Je, Kanisa Katoliki ndiye mnyama wa nne duniani wa Unabii wa Daniel na Ufunuo?

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
7,621
16,700
Mnyama wa kitabu cha Ufunuo

Watu wengi hawafahamu kuwa mnyama ni nani, na wengi wamejihusisha naye bila wao wenyewe kujua kama wanashiriki na mnyama. Lakini Mungu hajatuacha gizani, hivyo, kwa kupitia neno lake (Maadiko Matakatifu) tunaweza kumfahamu mnyama huyu aliyelezwa katika kitabu cha Danieli na Ufunuo.

Tunapaswa kuyaacha maandiko yajitafisiri yenyewe; kwa maana “hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2Petro 1:20-21. Hatupaswi kumuacha mtu flani atafsri unabii kwa jinsi yake mwenyewe, badala yake tunapaswa kuiacha Biblia ijitafsiri yenyewe.

Katika Danieli 7 wametajwa “wanyama wanne” ambao wanawakilisha falme nne. Kumbuka mmyama wa 4 aliyetajwa katika Danieli 7 ndiye mnyama aliyetajwa katika kitabu chote cha Ufunuo. Hivyo hapa tutaangalia sifa za mnyama wa nne wa kitabu cha Danieli, na mnyama wa kitabu cha Ufunuo, kisha tutaangalia ni wapi hapa duniani ambapo sifa za mnyama zinatimizwa kikamilifu.

1. Mnyama atakuwa na uwezo wa kisiasa na kidini (kanisa na serikali).

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona MWANAMKE, AMEKETI JUU YA MNYAMA mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”

Mwanamke au bibi-arusi katika unabii huwakilisha kanisa.

Ufunuo 21:2 “…Yerusalemu mpya…umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.”

Ufunuo 21:9 “…Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.”

Mnyama huwakilisha taifa au ufalme

Danieli 7:17 “Wanyama hao…wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani”

Danieli 7:23 “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia…”

Kutokana na Ufunuo 17:3, mnyama huyu ana mwanamke aliyeketi juu yake, na kwa sababu unabii unatafisiri mwanamke kama kanisa, na mnyama kama taifa. Je kuna taifa au serikali ambayo imechanganywa pamoja na kanisa kama kitu kimoja? Ndiyo! Vatican, ni serikali au taifa ambalo limechanganywa pamoja na kanisa la Romani Katoliki kama kitu kimoja, na kuongozwa na mtu mmoja ambaye ni Papa.

2. Mnyama atakuwa na kanisa & serikali vimekaa juu ya milima 7.

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana…mwenye VICHWA SABA na pembe kumi.”

Vichwa saba katika unabii vinawakilisha milima saba.

Ufunuo 17:9 “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.”

Je hapa duniani kuna kanisa na serikali vimekaa juu ya milima saba?

“Ni ndani ya mji wa Roma, uitwao Mji wa vilima saba, hivyo eneo lote la Serikali ya Vatican limewekewa mpaka kikamilifu.” –The Catholic Encyclopedia, p 529.

“Je vilima saba vya Roma ni nini?

Roma inajulikana kuwa imejengwa juu ya vilima saba. Roma ilisemwa imepatikana wakati Romulus na Remus, wana mapacha wa Mars, walifika katika futi ya kilima Palatine na wakauanzisha mji, Vilima sita vingine ni Capitoline (kiti cha serikali), Quirinal, Viminal, Esquiline, Caelian, na Aventine.” –Geography.about.com

ENCYCLOPÆDIA BRITANNICA
Vilima saba vya Roma

“…kundi la vilima juu au kuhusu ambapo mji wa Roma wa zamani ulijengwa. Mji wa awali wa Romulus ulijegwa juu ya kilima Palatine (#1) (Kilatini: Mons Palatinus). Vilima vingine ni Capitoline, (#2) Quirinal, (#3) Viminal, (#4) Esquiline, (#5) Caelian, (#6) na Aventine (#7) (Vinavyojulikana kimoja kimoja kwa kilatini kama Mons Capitolinus, Mons Quirinalis, Mons Viminalis, Mons Esquilinus, Mons Caelius, na Mons Aventinus).” –http://www.britannica.com/seo/s /seven-hills-of-rome/

Kwa hiyo unabii huu wa Ufunuo 17:3, unaonyesha wazi kuwa mwanamke aliyeketi juu ya mnyama, amekaa juu ya vilima saba vya mji wa Roma. Kwa vyovyote, ni Vaticani na kanisa la Romani Katoliki ambavyo vimekaa juu ya milima saba, na kutimiza unabii huu. Danieli 7:23 inasema mnyama wa mwisho (Roma) anatofautiana na wanyama wengine watatu waliopita. Kwa hakika hakuna taifa wala ufalme mwingine ambao una kanisa na serikali, harafu kwa wakati huo huo umekaa juu ya milima saba. Ila ni kanisa la Romani Katoliki pekee.

