani. Siku ya kwanza akalala, asubuhi alipoamka akaamua kuchungulia kwake kukoje, si akamuona jamaa yuko nje ya nyumba yake kavaa taulo lake anapiga mswaki bila wasiwasi wowote. Akapiga ukelele, 'Allo we nani?', Jamaa akajibu, 'Ahhh mshikaji mambo ya mjini, mume wa huyu demu kasafiri kaenda Songea huko mi ndo navinjari hapa'. Mume akajibu kwa uchungu, Shenzi mkubwa, ngoja nirudi toka Songea nikikukuta nakuuwa'

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Umeonaaa eee hehe pmwak noma umenichekesha best ukila vya wenzio usiogope na vyako kuliwa chezea vya kuiba hahahah

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ukiona mwenzio kanyolewa zako tia maji hahahahahhhaha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
ha ha ha kwe kwe kwe kwi kwi kwi kwa kwa kwa...........Kipimo alichompimia mke wake, ndicho alichopimiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom