Unapenda kuingia kwenye Ndoa Bora?

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,585
4,270
Mimi ni kijana (Mwanamme) mwenye umri wa kukaribia miaka 40 naishi kanda ya Kaskazini.
Historia yangu ya maisha ni ndefu kiasi ila kwa kifupi ni kuwa; nimetoswa na msichana niliyempenda na kumuamini sana kuwa angekuwa mwenza wangu.
Hii ilitokea baada ya kumsaidia kupata scholarship ya kwenda kusoma Holland kozi ya miaka mitatu (kuanzia mwaka 2007). Huyu msichana nilimpata wakati nipo chuoni….
Kwa kifupi ni kuwa nigharamikia mambo yote muhimu kwa safari ya nje ya nchi. Visa/ passport nk muda ulipofika alienda chuoni na tulikuwa na mawasiliano mazuri sana kwa mwaka wa kwanza (Facebk/skype na hata simu) ila yalienda yakipungua mwaka wa pili. Miezi ya katikati ya 2009 nilipata wakati mgumu sana kwani mara kadhaa usiku nawasha computer yangu nakuta yupo hewani kwenye Messenger ila niki chat anabakia kimya; baadae sana akinijibu anasema kuwa aliacha Comp. yake on akalala. Ilienda hivyo hivyo hadi mwishoni mwa mwaka (2009) akawa anadai mimi sina mapenzi ya kweli kwani sijawahi hata kuwa na wazo la kwenda kumtembelea chuoni kwake (huko Holland) nafikiri wanao jua Geography wanaweza kujua unavyosema unaenda kumasalimia mtu aliyeko East Holland unaongelea $$$ ngapi?
Iliniumia sana, kwani nilijua kabisa huo sio mwisho mzuri…iliendelea hivyo hivyo kwa malumbano madogo madogo hadi muda wa kurudi ukafika. Ile tar. Aliyo niambia angekuja hakuonekana na kila nikiimuuliza kuwa ameahirisha hadi lini anakwepa…
Baada ya kufuatilia kwao ( kwa kutumia mpambe) nikajulishwa kuwa amesha pata mtu mwingine raia wa nchi jirani na kwetu (walikutana huko chuoni) na wana tegemea kufunga ndoa.
....Nilijilaumu kwa kumpa nafasi ya kusoma….labda tungekuwa tumezaa naye mtoto????
Kinachoniumiza:
1. Nili dedicate mawazo yangu yote kwake sasa kwa umri huu (karibia 40yrs)nita anzaje tena kutafuta mchumba?
2. Wasichana wazuri ambao nafikiri nitamatch nao umri naona wengi wapo kwenye ndoa
3. Kama kuna bint decent anayejiamini na anahisi yupo tayari kuingia kwenye ndoa bora naomba ani pm
4.
Frankly I am desperately and I need your hands!
 
pole sana, ngoja nikusanye busara zangu na niondoe yale ma-brutal truzi yangu.

Pole, hakuna gumu kwa akili ya binadamu kama ukiamua.
 
lol! si unamuona Le Mutuz inadaiwa ana miaka 50 lakini bado ni mvulana :):) kutokana na matendo yake ya kivulana. Mie bado bana lakini siwezi kujiweka kwenye kundi la wavulana.

Hahaaaa Bubu my friend, we ushafikisha nini hiyo age? Manake unanitia shaka kidogo....
 
Wazee wenzio (waschana wazee) wako kibao tu, vuta pumzi mbavu utaipata tu kwani ujazeeka sana!
 
Pole sana, it could have been worse!
God's time is the best time, jichanganye, weka bandiko la kutafuta rafiki na omba Mungu akujalie tamanio la moyo wako.

I know it hurts a lot, lkn again it could have been worse!
 
Mi bado mtoto (itifaki izingatiwe in 20's) ila kila nikicheki threads inaonekana mademu wa chuo ni disaster. Sasa sijui itakuwaje huko niendako maana post nyingi utata mtupu.
 
