Unajua nini kuhusu mnyama aitwae "Kakakuona"?

mbapa

Member
Feb 4, 2014
63
18
U hali gani mwana JF?

Ningependa kujua faida au thamani ya mnyama aitwae Kakakuona katka maisha na mizunguko ya binadamu!.

Nawakaribisha wataalam jamvini..
 
Ni mnyama kama wanyama wengine na thamani yake utaijua kama utaonekana kumuiba au kumuua wakiwa chini ya ulinzi wa wanyama pori.
 
Asili ya neno kakakuona(pangolins kwa kingereza)ni nchini malaysia,

Likiwa na maana ya "mwenye kujikunja" kwasababu kakakuona hufanya hivyo kama defense mechanism yake ili kujikinga na maadui

Life span ya kakakuona ni takribani miaka 20,moja ya sifa kubwa ya kakakuona ni hii;

Ulimi wake ni mrefu kuliko mwili mwake,na ngozi yake imefunikwa na magamba...

Faida kubwa ya kakakuona kwa mwanadamu haswa wale wanaoamini miujiza ni pamoja na "utabiri",yaani kakakuona anakuwa kama "futurist" anayetumika kuwatabiria watu matukio ya mbeleni,ukiacha hilo la utabiri kakakuona hana faida yoyote kwa mwanadamu na pia ni nadra sana kwa yeye kuonekana
 
nimewahi kumuokota, nikamfuga kwa takribani mwezi mzima kabla ya maaskari kuja kunipokonya, ulimi wake ni mrefu na unamsaidia kula sisimizi kutoka kwenye mashimo marefu. binafsi namfahama sana mnyama huyu!
 
Huyu mnyama simjui kihivyo zaidi ya kumwona mara moja ,na anapo onekana mfano wakati mvua zimeanza kunyesha basi zitanyesha hadi kutisha au akionekana shambani wakati mnapanda basi msimu huo utakua na mazao mengi sana
Ni hayo tu niliyoyaskia toka kwa wahenga
 
Mafuta yake na magamba yake yanatumika kuleta utajiri....endapo ukaya tumia.
 
Asili ya neno kakakuona(pangolins kwa kingereza)ni nchini malaysia,likiwa na maana ya "mwenye kujikunja" kwasababu kakakuona hufanya hivyo kama defence mechanism yake ili kujikinga na maadui...life span ya kakakuona ni takribani miaka 20,moja ya sifa kubwa ya kakakuona ni hii;ulimi wake ni mrefu kuliko mwili mwake,na ngozi yake imefunikwa na magamba...faida kubwa ya kakakuona kwa mwanadamu haswa wale wanaoamini miujiza ni pamoja na "utabiri",yaani kakakuona anakuwa kama "futurist" anayetumika kuwatabiria watu matukio ya mbeleni,ukiacha hilo la utabiri kakakuona hana faida yoyote kwa mwanadamu na pia ni nadra sana kwa yeye kuonekana

kwani ulimi wake sio sehemu ya mwili wake?
(hapana natania tu)
 
Mkuu uongo/ukweli nipo upande wako big up
 
nimewahi kumuokota, nikamfuga kwa takribani mwezi mzima kabla ya maaskari kuja kunipokonya, ulimi wake ni mrefu na unamsaidia kula sisimizi kutoka kwenye mashimo marefu. binafsi namfahama sana mnyama huyu!
Sasa kama unamfahamu mbona hujafunguka vya kutosha zaidi ya kumfuga mwezi 1? Na tutaamini vp kama kweli unamfahamu?
 
Back
Top Bottom