3. Mnyama atatoka baharini

Ufunuo 13:1 “Kisha nikaona mnyama AKITOKA KATIKA BAHARI, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.”

Bahari katika unabii huwakilisha watu/jamaa, mataifa, lugha.

Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.”

Ukatoliki wa Romani ulitokea ulaya ya magharibi pamoja na makutano ya “watu/jamaa, mataifa, na lugha.” Na kwa wakati huu kanisa la Romani Katoliki lina idadi kubwa ya “watu, mataifa, na lugha,” kuliko kanisa jingine lolote duniani mwote. Na sasa, baada ya kuanzishwa kanisa moja duniani, Juni 26, 2000, Papa alichaguliwa kama kiongozi wa makanisa yote ambayo yameungana na lake. Hii ilifanya kanisa liongezeke mara mbili. Na hivi karibuni, makanisa yote pamoja na yasiyo ya Kikristo yatatangaza kwamba Papa ni kiongozi wao mwema.

Na Juni, 2008 mataifa 174 katika mataifa 192 duniani, yana serikali zao zikiwakilisha Vatican. Hivyo, kanisa la Romani Katoliki linatimiza unabii huu kwa ukamilifu.

4. Mnyama atatawala miaka 1260. (kabla hajapata jeraha la mauti).

Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataadhimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake KWA WAKATI, NA NYAKATI MBILI, NA NUSU WAKATI.”

Ufunuo 12:6 “Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko mda wa SIKU ELFU NA MIA MBILI NA SITINI.”

Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake MIEZI AROBAINI NA MBILI.”

Danieli 7:25 inaonyesha muda ambao angetawala mnyama, kama wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. Ufunuo 13:5 inauonyesha mda huu wa utawala wa mnyama, kama miezi 42, miezi 42 = miaka 3 na 1/2. Hivyo, ukiangalia kwa makini hapa utaona kuwa, wakati = mwaka 1, na nyakati mbili = miaka 2, na nusu wakati = nusu mwaka.

Kwa hiyo, wakati nyakati mbili nusu wakati = miaka 3 na nusu ya Danieli 7:25, au miezi 42 ya Ufunuo 13:5, au siku 1260. Mahesabu haya yanathibitishwa katika Ufunuo 12:6 ambapo inasema, “Yule mwanamke (kanisa) akakimbilia nyikani…wamlishe huko mda wa siku 1260.” Kwa hiyo miaka 3 na 1/2 = miezi 42 au siku 1260 ambazo mnyama angetawala kabla hajapata jeraha la mauti.

Bado, wengine watakataa na kusema, hapana, miezi 42 haiwezi kuwa sawa na siku 1260, kwa sababu miezi mingine haina siku 30. Lakini katika unabii mwezi 1 = siku 30. Mwanzo 7:11 inasema, mvua za garika zilianza siku ya 17 ya mwezi wa pili, na Mwanzo 8:3, 4. inasema kuwa maji yakapunguka mwishoni mwa siku 150, harafu safina ikatua siku ya 17 ya mwezi wa saba. Hizo ni miezi 5 tangu mvua zilipoanza. Kama ukigawanya siku 150, kwa miezi 5, utapata siku 30 kwa kila mwezi. Hivyo, miezi 42 ikizidishwa kwa 30 jibu litakuwa 1260. Kwa hiyo wakati, nyakati mbili, na nusu wakati, ni sawa na miaka 3 na nusu, au miezi 42, au siku 1260. Kwa hakika, Ufunuo 12:6 inathibitisha mahesabu haya inaposema kuwa watoto wa Mungu watakimbilia nyikani kwa muda wa siku 1260 wakati wa utawala wa mnyama (upapa).