Mimi ni kijana (Mvulana) mwenye umri wa kukaribia miaka 40.
Historia yangu ya maisha ni ndefu kiasi ila kwa kifupi ni kuwa; nimetoswa na msichana niliyempenda na kumuamini sana kuwa angekuwa mwenza wangu.
Hii ilitokea baada ya kumsaidia kupata scholarship ya kwenda kusoma Holland kozi ya miaka mitatu (kuanzia mwaka 2007). Huyu msichana nilimpata wakati nipo chuoni….
Kwa kifupi ni kuwa nigharamikia mambo yote muhimu kwa safari ya nje ya nchi. Visa/ passport nk muda ulipofika alienda chuoni na tulikuwa na mawasiliano mazuri sana kwa mwaka wa kwanza (Facebk/skype na hata simu) ila yalienda yakipungua mwaka wa pili. Miezi ya katikati ya 2009 nilipata wakati mgumu sana kwani mara kadhaa usiku nawasha computer yangu nakuta yupo hewani kwenye Messenger ila niki chat anabakia kimya; baadae sana akinijibu anasema kuwa aliacha Comp. yake on akalala. Ilienda hivyo hivyo hadi mwishoni mwa mwaka (2009) akawa anadai mimi sina mapenzi ya kweli kwani sijawahi hata kuwa na wazo la kwenda kumtembelea chuoni kwake (huko Holland) nafikiri wanao jua Geography wanaweza kujua unavyosema unaenda kumasalimia mtu aliyeko East Holland unaongelea $$$ ngapi?
Iliniumia sana, kwani nilijua kabisa huo sio mwisho mzuri…iliendelea hivyo hivyo kwa malumbano madogo madogo hadi muda wa kurudi ukafika. Ile tar. Aliyo niambia angekuja hakuonekana na kila nikiimuuliza kuwa ameahirisha hadi lini anakwepa…
Baada ya kufuatilia kwao ( kwa kutumia mpambe) nikajulishwa kuwa amesha pata mtu mwingine raia wa nchi jirani na kwetu (walikutana huko chuoni) na wana tegemea kufunga ndoa.
....Nilijilaumu kwa kumpa nafasi ya kusoma….labda tungekuwa tumezaa naye mtoto????
Kinachoniumiza:
1. Nili dedicate mawazo yangu yote kwake sasa kwa umri huu (karibia 40yrs)nita anzaje tena kutafuta mchumba?
2. Wasichana wazuri ambao nafikiri nitamatch nao umri naona wengi wapo kwenye ndoa
3. Frankly I am desperately and I need your hands!
Naomba uni "pm" kama unacha kunishauri

Aisee ambiere, pole sana mdughu wangu. Sio wewe peke ako kutokewa na jambo kama hilo, hivyo usiwaze sana.

Mimi ndugu yako japo ni mdogo kwako yameshanikuta mara 2. Wa kwanza alitoka kwenye familia bora, nikahisi hatukuelewana sababu alikua ana kiburi cha hela. Huyu wa pili kwao hawana kabisaaaa, I gave her everything I could, yani mpaka wazazi walianza kua na wasiwasi. Si akalaghaiwa na kajamaa ka Kenya tulikutana nako Dubai. Tulibarikiwa mtoto, binti akamwacha my son kwa mama ake kijijini nilikokuwa nimewapeleka likizo. Akenda kula bata Dar. Mungu si Athumani jamaa akamkimbia binti hotelini.
Mimi nikaenda chukua mtoto tena na bunduki kabisa huko kijijini kwao.
I am settled with my son. Satisfaction yangu mimi ni kutengeneza hela na kutumia na mwanangu. Kwa kweli imani na mwanamke sitaki kabisaaa na wala sitafuti.

In the process nimeumiza mioyo ya mabinti wengi sana lakini heri wao waumie sio mimi tena.
Let money and the development it brings be your goal and happiness. Sio hawa viumbe wenzetu!
 
Mimi ni kijana (Mvulana) mwenye umri wa kukaribia miaka 40.
Historia yangu ya maisha ni ndefu kiasi ila kwa kifupi ni kuwa; nimetoswa na msichana niliyempenda na kumuamini sana kuwa angekuwa mwenza wangu.
Hii ilitokea baada ya kumsaidia kupata scholarship ya kwenda kusoma Holland kozi ya miaka mitatu (kuanzia mwaka 2007). Huyu msichana nilimpata wakati nipo chuoni….
Kwa kifupi ni kuwa nigharamikia mambo yote muhimu kwa safari ya nje ya nchi. Visa/ passport nk muda ulipofika alienda chuoni na tulikuwa na mawasiliano mazuri sana kwa mwaka wa kwanza (Facebk/skype na hata simu) ila yalienda yakipungua mwaka wa pili. Miezi ya katikati ya 2009 nilipata wakati mgumu sana kwani mara kadhaa usiku nawasha computer yangu nakuta yupo hewani kwenye Messenger ila niki chat anabakia kimya; baadae sana akinijibu anasema kuwa aliacha Comp. yake on akalala. Ilienda hivyo hivyo hadi mwishoni mwa mwaka (2009) akawa anadai mimi sina mapenzi ya kweli kwani sijawahi hata kuwa na wazo la kwenda kumtembelea chuoni kwake (huko Holland) nafikiri wanao jua Geography wanaweza kujua unavyosema unaenda kumasalimia mtu aliyeko East Holland unaongelea $$$ ngapi?
Iliniumia sana, kwani nilijua kabisa huo sio mwisho mzuri…iliendelea hivyo hivyo kwa malumbano madogo madogo hadi muda wa kurudi ukafika. Ile tar. Aliyo niambia angekuja hakuonekana na kila nikiimuuliza kuwa ameahirisha hadi lini anakwepa…
Baada ya kufuatilia kwao ( kwa kutumia mpambe) nikajulishwa kuwa amesha pata mtu mwingine raia wa nchi jirani na kwetu (walikutana huko chuoni) na wana tegemea kufunga ndoa.
....Nilijilaumu kwa kumpa nafasi ya kusoma….labda tungekuwa tumezaa naye mtoto????
Kinachoniumiza:
1. Nili dedicate mawazo yangu yote kwake sasa kwa umri huu (karibia 40yrs)nita anzaje tena kutafuta mchumba?
2. Wasichana wazuri ambao nafikiri nitamatch nao umri naona wengi wapo kwenye ndoa
3. Frankly I am desperately and I need your hands!
Naomba uni “pm” kama unacha kunishauri

bado unajiita mvulana?!nani anataka kuolewa na mvulana?
 
