Unaweza kuchagua Rais kutoka chama usichokipenda?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,641
46,283
Ukiwa kama mpinzani au mtu asiye na chama lakini haukikubali chama cha CCM ni mtu gani wa CCM akiwekwa kugombea urais utampigia kura kwa maslahi mapana ya nchi?

Ukiwa kama mwana CCM kindakindaki ni mtu gani wa upinzani akigombea Urais unaweza kumpigia kura kwa maslahi mapana ya nchi
 
Ni kawaida kabisa Mwananchi kumchagua Magu CCM Urais, Mbunge Professor J, CHADEMA, Diwani akamchagua Kutoka chama Cha Rungwe. Hiyo ni u haguzi wa 2015.
 
Kura yangu ya kwanza ni 2005 kwa Mbowe nikiwa mwana Chadema Kindakindaki, kura ya pili kwa Slaa 2010. Kura yangu ya kwanza na ya mwisho kwa CCM ni 2015 na 2020 kwa Magufuli!

Japo sikuwahi kuwahi kuielewa CCM wakati wote, lakini tokea kuzijua siasa, nilitamani siku moja Magufuli awe rais. Alivyo teuliwa ni kama ndoto zangu zikitimia.

Bado namuombolezea aisee, apumzike kwa amani.
 
kura yangu ya kwanza ni 2005 kwa mbowe nikiwa mwana chadema kindakindaki, kura ya pili kwa slaa 2010 kura yangu ya kwanza na ya mwisho kwa ccm ni 2015 na 2020 kwa magufuli!
japo sikuwahi kuwahi kuielewa ccm wakati wote lakini tokea kuzijua siasa nilitamani siku moja magufuli awe rais, alivyo teuliwa ni kama ndoto zangu zikitumia.
bado namuombolezea aisee, apumzike kwa amani.
2015,

Magu alichaguliwa Kwa usafi wake, Si Kwa chama chake.
 
Ukiwa kama mpinzani au mtu asiye na chama lakini haukikubali chama cha CCM ni mtu gani wa CCM akiwekwa kugombea urais utampigia kura kwa maslahi mapana ya nchi?

Ukiwa kama mwana CCM kindakindaki ni mtu gani wa upinzani akigombea Urais unaweza kumpigia kura kwa maslahi mapana ya nchi
Ujinga wa Watanzania ndio huu, kuchagua mtu kwa kuwa anatoka chama unachokishabikia hata akiwa poyoyo kiasi gani. Siku tutakapouondoa ujinga tutaenda mbali sana.
 
Chini ya Katiba hii iliyopo, yeyote atakayeteuliwa atamezwa na mfumo, wapo wengi wanaoona Magufuli alikuwa jembe, lakini hawakumbuki Magufuli nae alitengeneza kikundi chake cha upigaji.

Hapo kwanza Katiba mpya ipatikane, Rais awe responsible kwa matendo yake, utaona wote kati ya hao uliowataja watafaa kutuongoza, kwasababu watawajibishwa wakikosea, huu uhuru alionao Rais sasa, unaifanya hiyo taasisi ionekane ya kututawala zaidi badala ya kututumikia.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Leo nahisi kuna tafiti zinaendelea kuhusu uchaguzi ujao maana nyuzi za uraisi zimetaradadi kwa kasi! Anyway Aliekutuma umfanyie huu utafit anafuatilia uzi kwa umakini sana akisubiri jina lake litajwe
 
Leo nahisi kuna tafiti zinaendelea kuhusu uchaguzi ujao maana nyuzi za uraisi zimetaradadi kwa kasi! Anyway Aliekutuma umfanyie huu utafit anafuatilia uzi kwa umakini sana akisubiri jina lake litajwe
Sidhani kama ametumwa,

Tanzania ni Nchi ambayo, Rais akishakalia KITI hicho , wananchi hawawezi mtoa awapo madarakani Kwa namna yoyote hata akiboronga vp, labda kifo tu.

Ndomana ukikaribia uchaguzi wananchi Huwa wanakuwa na shauku sana ya Mabadiliko.
 
Back
Top Bottom