Katika unabii siku 1 ni sawa na mwaka 1,

Ezekieli 4:6 “…siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza.”

Hesabu 14:34 “…siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka…”

Kutokana na Ezekieli 4:6 na Hesabu 14:34, ni hakika kwamba siku 1260 ni sawa na miaka 1260 ambayo Upapa ungetawala na kuwadhofisha watakatifu. Je hii ilitokea? Je unabii huu ulitimia? Au Je kuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa unabii huu ulitimia?

Kwanza kabisa tunatakiwa kujua ni lini kanisa la Romani Katoliki lilipata nguvu zote za kutawala kama “mwanamke juu ya mnyama” (kanisa na serikali), na kutawala kisiasa na kidini kwa wakati mmoja kama Ufunuo 17:3 inavyosema.

“Vigillius…alikalia kiti cha upapa (538 B.K.) chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius.” –History of the Christian Church, Vol. 3, p. 327

Hiistoria inathibitisha kuwa upapa umeanza utawala wake kama “kanisa na serikali” mwaka 538 B.K. juu ya amri ya mfalme Jastinian, na chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius. Na unabii unasema mnyama (upapa) atatawala miaka 1260 kabla haujapata jeraha la mauti.

Ukiongeza miaka 1260 katika mwaka ambao kanisa la Romani Katoliki lilianza kutawala kisiasa na kidini, mwaka 538 B.K., utapata 1798 B.K. Hivyo, unabii unasema utawala wa kwanza wa mnyama ungeisha 1798 B.K. Je utawala wa mnyama uliisha mwaka huo 1798 B.K?

“Katika mwaka 1798 Generali Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition

Kwa hakika, hizo ni miaka 3 na 1/2 au wakati, nyakati mbili, na nusu wakati, ambazo ni miezi 42 au siku 1260 za unabii ambazo mnyama angetawala kisha angepata pigo la mauti au kuchukuliwa mateka. Je mnyama alipata pigo la mauti mwaka huo 1798 B.K?

5. Mnyama atapokea jeraha la mauti.

Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake lake la mauti likapona…”

Ufunuo 13:10 “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga…”

Kama tulivyoona huko nyuma baada ya mnyama kutawala miaka 1260 angepata jeraha la mauti na kuuawa kwa upanga (upanga = vita). Baada ya mnyama kumaliza utawala wake wa miaka 1260, ambao ulianza 538 B.K. hadi 1798 B.K., Napoleon alimtuma Generali/Jemedari wake Berthier pamoja na jeshi lake, kwenda Roma kuuondoa utawala wa upapa.

Napoleon alipomtuma Generali wake Berthier kwenda kumuondoa Papa madarakani, hapo ndipo jeraha la mauti lilipompata mnyama, na mwaka uliofuata 1799 B.K. Papa alikufa. Hii ndiyo sababu watoto wa kikatoliki katika parokia hufundishwa kuwa Napoleoni alikuwa mpinga Kristo.

“Nusu ya Ulaya walidhani…kwamba pamoja na papa upapa ulikuwa umekufa.” –Joseph Rickaby “The Modern Papacy” Lectures on the History of Religion, Lecture 24, (London Catholic Truth Society, 1910), p. 1

Lakini unabii ulisema kuwa jeraha hili lililompata mnyama lingepona. Je jeraha hili lilipona? Je utawala wa upapa ulipoondolewa madarakani na Generali Berthier ulipata nguvu zake tena?

6. Mnyama atapona jeraha lake la mauti.

Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, NA PIGO LAKE LA MAUTI LIKAPONA. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.”

Kama tulivyoona, upapa ulipata jeraha la mauti mwaka 1798 B.K. Vaticani ilibaki kama kanisa tu bila nguvu za kisiasa, na unabii ulisema jeraha hili lingepona. Je jeraha la mauti lilipona? Baada ya jeraha la mauti kutokea miaka kadhaa badaye katika mwaka 1929 B.K. Italia ikautambua mji wa Vaticani kama serikali ya kujitegemea, hii ilimfanya papa kuwa na nguvu tena kama mtawala wa kisiasa na kidini. kama unabii ulivyosema kwamba jeraha la mauti lingepona, na upapa ungerudishiwa tena uwezo wake wa kanisa na serikali kwa pamoja. Hebu angalia magaziti yaliyotoa taarifa hiyo jinsi waandishi wake walivyotumia lugha ya unabii bila ya wao wenyewe kujua.

