Unakumbuka nini katika enzi za gazeti la Sani?

stori ya maji mazito ilikuwa kiboko. Unamkuta ommy kiss, vicky na mzee nani yule sijui. Upande wa pili wimbi la kitintale. Enzi hizo Sani lilisubiriwa kama kimwana getto siku ya kwanza
 
ulieanzisha hii mada hongera sana maana umenikumbusha mbali sana kipindi kile gazeti unalisubiria mwezi mzima vituko vya kipepe na mikasa ya mapenzi ya Dr.love pimbi.
 
Ndumilakuwili na mingo zake bwana, lile sijui lilikuwaga toleo gani,
mida ya usiku kituoni anamlia mingo jamaa amkabe kumbe jama naye anampigia hesabu Ndumilakuwili, kujipindua akawahiwa yeye, kumbe Ndumilakuwili mfukoni alikuwa hana kitu jamaa alimtukana.
Kuna kisa kingine cha Ndumilakuwili alikuwa anataka kumkaba mtu basi akatafuta mteja kabisa akawa ana-bargain bei kabla hajamkaba mtu mwenyewe, nilikuwa nacheka sana na bwana Ndumilakuwili.

Kali zaidi ni pale waliingia dili na Lodilofa kwaajili ya mradi wao wa "fruit na juice ya ajabu"
hahahahaha

Nikikumbuka hayo na nkiangalia saiv kinachoendelea kwenye idara ya burudani huwa nakubali kuwa tunapotea tu!

unakumbuka Pulamalaka msosi pliz, na kidan shan shao?
 
Hongereni sana
1. Philip Ndunguru
2. John Kaduma
3. Ibra Radi W.
4. Ted Marealle
na wengine wote waliowezesha jarida la Sani kutufikia enzi hizo.
 
mzee ole, obi na linda
kipepe mzee wa pori
ndumilakuwili kibaka
betina na zena wapinzani wa jadi
pimbi mr love
lodi lofa na mgongo wa chura

aisee umenifurahisha kunikumbusha ndumilakuwilii....siku moja alimuibia briefcase jamaa mmoja hv kumbe wizard...si akaanza kupuliza puto kijiweni! kila anapopuliza busha linazidi kushuka kwa ndumilakuwili....da mbona alirudisha!!!
 
aisee umenifurahisha kunikumbusha ndumilakuwilii....siku moja alimuibia briefcase jamaa mmoja hv kumbe wizard...si akaanza kupuliza puto kijiweni! kila anapopuliza busha linazidi kushuka kwa ndumilakuwili....da mbona alirudisha!!!

Halafu hii dawa ya kupuliza/kujaza ugpepo puto/tairi la baiskeli na mwizi kujaa bado ipo au zimebaki stori?
 
Dah!!!! Mmenikumbusha mbali sana miaka ya nyuma tulikuwa tunafaidi sana,ndumilakuwili alikuwa ni mwizi professional,akikuibia akachomoka humpati alikuwa na speed utadhani ndege huku nyuma shati lake la madoadoa linapepea tu,
Katika fikra zangu nilikuwaga najua Ndumilakuwili yupo dar, natamani sana maisha ya zamani kwa kweli.
 
hebu imagine JF ndo ingekuwa jarida la SANI la enzi zile unahisi JF members gani wangefit kuwa wahusika wa sani??
Nani angekuwa zena na Betina?? Nani angekuwa Ndumilakuwili? Madenge? Pimbi?? Lodilofa?? Kipepe?? Sokomoko?? Na wengineo!
 
Back
Top Bottom