Ungekuwa ni wewe ungechukua uamuzi gani?

Mtoa mada usituone sisi wajinga.
Stori zako za kutunga peleka shule za msingi humu ni great thinkers acha upumbavu.
 
Siku zote mke wangu amekuwa akiniambia kuwa ananipenda sana kitu kizuri zaidi amekuwa akinionyesha upendo huo, jambo ambalo limenifanya nijivunie kuwa naye siku zote siku moja nikaamua kumtania kwani tumezoea kutaniana, na siku zote amekuwa akifurahia utani wangu.

Nikamtania, ‘mke wangu, nimefukuzwa kazi na kibaya zaidi wamesema nitafirisiwa nyumba pamoja na gari zangu ili kufidia hasara ya kampuni mke wangu aliniangalia kwa ukali, kitu ambacho hakijawahi kutokea hata siku moja, kisha akanifyonya kwanza kabisa nilishangaa, mke wangu ananifyonya! Haijawahi tokea tangu tuanze mahusiano yetu, ila nikaona huenda tu ame-panick kwa sababu ya taarifa niliyompa.

Basi akaenda zake kulala na usiku mzima hakutaka kuniongelesha kabisa asubuhi kulipokucha nilishangaa kuona mke wangu amekusanya vitu vyake nje, nikamuuliza mbona anatoa vitu nje? Akanijibu hawezi tena kuishi na mimi kwani hawezi kuishi na mwanaume ambaye hana kazi, pesa, nyumba wala gari.

Nikamwambia naomba uniachie mwanangu basi, akanijibu kwa ukali, huyu sio mwanao na hapa unaponiona nataka kuelekea kuishi kwa baba wa mtoto wangu kichwa changu kilichanganyikiwa, sikutegemea kama utani ule ungeweza kuzua yote yale nikaamua kumuita mke wangu niongee naye kumjulisha kuwa nilikuwa namtania tu.

Nikamwambia, ‘mke wangu, pole sana nilikuwa nakutania tu ukweli ni kwamba nimepandishwa cheo kazini, na pia nimepewa nyumba nyingine kubwa zaidi ya hii pamoja na gari zuri zaidi la kutembelea, hivyo kesho tunahamia nyumba nyingine ambayo ni nzuri sana’.

Huwezi amini, mke wangu aliruka juu kwa furaha akanikumbatia na kunipa mabusu tele huku akisema, ‘nakupenda sana mume wangu kipenzi, siku zote za maisha yangu sijawahi kujuta kuwa nawe naomba unisaidie kurudisha vitu ndani’
nikamsaidia kuingiza vitu vyote ambavyo alikuwa ametoa tulipomaliza, nikamuuliza kwa upole, mke wangu ina maana kweli ndio ulikuwa unaondoka?

Akanijibu, ‘hapana mume wangu, nilikuwa nakutania tu k namna ninavyokupenda nisingeweza kukuacha peke yako’
tayari tumehamia nyumba mpya, na maisha yamekuwa bora zaidi kuliko mwanzoni kutokana na kupandishwa cheo lakini akili yangu bado inafikiria kitendo kile na pia maneno aliyoniambia juu ya mtoto hivi hapa kuna upendo kweli? na ungekuwa ni wewe ungefanyaje? tupia comment yako hapo chini...!
Kaka kua makini unapendwa sababu ya Nyumba na Gari. Cku ukifulia ataondoka kweli. Ww umeoa Gold digger
 
Tatizo matani mengine yanapita mipaka, utani gani huo...
Hata nikiwa naishi kwa mzee wangu yeye ndo nguzo ya family.. Alafu siku aje kunambia kafukuzwa kazi, atanilet down kabisa. Maana hyo ni dalili ya kuanza kula majani
Ila kumbuka hyo ni unconditional love
 
Siku zote mke wangu amekuwa akiniambia kuwa ananipenda sana kitu kizuri zaidi amekuwa akinionyesha upendo huo, jambo ambalo limenifanya nijivunie kuwa naye siku zote siku moja nikaamua kumtania kwani tumezoea kutaniana, na siku zote amekuwa akifurahia utani wangu.

Nikamtania, ‘mke wangu, nimefukuzwa kazi na kibaya zaidi wamesema nitafirisiwa nyumba pamoja na gari zangu ili kufidia hasara ya kampuni mke wangu aliniangalia kwa ukali, kitu ambacho hakijawahi kutokea hata siku moja, kisha akanifyonya kwanza kabisa nilishangaa, mke wangu ananifyonya! Haijawahi tokea tangu tuanze mahusiano yetu, ila nikaona huenda tu ame-panick kwa sababu ya taarifa niliyompa.

Basi akaenda zake kulala na usiku mzima hakutaka kuniongelesha kabisa asubuhi kulipokucha nilishangaa kuona mke wangu amekusanya vitu vyake nje, nikamuuliza mbona anatoa vitu nje? Akanijibu hawezi tena kuishi na mimi kwani hawezi kuishi na mwanaume ambaye hana kazi, pesa, nyumba wala gari.

Nikamwambia naomba uniachie mwanangu basi, akanijibu kwa ukali, huyu sio mwanao na hapa unaponiona nataka kuelekea kuishi kwa baba wa mtoto wangu kichwa changu kilichanganyikiwa, sikutegemea kama utani ule ungeweza kuzua yote yale nikaamua kumuita mke wangu niongee naye kumjulisha kuwa nilikuwa namtania tu.

Nikamwambia, ‘mke wangu, pole sana nilikuwa nakutania tu ukweli ni kwamba nimepandishwa cheo kazini, na pia nimepewa nyumba nyingine kubwa zaidi ya hii pamoja na gari zuri zaidi la kutembelea, hivyo kesho tunahamia nyumba nyingine ambayo ni nzuri sana’.

Huwezi amini, mke wangu aliruka juu kwa furaha akanikumbatia na kunipa mabusu tele huku akisema, ‘nakupenda sana mume wangu kipenzi, siku zote za maisha yangu sijawahi kujuta kuwa nawe naomba unisaidie kurudisha vitu ndani’
nikamsaidia kuingiza vitu vyote ambavyo alikuwa ametoa tulipomaliza, nikamuuliza kwa upole, mke wangu ina maana kweli ndio ulikuwa unaondoka?

Akanijibu, ‘hapana mume wangu, nilikuwa nakutania tu k namna ninavyokupenda nisingeweza kukuacha peke yako’
tayari tumehamia nyumba mpya, na maisha yamekuwa bora zaidi kuliko mwanzoni kutokana na kupandishwa cheo lakini akili yangu bado inafikiria kitendo kile na pia maneno aliyoniambia juu ya mtoto hivi hapa kuna upendo kweli? na ungekuwa ni wewe ungefanyaje? tupia comment yako hapo chini...!
Okomi Zoba | Wewe Mjinga
 
Back
Top Bottom