Kusaini kwa Mussolini na (Kadinali) Gasspari mkataba wa kihistoria wa Romani

“Suala la Romani usiku huu lilikuwa ni jambo lililopita, na Vaticani ilikuwa katika amani na Italia…katika kuweka sahihi kwenye mkataba wa kukumbukwa kuponya jeraha la miaka mingi, uchangamfu wa kupindukia ulionyeshwa na pande zote.” –The San Francisco Chronicle. Feb. 11, 1929

Papa Amekuwa Kiongozi Wa Serikali Tena

“Roma, Juni 7.–Kutoka saa 5 kamili asubuhi hii kulikuwa na mtawala mwingine wa serikali ya kujitegemea duniani. Katika mda huo waziri mkuu Mussolini, kama waziri wa mambo ya nje Italia akimuwakilisha mfalme Victor Emmanuel–waziri mkuu wa kwanza Italia kuvuka kizingiti cha chini cha mlango wa Vaticani–akibadilishana na kadinali Gasspari, wakala wa serikali ya upapa, akimuwakilisha papa Pius XI, makubaliano ya mikataba yalisainiwa katika ikulu ya Lateran Feb. 11. Kwa kitendo hicho rahisi mtawala wa serikali ya kujitegemea ya mji wa Vaticani amekuwepo.” — New York Times July 7, 1929

Hivyo, unabii huu ulitimia kikamilifu na jeraha la mauti lililoupata upapa 1798 B.K. lilipona kabisa tangu 1929 B.K. mpaka leo kanisa la Romani Katoliki lina nguvu za “kisiasa na kidini” au “mwanamke juu ya mnyama.” Kwa kumaliza sehemu hii tunagundua kwamba mnyama huyu ndiye aliyekuwako, naye hayuko, na sasa yupo.

7. Mnyama aliyekuwako, naye hayuko, naye yuko.

Ufunuo 17:8 “Yule mnyama…alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari…”

Mnyama aliyekuwako: ni kanisa la Romani Katoliki tangu lilipoanza kutawala kama “kanisa & serikali” 538 B.K. na likaendelea mpaka. Napoleon alipomtuma Berthier kwenda kuuondoa utawala wa upapa. 1798 B.K.

…naye hayuko tokea 1798 B.K. mpaka kusaini kwa mkataba uliofanyika katika ikulu ya Lateran katika mwaka 1929 B.K. Vaticani ilikuwa kanisa tu bila uwezo wa kiserikali.

…naye yu tayari kutoka 1929 B.K. mpaka leo kanisa la Romani Katoliki lina nguvu za kisiasa na kidini, “kanisa & sesikali” au mwanamke juu ya mnyama.

8. Mnyama atabadili majira na sheria za Mungu.

Danieli 7:25 “…naye ataadhimu kubadili majira na sheria…”

Unabii huu ni ushahidi ulio wazi sana ambao karibu kila mtu hawezi kusumbuka kuelewa kwamba ni kanisa gani hapa duniani lililobadilisha sheria za Mungu. Ni kanisa moja tu la Romani Katoliki ndilo lililobadilisha sheria za Mungu kama Danieli 7:25 inavyodai kuwa. Kanisa la Katoliki limebadilisha sheria ya pili inayozuia kuchonga sanamu ya kitu chochote kile (angalia Kut 20:4). Katika katekism kanisa limeirarua amri ya 2 kisha likaigawa amri ya 10 katika sehemu mbili ili kuonyesha amri 10 zote. Lakini Je ni nani hapa duniani anayedai kuwa anauwezo wa kubadili amri za Mungu?

“Papa anauwezo wa kubadili majira, kubadili sheria, na kuachana na mambo yote, hata maagizo ya Kristo!” “Papa anayo mamlaka na mara nyingi ameyatumia, kuachana na amri ya Kristo.” –Decretal, de Tranlatic Episcop. Cap. (The Pope can modify divine law.) Ferraris’ Ecclesiastical Dictionary.

“Papa ni wa mamlaka kuu na nguvu kiasi kwamba anaweza kurekebisha, kuelezea au kutafsiri hata sheria za Mungu…Papa anaweza kurekebisha sheria ya Mungu, kwa sababu nguvu zake si za mwanadamu, bali ni nguvu za Mungu, na hutenda kama mwakilishi wa Mungu juu ya dunia.” –Lucius Ferraris,Prompta Ribliotheca, “Papa,” art. 2, translated.

