Unaupimaje utendaji wa Waziri wa uchukuzi?

“Jamani fedha zimetengwa na mmekabidhiwa mnaziweka ofisini kama mapambo huku wafanyakazi wanafanya kazi ngumu halafu hamuwalipi, mimi nataka kusikia fedha zimeisha tujue jinsi ya kuongeza, kinyume na hapo mnataka niwafukuze kazi, tena mwambie huyo Shekimweli nataka ifikapo mwezi Oktoba naanza kutoa huduma hii,” alisema na kuongeza:

Come october hii project isipoanza ivi mtamlaumu waziri au viongozi wa mashirika haya!UKishapata jibu utajua ni kwa nini alifanya surprise visit imagine hela wanazo na wafanyakazi hawapewi posho angekuwa ofisini angejua hili
 
nyie pigeni majungu kama kawaida lakini Mwakyembe is doing a very good job.

ni vizuri kusupport kuliko kufikiria kila wakati kupinga maana wabongo walivyo hata treni zikianza utasikia oooh msipande
 
Utendaji wa waziri uchukuzi ni wa chini sana (extremely poor). Amejigeuza kuwa CEO, mkaguzi, abiria,karani wa mashirika/idara zilizo chini ya wizara yake na mbaya zaidi anaonekana kujikita kwenye trivial issues! Wizara (serikali) inatakiwa iaandae mazingira mazuri kwa mashirika kufanya kazi hii ni pamoja na kuandaa policy, sheria na kusimamia, lakini anachofanya waziri kwa sasa ni micro-manage to the last small issue.

Sijamsikia anaongea susbtantive programme au mkakati na wala sieweli anataka ku-achieve kitu gani?
 
Waswahili wanasema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza(sina uhakika kama sijabadili maneno)!
Kiboko yake ni waziri anayeshughulikia barabara ingawaje kipande cha Somanga kimemshinda!
 
mosagane Kichekesho ni kuwa juzi nilipanda basi Ubungo bado nikatozwa elfu tanoi zaidi ya nauli sasa mizunguko yake hapo kituo cha Ubungo ina tija gani?

Baada ya hapo wewe ulichukua hatua gani? pamoja na abiria wenzako? wajinga ndiyo waliwao! huyo waziri bora akae kimya tu hakuna zuri nchi hii! Ibeni tu mkifanya kazi mtaishia kutukanwa tu na kukejeliwa na akina mosagane!
 
kajembe usichojua bosi kulingana na sheria lazima awe mzambia na Mwakyembe hana ubavu wa kumwondoa.....sijui tangia lini wazambia wakawa ni ndugu zangu.................la muhimu hapa ni kuwa tutaendelea kukosoa hadi majambozi yatakapowekwa sawa ni haki yetu ya kikatiba...................aache kuingilia watendaji ambao wamewekwa kisheria na hata katibu mkuu wake hamshirikishi kama ni kasi ya kwenda Ikulu hatafika........

Kwahiyo siku hizi kufanya kazi kwa bidii ni kasi ya Ikulu? Lowassa anawapotosha sana!hahahahahah!
 
masikitiko tatizo ni kuwa anavunja sheria zilizopo kwa kuwaingilia wasaidizi wake wakati sheria hiyohiyo inampa madaraka ya kuiondoa bodi kama anaona imeshinwa kazi.....................swali kwanini haiondoi bodi anabakia kuingilia majukumu yake kama siyo kuleta vurugu kazini na kutamba mbele ya wapagasi anafikiri ndiyo uwaziri ulivyo?

sasa kama wamelala usingizi wa pono aache tu?
 
Hili ndo tatizo ambalo linamkabili hata rais wetu wa nchi ni kutokana na watendaji wake kukakaa kama mizoga maofisini wakati mambo yanaenda kombo huko. Mnataka afanyaje? acheni afanye kama anavyoweza nchi hii watu wamejisahau sana na kuona taasisi/makampuni mashirika ya uma kama ya kwao. Mia namuunga mkono acha achape kazi awezavyo wizara ya uchukuzi ni moja ya wizara ambayo imeoza sana hakuna hata kitengo kimoja ambacho kiko ndani ya wizara hiyo kinafanya vizuri. Lakini tunajuwa katika wizara ile mchawi ni nani. Lema alikuwa ameota mizizi Tanroads lkn Magufuli alimng'oa. Inakuwa je malori yanasafirisha maizigo na mafuta kwenda zambia alihali reli ya tazara ipo? hivi wewe bosi mzima unakaa ofisini unadai mshahara for what wakati hamuuinginzi na oportunities mnaziacha tu?

