Start-Menu
Member
- Sep 10, 2023
- 12
- 63
Walengwa ni hasa wale tunaonunua laptops zilizotumika lakini pia vyuo vinakaribia kufungua ni kipindi ambacho laptops zinanunulika sana.
Unaponunua Pc ni rahisi kukagua Ram, Hard Disk, Processor, Speaker, tachi, n.k. lakini wengi wanategemea kauli mali linapokuja suala la battery, utaambiwa tu “Battery ipo fresh” ila ukianza kuitumia mashine unajionea uhalisia battery inakaa nusu saa tu kwisha habari.
Kujua namna ya kupata makadirio ya battery inakaa muda gani fanya hivi.
1. Minya start kisha andika cmd, fungua command prompt
2. Andika cd desktop alafu minya enter.
3. Andika powercfg /batteryreport alafu minya enter.
4. Nenda kwenye desktop utaona file limeandikwa power cfg/battery report
5. Fungua file
6. Shuka mwisho kabisa kuna sehemu imeandika Since Os Install, angalia muda wa upande wa kushoto ndio makadirio ya muda ambao battery itakaa, (upande wa kulia ni makadirio laptop ilivyokua mpya, ni wachache sana wanaweza kununua laptop mpya, wengi hununua refurbished / mitumba)
Mfano hapa kwenye pc yangu imeandika 3:09:50, ni kwamba nkiichaji full, makadirio ya wastani naweza kuitumia mashine kwa masaa matatu, dakika 9 na sekunde 50.