Tangu kwamba papa ana mamlaka na maranyingi ameyatumia kubadili majira na sheria za Kristo, Je alibadili sheria ya Sabato? Je kanisa katoliki liliibadili Sabato ya siku ya saba ya wiki kwenda siku ya kwanza ya wiki? Kwa hakika kanisa lenye linakubali!

“Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons

“Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” –Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923.

“Swali: Siku ipi ni siku ya Sabato?
Jibu: Jumamosi ni siku ya Sabato.
Swali: Kwanini tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi?
Jibu: Tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa katoliki, katika balaza la Laodikia (364 BK) liliihamisha kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.” –The Convert’s Catechism of Catholic Doctrine,p. 50, 3rd ed.

“Kanisa la Romani (Katoliki) liliigeuza amri ya nne kwa kuiondolea mbali Sabato ya neno la Mungu, na kuanzisha Jumapili kama siku ya mapumziko.” –Nicholas Summerbell, History of the Christian Church, 3rd edition, 1873, p. 415 [Christian Church (Christian Connection)].

“Na ni wapi tumeambiwa katika maandiko kwamba tutunze siku ya kwanza kabisa? Tumeamriwa kutunza siku ya saba; lakini hakuna sehemu yoyote tuliyo amriwa kutunza siku ya kwanza. Sababu ya kutunza siku ya kwanza ya wiki kitakatifu badala ya siku ya saba ni kwa sababu ile ile kwamba tunatunza mambo mengine mengi, siyo kwa sababu ya Biblia, lakini kwa sababu kanisa, limeyaingiza [limeyaamuru].” –Isaac Williams, Plain Sermons on the Catechism, vol 1, pp. 334, 336 [Anglican].

Hivyo, kanisa la Romani Katoliki liliibadili sheria ya Sabato na kuwaamuru watu watunze jumapili badala yake. Na mwaka 1582. Papa Gregory XIII, alianzisha kalenda mpya. Kwa vyovyote, ni Vaticani ndiyo ilitimiza unabii huu kwa ukamilifu kabisa, hakuna jumuiya, wala shirika, wala sehemu yoyote ya kidini au isiyo ya kidini ambayo imetimiza unabii huu, kama ilivyo Vaticani. Ni kanisa la Romani Katoliki pekee ambalo lilibadili sheria, na majira, na kuamuru siku ihesabiwe kuanzia saa sita usiku kinyume na Maandiko yanayothibitisha kuwa siku huanza kuhesabiwa jioni.

Mwanzo 1:5 “Mungu akaiita nuru Mchana, na giza Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.”

9. Mnyama atanena maneno ya makufuru juu ya Mungu.

Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu…”

Ufunuo 17:3 “…nikaona mwanamke ameti juu ya mnyama…mwenye kujaa majina ya makufuru…”

Ufunuo 13:1 “…nikaona mnyama…mwenye…vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.”

Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena makuu, ya makufuru…”

Kukufuru katika Biblia inaelezewa kama hali ya mtu kujifanya yeye mwenyewe kama Mungu.

Yohana 10:33 “Wayahudi wakamjibu, kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwamadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.”

Je nani hujiita na kujifananisha na Mungu hapa duniani?

“Papa siyo mwakilishi tu wa Yesu Kristo, yeye ni Yesu Kristo mwenyewe, amejificha chini ya uficho wa mwili.” –Catholic National July 1895.

“Kwa kuwa wewe u mchungaji, wewe u tabibu, wewe u mwongozaji, wewe u mkulima, hatimaye wewe u Mungu mwingine duniani.” –Labbe and Cossart’s “History of the Councils.” Vol. XIV, col. 109

“Tunapachukulia juu ya dunia hii sehemu ya Mwenyezi Mungu…” –Pope Leo XIII Encyclical Letter of June 20, 1894,

Katika “The Bull Unam Sanctam” iliyotolewa na Papa Boniface VIII inasomeka kama ifuatavyo…
“Papa wa Roma huukumu watu wote, lakini yeye haukumiwi na mtu. Tunatangaza, kutetea, kuelezea, na kutamka; kutawaliwa na Papa wa Roma ni kwa kila kiumbe cha mwanadamu muhimu kwa ajili ya wokovu ambao ulisemwa na Kristo ‘Ameviweka vitu vyote chini ya miguu yake’ inaonekana vizuri imethibitishwa kwangu…Nina mamlaka ya Mfalme wa Wafalme. Mimi ni yote katika yote na juu ya yote, hivyo basi, Mungu Mwenyewe na mimi, kasisi wa Mungu tuna usawa mmoja, na ninaweza kufanya yote ambayo Mungu anaweza kufanya.”