Kuna taasisi ambazo sasa zinahitaji reconstruction ya hali ya juu ikiwemo kuwaondoa na bodi zao, taasisi hizo ni: mamlaka ya bandari, trc, tazara, chuo cha mabaharia, nk. Hivi vyote vilitajwa ktk ripoti ya CAG
 
masikitiko tatizo ni kuwa anavunja sheria zilizopo kwa kuwaingilia wasaidizi wake wakati sheria hiyohiyo inampa madaraka ya kuiondoa bodi kama anaona imeshinwa kazi.....................swali kwanini haiondoi bodi anabakia kuingilia majukumu yake kama siyo kuleta vurugu kazini na kutamba mbele ya wapagasi anafikiri ndiyo uwaziri ulivyo?

Hata Angeondoa hiyo bodi bado ungelalamika tu! Uwaziri ndivyo ulivyo mbona hata Lowassa unae mwabdu sana alikua hivyo?
 
siku yake itafika tu huyu mnafiki...... hata akiumwa homa au akijikwaa huwa anaanza kutangaza kuwa wabaya wake ndio

wamesababisha......na anafanya hivyo akijua kuwa watz wengi ni vilaza

Kweli siyo vilaza tunawajua mmetumwa na nani!Mwakyembe usisikilize fanya kazi.
 
Boflo ninaafiki hoja zako zote.......................huyu Mkuu anafikiri nchi yaendeshwa kwa vitisho na kudhalilishana hadharani..............................kama yeye kweli ni kibosile kwani atoe matambo kwa wadogo wa bosi kwa nini asimfuate ofisini na kumtambia kule kama siyo uabbaishaji na kutafuta umaarufu kwenye dirisha la vyombo vya khabari?

Mambo bila kufanya hadharani ndiyo maana tumeibiwa madini sababu ya tamaduni wa hovyo wakuficha mambo,Mtu akizembea anaambiwa hadharani,uzembe wao unawaumiza watu hadharani!hiyo ndiyo dawa inayofaa hapa Tanzania,zama za kuonyana mafichoni zinaanza kupitwa na wakati!
 
mlallilaN nimekuelewa wewe na wengineo ambao kutokana na kuzidiwa na kero mwaona kheri njia za mkato hata kama hazitufikishi tutakakokwenda......................kuhusu nilifanya nini msafiri kafiri......................lengo langu ni kufika A-Town na sina muda wa kuingia gharama kubwa zaidi za kutatua matatizo ambayo Waziri mhusika alivalia njuga na sasa yamemshinda yako palepale........................hata hili la kuripoti hapa jamvini ni hatua ya kuelimisha umma ya kuwa tatizo bado lipo palepale.........................na kuendeleza mjadala wa kutafuta majibu yake............

Njia ndefu ndiyo zimetufikisha hapa,wametajirika wachache na wageni sababu ya njia mnazo zifagilia!Mtu anaiba anaangaliwa tu kisa hakuna ushaidi! wezi wote smart wanatamba hapa Tz,maana kuna njia za kufuata, Ujinga tu!
 
Anatakiwa kuweka system. Corporate strucure ambayo itakuwa na line of command and reporting strucre iliyo wazi. Yeye natakiwa kutengeneza system jinsi ya kupata reort mbalimbali ambazo atakuwa natumia kupima utendaji wa walio chini yake huku akitoa carrot and stick inavyotakiwa. Mfano anaweza fanay upembenuzi yakinifu kujua matatizo yote yaiyo kwenye wizara yake na kupata jinsi ya kutatua. SUMATRA wapo chini yake nk. Yafaa awatumie hao la sivyo atafeli muda si mrefu.

Mkuu akitumia mbinu hizi za kwenye vitabu hatafika mbali, kumbuka Wizara yenyewe ina viongozi ambao wamekaa pale kwa muda mrefu hivyo wanaweza kumuwekea spana akajikuta anakwama. Cha muhimu hapa ni kubadilisha viongozi hao wawahamishie Wizara nyingine, mambo ya kutegemea ripoti zinazo andikwa na watu walio zoeana au za kutunga tu aziwezi kubadirisha mind set za Viongozi walio katika Wizira hiyo na mashirika yaliyo chini yake.

Mimi sioni kama leadership style ya Dr.Mwakyembe ina walakini wowote, cha umuhimu hapa ni kumpa moyo na ushauri na sio kumlahumu.
 
Baada ya hapo wewe ulichukua hatua gani? pamoja na abiria wenzako? wajinga ndiyo waliwao! huyo waziri bora akae kimya tu hakuna zuri nchi hii! Ibeni tu mkifanya kazi mtaishia kutukanwa tu na kukejeliwa na akina mosagane!

kajembe hivi msafiri umesahau ni kafikiri............anachotaka ni kwenda atakako hana uwezo wa kugharimia uchunguzi au kudhibiti ufisadi kazi ambayo taasisi zipo na wahusika wanakula hela bila ya kutekeleza majukumu yao..........kuripoti hapa ni sehemu ya mchango.............
 
