unatakiwa kuomba ruhusa au kuaga

........... Yaani wewe!! hata sikuwezi kwa ukorofi

MJO net kwangu imekuwa slow sana, nikumbushe kesho nikiingia huku nikugee kisa kingine ili jue watu tunavyogangamala na hawa binadamu, unakomaa nae tu, tchao mami, kesho mungu akipenda.
 
Kuaga kuna beba vitu gani?
Kuomba ruhusa nako?
Kuaga ni kutoa taarifa ya kile unachotaka kukifanya. Unakuwa tayari umejiamulia, kumbe unamfahamisha tu mwenzako ajue kinachoendelea. Kuomba ruhusa ni kuomba ridhaa ya mwenzio ili abariki unalotaka kufanya au pia alikatae kama kukiwa na sababu ya msingi. Na kama anakataa mara nyingi atakuambia sababu ni nini ya kutokukubaliana nawe.
 
tofati yetu ni kwamba cc tunaweza kuomba tukanyimwa lakini nyie ni kama unamtaarifu tu mwenzako kuna kuna hili na lile na hawezi kukuzuia/kunyima.
[/COLOR]
hapo mummy uko right asilimia mia moja , ila nitakwambia kitu kimoja mahusiano yeyote katika ndoa yanategemea nyinyi kabla ya ndoa mlikuwa na utaratibu gani, kama mwanamke ulikuwa na mazoea ya kumuonyesha mwenzio mapenzi ya uoga na kujionyesha unnecessarly that u r inferior usitegemee kubadilika ukishaingia kwenye ndoa, lakini kama mnaweka base ya understanding tangu mwanzo wa mahusiano kila mmoja atauona umuhimu wa mwenzie, bilieve me i know wanaume wanabadilika mkishaona lakini kama utamwacha afanye anavyotaka kabla ya kuoana ndio ataendelea kukuburuza baada ya ndoa , lakini mkiweka heshima mbele kwa kila mmoja wenu kabla ya ndoa unakuwa na uwezo hata wa kumuuliza mpenzi wako wat happened mbona mwanzo hukuwa hivyo ? na kunakuwa na chance ya mwenzi wako kujisuta na kukumbuka kweli sikuwa hivyo akajirekebisha , ndo maana kuna baadhi ya ndoa zina miaka lakini utafiri wameoana jana jinsi wanavyoheshimiana na kupendana mpaka MIAFRIKA mingine inasema haiwezekani huyu mwanaume kalishwa limbwata kumbe hawajui walikoanzia....
 
Unajua kwa sisi wanawake , mwanaume anataka aombwe ruhusa, fulani naomba ruhusa nataka kesho niende kwenye sherehe, anaweza akubali au akatae, mimi nakataa inatakiwa uage tu naenda sehemu fulani kutoa taaarifa siyo lazima uombe ruhusa huo ni ukoloni mamboleo,

Joy kauli nzito hiyo nayo! Unaposema uage tu si sawa nadhani, pengine jamaa anakuhitaji kwa muda huo utakao kuwa haupo je, kwanini usimshirikishe tangu mwanzo ulipoifikiria hiyo safari? Cha msingi ni wote kushirikishana nadhani, na najua unasema hivyo sababu unaweza kuamua cha kufanya unapotaka, je kama unapanga kwenda safari na unamtegemea yeye akupe nauli utaoga unaulamba kisha ndio unamwambia nipe nauli naenda sehemu fulani? Hata kwa mume nae ni busara kuomba ruhusa ikibidi
 
hapo mummy uko right asilimia mia moja , ila nitakwambia kitu kimoja mahusiano yeyote katika ndoa yanategemea nyinyi kabla ya ndoa mlikuwa na utaratibu gani, kama mwanamke ulikuwa na mazoea ya kumuonyesha mwenzio mapenzi ya uoga na kujionyesha unnecessarly that u r inferior usitegemee kubadilika ukishaingia kwenye ndoa, lakini kama mnaweka base ya understanding tangu mwanzo wa mahusiano kila mmoja atauona umuhimu wa mwenzie, bilieve me i know wanaume wanabadilika mkishaona lakini kama utamwacha afanye anavyotaka kabla ya kuoana ndio ataendelea kukuburuza baada ya ndoa , lakini mkiweka heshima mbele kwa kila mmoja wenu kabla ya ndoa unakuwa na uwezo hata wa kumuuliza mpenzi wako wat happened mbona mwanzo hukuwa hivyo ? na kunakuwa na chance ya mwenzi wako kujisuta na kukumbuka kweli sikuwa hivyo akajirekebisha , ndo maana kuna baadhi ya ndoa zina miaka lakini utafiri wameoana jana jinsi wanavyoheshimiana na kupendana mpaka MIAFRIKA mingine inasema haiwezekani huyu mwanaume kalishwa limbwata kumbe hawajui walikoanzia....

hapo sawa kabisa,

Mimi binafsi nafahamu ndoa moja iliyoota mbawa kutokana na kutokuelewana kwenye haya masuala ya mwanamke/mwanaume kutaka kutoka

Ilivo ni kuwa mwanamke alikuwa mtu wa kujirusha sana viwanja, madisko, club, bendi za dansi..kifupi ni mtu wa kawaida kuonekana kwenye kumbi za starehe..sasa sijui ndiko walikokutana na mumewe, lakini baad aya ndoa binti akataka kuendeleza libeneke, hata pale ambapo mumewe alikuwa hapendi, ndo katika kulazimishana ikawa kupigana hadi ndoa imevunjika...binti anataka 'uhuru wake' na kumbe jamaa anataka mke 'wa kukaa ndani na kumsikiliza'.