“Mwokozi mwenyewe ni mlango wa zizi la kondoo; ‘Mimi ni mlango wa kondoo’. kwenye zizi hili la Yesu Kristo, hakuna mtu anayeweza kuingia mpaka awe ameingizwa na Papa mtawalawa na ni pale tu kama wameunganika naye ndipo wanadamu wanaweza kuokolewa, kwa sababu Papa wa Roma ni kasisi wa Kristo na ni mwakilishi wake kwa nafisi duniani.” –(Pope John XXIII in his homily to the Bishops and faithful assisting at his coronation on November 4, 1958).

Kudai kuwa Mungu duniani Biblia inathibitisha kuwa ni kukufuru ju ya Mungu aliye hai. Kufuru nyingine ni kudai kuwa na uwezo wa kusamehe dhambi.

Marko 2:7 “Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi ispokuwa mmoja, ndiye Mungu?”

Je makuhani wa kanisa la Romani Katoliki hudai wana uwezo wa kusamehe dhambi?

“Kuhani kiukweli kabisa husamehe dhambi kwa uwezo aliopewa na Kristo.” -Joseph Devarbe’s Catechism, p. 279

“Dhambi zinaweza kusamehewa kupitia sakramenti pekee…wote makuhani na sakramenti ni vifaa ambavyo Kristo anavitumia kukamilisha msamaha ndani yetu na neema ya utakaso.” -Catechism of Trent, p. 115.

“Haya mamlaka ya jaji (Judicial authority) yatajumuisha hata uwezo wa kusamehe dhambi.” –[The Catholic Encyclopaedia Vol 12, -article “Pope” pg 265]

“Na Mungu mwenyewe analazimika kufungwa na hukumu ya kuhani wake na ama kutokuomba msamaha au kuomba msamaha, kutokana na kama wanakataa kutoa ukamilifu, unaotoa toba inayoridhisha.” –Liguori, «Duties and Dignities of the Priest», p.27

10. Mnyama ana jina lenye namba 666.

Ufunuo 13:17 “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, ispokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Ufunuo 13:18 “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinaadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.”

Biblia inatuambia kuwa hesabu au namba ya jina la mnyama ni 666

Kanisa la Romani Katoliki hudai kuwa Papa ni kichwa cha kanisa au mwakilishi wa Yesu.

“Maneno yaliyoandikwa katika kofia (miter) ya Papa ni haya, ‘VICURIUS FILII DEI’. ambayo ni ya kilatini kwa ajili ya ‘KASISI WA MWANA WA MUNGU’. Wakatoliki huchukulia kwamba kanisa, ambalo ni jumuiya ya kuonekana, lazima liwe na kichwa cha kuonekana. Kristo, kabla ya kupaa kwake kwenda mbinguni, alimteua M.t. Petro kuwa kama mwakilishi wake…hata hivyo Askofu wa Roma, kama kichwa cha kanisa, alipewa jina ‘KASISI WA YESU.'” –Our Sunday Visitor, (Catholic Weekly) “Bureau of information,” Huntington, Ind., April 18, 1915.

Kwa hiyo “VICARIUS FILII DEI” ndilo jina linalotumiwa na mamlaka ya Upapa na kumthibitisha Papa kama kichwa cha kanisa.

Helufi za kilatini zinaweza kutumika pia kama namba, na siku hizi hujulikana kama “Namba za Kirumi,” na helufi U inaweza pia kutumika kama V.

“VICARIVS FILII DEI”

(Kasisi wa Mwana wa Mungu)

V........5
I........1
C..... 100
A...... 0
R.......0
I........1
V.......5
S.......0
F........0
I.........1
L .......50
I.........1
I.........1
D........500
E.........0
I............1
Jumla= 666

Vicarius inamaanisha, katika nafasi ya
Filii Mwana
Dei Mungu
Hivyo, kanisa la Romani Katoliki linatimiza unabi huu wa hesabu ya mnyama 666 kwa ukamilifu kabisa.