Last edited by a moderator:
Mkuu akitumia mbinu hizi za kwenye vitabu hatafika mbali, kumbuka Wizara yenyewe ina viongozi ambao wamekaa pale kwa muda mrefu hivyo wanaweza kumuwekea spana akajikuta anakwama. Cha muhimu hapa ni kubadilisha viongozi hao wawahamishie Wizara nyingine, mambo ya kutegemea ripoti zinazo andikwa na watu walio zoeana au za kutunga tu aziwezi kubadirisha mind set za Viongozi walio katika Wizira hiyo na mashirika yaliyo chini yake.

Mimi sioni kama leadership style ya Dr.Mwakyembe ina walakini wowote, cha umuhimu hapa ni kumpa moyo na ushauri na sio kumlahumu.

Bukyanagandi uko sahihi afanye kazi na wenzie kwa kushirikiana nao asidhani yeye ndiye mjuaji nwakati akipewa spana aonyeshe inatumika wapi atatumbua macho tu hajui cha kufanya.....................asifikiri kazi zinakwenda kwa vitisho........
 
Last edited by a moderator:
Njia ndefu ndiyo zimetufikisha hapa,wametajirika wachache na wageni sababu ya njia mnazo zifagilia!Mtu anaiba anaangaliwa tu kisa hakuna ushaidi! wezi wote smart wanatamba hapa Tz,maana kuna njia za kufuata, Ujinga tu!

kajembe ninaamini unafahamu fika waziri hana mamlaka ya kukamata mwizi zaidi ya kumshitaki polisi............kama anawajua wezi aache kuwatishia au kuchukua sheria mkononi akawaripoti kunakohusika..................
 
Last edited by a moderator:
Nikweli kwasababu si hampendi ukweli! mnapenda wezi wanaoinamisha vichwa chini!

kajembe hata Mwakyembe hajamtuhumu yeyote ndani ya wizara yake kuwa ni mwizi hizi tuhuma mwenzetu unazitoa wapi? Kama una ushahidi harkisha polisi wachukue hatua stahiki
 
Last edited by a moderator:
Mambo bila kufanya hadharani ndiyo maana tumeibiwa madini sababu ya tamaduni wa hovyo wakuficha mambo,Mtu akizembea anaambiwa hadharani,uzembe wao unawaumiza watu hadharani!hiyo ndiyo dawa inayofaa hapa Tanzania,zama za kuonyana mafichoni zinaanza kupitwa na wakati!
[MENTION]
Kajembe[/MENTION] tangia waziri aende kituo cha mabasi cha Ubungo na kufanya mambo kwa "uwazi" hivi dhuluma pale imekwisha? Au vitisho kwa mzambia mkandawire ambaye huteuliwa na Raisi wa Zambia kuwa atamfuta kazi wakati mamlaka hayo hana kama siyo utapeli wa kisiasa ni nini?
 
Utendaji wa waziri uchukuzi ni wa chini sana (extremely poor). Amejigeuza kuwa CEO, mkaguzi, abiria,karani wa mashirika/idara zilizo chini ya wizara yake na mbaya zaidi anaonekana kujikita kwenye trivial issues! Wizara (serikali) inatakiwa iaandae mazingira mazuri kwa mashirika kufanya kazi hii ni pamoja na kuandaa policy, sheria na kusimamia, lakini anachofanya waziri kwa sasa ni micro-manage to the last small issue.

Sijamsikia anaongea susbtantive programme au mkakati na wala sieweli anataka ku-achieve kitu gani?

Mkuu FJM yaani Wizara ya uchukuzi ilivyo hivi sasa, mimi naona Dr.Mwakyembe hata akiwa a jack of all TRADE ni sawa tu. utendaji wa wizara hii na mashirika yake ni dismal kabisa, aibu tupu mkuu!

Mwache Waziri aendeshe Wizara na mashirika yake kipolisi polisi na avunje bodi zote za mashirika ya uchukuzi na bandari alafu watangaze nafasi za Board members kwa kutumia a reputable recruiting consultant/agency na wawe vetted properly wasilete mambo ya kujuana na blatant nepotism ambayo hiko rampat katika mashirika hayo, operation hiyo aifanye kwa mwaka mmoja na ushee hivi, baada ya hapo ndio wafuate conventional modus operandi - yaani kuandaa mazingira mazuri kwa mashirika kufanya kazi and what have you, sio sasa hivi mkuu.

Dr. Mwakyembe amepewa Wizara ambayo ilikuwa imejisahau SANA, raia wenye nia njema na TAIFA letu wanapashwa kumpa ushauri mzuri na sio kumlahumu au kutaka kumkatisha tamaa.
 
Back
Top Bottom