Kumbe wangekuwa wameweka sawa tangu mwanzo haya wala yasingefika huku!
 
you are welcome!, wapitie kina WoS, MJ1 na wengineo, ntatoa ofa kwa wote.
actually mi ndio namtumia sms hapa mwanandoa mwenzangu mtarajiwa kwamba nina kikao na wanaJF, kila mtu aage kwake kunako husika, hatutaki kutoana manundu bure, wengine mmesema mnafuatiliana yendo zenu!.

hivi hayo mambo bado yapogo? nimecheka kweli.
 
Kutoka katika uzoefu wangu:

Kuaga huja pale ambapo ninakuwa ninatoka kwa jambo ambalo ni routine, sababu ya kuaga ni kutoa taarifa. Kwa mfano kwenda kazini, sokoni, kupeleka watoto shule nk

Ruhusa huja pale ninapotaka kwenda mahali au katika shughuli ambayo si sehemu ya routine. Na sababu kubwa ya kuomba ruhusu ni kupata ridhaa ya mwenzio. Kwa mfano, unapotaka kusafiri kwenda safari itakayochukua umbali mrefu au muda mrefu ni lazima upate consent ya mwenzako.

Kwa safari za kikazi hii hubeba semi-kuaga na semi-ruhusa.
Mara nyingi kama mtu huwa unasafiri mara kwa mara ni wazi basi mwenzio atakuwa anelewa mazingira hayo, na kama si safari ya ghafla basi utakuwa safari yako umeshaieleza ndani ya muda muafaka na siku ikifika huwa ni kuagana.
Lakini hata hivyo kama huna mazoea ya kusafiri mara kwa mara na ikatokea siku umepata safari ya ghafla ya kikazi, ni wazi utaeleza mazingira ya safari hiyo jinsi yalivyotokea na kuainisha the urgency iliyopo, binadamu wa kawaida huelewa! Lakini endapo kila siku safari zako ni ghafla-ghafla hapo unaweza kuleta utata, kwani kuna watu wengine wakishapatana na nyumba ndogo kuwa leo usiku utapita kwako basi hutunga safari za ghafla bin vuu!
 
Jamani kuaga muhimu hata kama unaenda kuoga,msalani,kokote pale lazima uage bana sasa unajiondokea kama kuku alafu nakukuta mazingira tata lakini ndo kwenye njia hiyo hiyo uliko kuwa unakwenda nitakwelewa sikuelewi hapo hapo talaka 3.

kama una mitara je
 
sio swal la kuaga tu! hata kusema ulipo pindi unapokuwa huko uliko baada ya kusema. kwa mfano umeaga unaenda gereji tangu asubuhi mpaka saa nane we kimya tu! hiyo kuaga yako itakuwa haina maana.
 
sio swal la kuaga tu! hata kusema ulipo pindi unapokuwa huko uliko baada ya kusema. kwa mfano umeaga unaenda gereji tangu asubuhi mpaka saa nane we kimya tu! hiyo kuaga yako itakuwa haina maana.

gkundi yaani hapa we ndo umegusa kabisa yaani mtu anawezakuaga mchana anaende kuonana na mtu ofcn ila hadi saa nane usiku kimyaaaaaa hata sms kusema kapitia wapi........... wanaume nao wangekuwa wanafanyiwa kitchen party bana !!
 
hapo sawa kabisa,

Mimi binafsi nafahamu ndoa moja iliyoota mbawa kutokana na kutokuelewana kwenye haya masuala ya mwanamke/mwanaume kutaka kutoka

Ilivo ni kuwa mwanamke alikuwa mtu wa kujirusha sana viwanja, madisko, club, bendi za dansi..kifupi ni mtu wa kawaida kuonekana kwenye kumbi za starehe..sasa sijui ndiko walikokutana na mumewe, lakini baad aya ndoa binti akataka kuendeleza libeneke, hata pale ambapo mumewe alikuwa hapendi, ndo katika kulazimishana ikawa kupigana hadi ndoa imevunjika...binti anataka 'uhuru wake' na kumbe jamaa anataka mke 'wa kukaa ndani na kumsikiliza'.

Kumbe wangekuwa wameweka sawa tangu mwanzo haya wala yasingefika huku!
yaaani weee acha tu haya mambo bwana yanataka kutukuza THREE C's yaani COMMUNICATION,COMPROMIZATION and COMMITMENT, sasa hizo mbili za kwanza ndio zinakuwaga ngumu , by my experience wanawake na wanaume wengi tu wana hilo tatizo.
kwenye communication bana mtu kumwambia mwenzie nini anapenda anaona ngumu ambapo inapelekeaga hata ndoa nyingine kuwa kwenye matatizo yakutoridhishana kwenye mapenzi kisa mmoja anaogopa kumwambia mwenziwe anapenda kushikwa wapi na vipi,
kwenye kucompromise ndo ishu hapo na mara nyingi ni sisi wanawake wenye hiyo weakness tunapenda sana kuwabadilisha wanaume zetu tukishakuwa kwenye mahusiano kitu ambacho hakiwezekani bila kutumia busara.you can not change mtu mwenye miaka zaidi ya 20 kuwa unavyotaka wewe for few months or years all you need to do ni kucompromise , jua weakness zake na tafuta njia ya kucope with them, au tafuta njia mmbadala ya kummbadilisha taratibu bila yeye kuwa offended ,
 
Naaam! endelea baada ya mkato naona bado hujafika mwisho.....
 
Unatakiwa kuomba ruhusa kwanza kisha ndio uage!

Ikibidi hata kwenda kuoga... wewe omba tu ruhusa, kisha angalia reaction ya mwenzako...!
 
we jamani huku kwetu nairobi lazima useme unatoka kwenda wapi, utakuwana nani na utarudi saa ngapi!!! Kinappings for ransoms are on the rise!!!!
 
Back
Top Bottom