11. Onyo la Mungu kwa wote walio katika kanisa katoliki.

Mungu anaoya vikali sana juu ya wale wote ambao wanashirikiana na mnyama huyu, kama wewe ni mmojawapo unapaswa kuchukua uamuzi sahihi sasa bila kupoteza muda; kwa maana hukumu itakuja juu ya mnyama na yule kahaba (kanisa Katoliki) aliyekaa juu mnyama. Hili ni onyo la mwisho la upendo na la rehema kutoka kwa Mungu.

Ufunuo 14:9-10. “Na mwingine, malaika watatu, akafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya gadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.”

Ufunuo 19:20 “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;”

Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amemkumbuka maovu yake…Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemuhukumu ni mwenye nguvu.
 
Screenshot_20230504_152214_com.facebook.litf.jpg
 
Unawatukana wakatoric wakat wao ndio waanzilishi wa ukristo.

Ukristo haujawai kuwepo kabla ya ukatoric, wakatoric ndio wao waliunda kalenda na mifumo ya Kutambua nyakati zilizopita na miaka kwa kutumia Mfumo wa B.C(before Christ) na A.D(Age after christ) yaan kiufupi mifumo hii waliitunga miaka 1700 iliyopita kwa kumfanya Yeshua ama Yesu awe kama nguzo ya majira na nyakati za kisasa ama awe kama mfumo wa kuhesabu miaka kwa kutenganisha nyakati kabla yake(agano la kale ama B.C) na miaka baada yake(A.D ama agano jipya pia kizazi kipya).

Pia wakatoric hawa hawa ndio wao waliounda kalenda mnayoitumia leo hii dunia nzima mpka humo makanisan.

Hawa hawa wakatoric ni wao waliounda biblia kwa kukusanya nakala mbalimbali za stori za zaman, walitafsir kwa lugha watakazo na kuondoa baadhi ya vitabu walivyoona ni threats kwa jamii kujua kwa kuvificha na kuunda kitabu kimoja ambacho ndio biblia ya leo mnayoitumia kuwatukana.

Mkatoric ndie mkristo PURE maana anaabudu Uhalisia wa ukristo unavyotaka, kama ukristo ni sanamu basi hata wao lazma waziabudu sanamu.

Huwezi kusema mkatoric anaabudu ushetan ama ni symbol ya shetan wakat huo hata wew unaabudu kupitia mifumo aliyounda yeye mwenyewe.

Mpinga kristo si mkatoric na hawez kuwa mkatoric maana huyo kristo mwenyewe walimuunda wao wenyewe iweje wampinge?.

Dini nyingi tu zipo chini ya mkatoric hata ile dini ya wale wanaoabudu mwezi na kwenda kuhiji mahala fulan nao imani yao ilitungwa na mkatoric kiujanja ili kutawala jamii za waarabu.

Madhehebu yote hayana ujanja kwa mkatoric ni suala la muda tu.

Ni mkatoric pekee anaabudu ktk uhalisia bila kufichaficha maana wanajua wanachokiabudu ndicho mnachokiabudu ninyi walokole na wasabato bila ninyi kukijua.

Fuatilia vizuri hutoona wakatoric wakiwazingua walokole wala makanisa yanayowatukana bali hawo walokole na jamii zao ndio humchokoza mkatoric.

Ukweli ni kwamba, Nabii wa uongo&mpinga kristo sjui mnaemuita hatotokea kanisani wala msikitini na wala hatokuja kuzipinga hizi dini na makanisa maana haya yote kayaanzisha yeye sasa kwanini ayapinge?

Mpinga kristo atakuja kukazia mafundisho ya dini kwa kuziunganisha dini zote(maana kiuhalisia zinamuabudu shetan bila watu kujua), hivyo basi Mpinga kristo vita yake si kuabudu ama kutokuabudu ktk Ukristo, bali kwenda kinyume na misingi ya dini mpya baada ya kuunganisha imani zote.

Kristo wa kweli hawezi kurudi leo wala kesho maana mpaka sasa hakuna amjuaye yuko vipi na muonekano wake uko vip, je akishuka sasa mtamtambua kwa lipi?.