Mparee2
pole sana jamani ....ila kuna wadada wengine kha! kama humpendi mtu why umpatie matumaini kiasi iko jamani mpaka mwenzake akawa 40 ndio amteme.....
ila mkuu huwezi jua mungu kakuepushia nn juu ya huyo dada
saivi inabidi ushike ule msemo wa tenda wema uende zako usingoje shukurani
na wlaa usimuombee mabaya mana ukimuombeaga mtu mabaya ndio mungu hua anazidi kumbariki ni bora ukamuombea v\s
 
bado unajiita mvulana?!nani anataka kuolewa na mvulana?

Pacha nadhani 40 yrs as a single boy..sounds like mvulana..i have my brother with 41 yrs..he is almost mvulana aisee..
Back to the topic Mparee2 hizi disappointments ziko kote kote tu..nimeona wavulana wakiwatenda wasichana na halikadhalika wasichana wakiwatenda wavulana as in your case. Kikubwa jishikilie mtoto wa kiume..mlango mmoja ukifungwa mwingine unakuwa wazi..Never mind so much about your wasted money..Italipa tu siku moja!!!
 
Last edited by a moderator:
Mparee2, Pole kwa yaliyokukuta. Kwanza ningependa kukufahamisha kuwa huna sababu ya kujilaumu kwa kumtafutia huyo mpenzi wako nafasi ya kwenda kusoma kwa sasa, maana haukujua kama ingetokea kilichotokea na imani yako ilikuwa asome ili mje msaidiane ktk kujenga maisha yenu kama mume na mke. Hakuna kosa hapo.

Kwa sasa mambo yameshatokea na hatuwezi kureverse hiyo hali kwa namna yeyote ile. Cha msingi ni kukubali na kuamini kuwa hali hiyo imetokea na kuanza kujipanga upya kimaisha. Ktk hali ya kawaida, inauma kuona kuwa umeinvest muda wako na resurces zako kwenye machimbo yaliyogoma kutoa madini, lakini ni hali ya kawaida maana siku zote huwa hatufahamu hao tunaowapenda kwa dhati huwa wanawaza nini juu yetu! laiti kama tungelijua mapema hakika tusingejidumbukiza kwenye matatizo haya ya kupenda.

Kwa sasa unaotakiwa kutulia na kuendelea kufanya kazi zako kama kawaida. Unaweza kutumia muda huo kutoka na marafiki zako au kufanya shughuli unazozipenda mara kwa mara kupunguza mawazo. Amini kuwa kuna wanawake wazuri zaidi kuliko huyo ambao Mungu aweza kukupatia. Jiamini na endelea na mchakato wa maisha huku unaomba Mungu na naamini utafanikiwa kumpata mwingine ambaye ni mwema na hata weza kukutenda. Unaweza pia kuanza kutupa macho taratibu kwa hao waliokuzunguka wenye tabia njema ambao pia wako single naamini utapata mmoja. Ila usiwe na papara, kwa sasa tumia hekima ktk kulifanya hili.

Kuendelea kumfikiria huyo wa zamani ni kuendelea kuitesa nafsi yako bila sababu ya maana. Haina maana hata kidogo kumng'ang'ania kwani ni sawa na kusubiri meli airport, haiwezi kufika kamwe.

Vingenevyo, pole sana na nakutakia kila la kheri kwenye mipangilio yako mipya.
 
Last edited by a moderator:
neno....mbalimbali.....lina maana pana sana....ngoja nikuPM mtani.....
 
bado unajiita mvulana?!nani anataka kuolewa na mvulana?

Hili tatizo ni la kitanzania zaidi, mimi ni mshichana wa miaka 31, au kama hii ya leo.
Nafikiri kwa mtazamo wa watu kama hao, ni kwamba kama hujaoa/hujaolewa au hauna mtoto wewe bado mvulana au msichana. Na kwa wao nafikiri kuwa msichana/mvulana ni sifa nzuri; lakini kwa maoni ya watu wengine hiyo inaonesha kutokomaa (kuwa immature); usichana uvulana unaishia at 18 according to culture nyingi za wenzetu na hata ukitafsiri kisheria za nchi yetu, hapo utoto unaisha na kuingia utu uzima.

If one wants to stress how young he/she is, kutumia neno "kijana" inatosha sana, au "young man/young woman" kama unataka kumomboka, lkn 'girl or boy' wakati uko 27 yrs old, haipendezi sana. Again ni mtazamo wangu tu!
 
Back
Top Bottom