Mambo ya kutukanana sababu ya utofauti wa kiimani ni Upumbavu, unamtukana mtu ilihali hata wew imani yako ina utatanishi,

Dini zote ni uzushi mtupu hazimfanyi mtu kwenda mbingun maana Muumba wa kweli hana dini wala dhehebu, hata hayo maandiko yenu ya uongo mnayotumia kukalilishana hayatambui maana yametungwa kwa maslahi ya wachache.
 
Followers of Jesus were first called “Christians” in Antioch. Acts 11:26 says, "…for a whole year Barnabas and Saul met with the church and taught great numbers of people. The disciples were called Christians first at Antioch." They were called "Christians" because their speech and behavior were like Christ.
Catholic they spread the same message, live and behave the same way as Christ ? .
 
Wasabato sio wakristo! Unajua hilo? Ni kwa sababu wasabato huishika sheria ya Musa ya kuitimiza Sabato wakifikiri bado kuwa Sabato ni siku kama vile Jumatatu, Jumatano, nk. Yesu Kristo ni Bwana wa Sabato na yeye ndiye Sabato yenyewe.

Usabato ni dini iliyojengwa juu ya Sabato ya Agano la kale na mafundisho yake makuu ni juu ya sheria ya Sabato. Na kwasababu wasabato hufikiri kuwa papa ndiye aliyebadilisha Sabato basi mafundisho ya wasabato ni dhidi ya papa kila wakati na juu ya unabii huku wakisahau kufundisha juu ya ubaya wa dhambi na umuhimu wa kumfuata Yesu Kristo na wokovu wake.

Hayo yote na mengine huwafanya wasabato kuwa watu wa Agano la kale wenye kuweka mkazo katika sheria za Mose na kusahau kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa Nyakati na Bwana wa Sabato ambayo Yesu Kristo mwenyewe wala hakuisisitiza kama kiini cha mafundisho yake. Sabato ni kiini cha dini ya wasabato.
 
Umeandika ANDIKO lefu la kunishtumu na sijaona Cha maana ulichokiandika.
Baada ya kujenga hoja kwa Maandiko unakuja kumshambulia mtoa hoja.

Sambulia hoja Kwa Maandiko na si mtoa hoja kwa umbea.

Lete REFERENCE YOYOTE YA WEMA WA CATHOLIC CHURCH BIBLICALLY MSIDANGANYWE.

FICHA UJINGA.

NAKUSHAURI SOMA
SOMA.
SOMA..... ELIMU ELIMU ELIMU

Lakini Nimefundishwa MITABU CHA METHALI

Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye.

Mithali 26:4
 
Wasabato sio wakristo! Unajua hilo? Ni kwa sababu wasabato huishika sheria ya Musa ya kuitimiza Sabato wakifikiri bado kuwa Sabato ni siku kama vile Jumatatu, Jumatano, nk. Yesu Kristo ni Bwana wa Sabato na yeye ndiye Sabato yenyewe.

Usabato ni dini iliyojengwa juu ya Sabato ya Agano la kale na mafundisho yake makuu ni juu ya sheria ya Sabato. Na kwasababu wasabato hufikiri kuwa papa ndiye aliyebadilisha Sabato basi mafundisho ya wasabato ni dhidi ya papa kila wakati na juu ya unabii huku wakisahau kufundisha juu ya ubaya wa dhambi na umuhimu wa kumfuata Yesu Kristo na wokovu wake.

Hayo yote na mengine huwafanya wasabato kuwa watu wa Agano la kale wenye kuweka mkazo katika sheria za Mose na kusahau kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa Nyakati na Bwana wa Sabato ambayo Yesu Kristo mwenyewe wala hakuisisitiza kama kiini cha mafundisho yake. Sabato ni kiini cha dini ya wasabato.

Nitakupa mstari mmoja Tu kutoka agano jipya nadhani UTAELEWA Kila kitu.
, sitaki KUZUNGUMZIA masuala ya Sabato, usabato nk.

UFUNUO WA YOHANA 12. 17.

Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu;....

KEY....
JOKA MEANS SHETANI.
MWANAMKE NI KANISA.

WAZAO NDIO WAUMINI wa KWELI wazishikao AMRI za Mungu 10.
Na ushuhuda wa YESU KRISTO.

Endelea Kudharau amli za Mungu.

N:B. AMRI NI SHERIA, TABIA, YA MUNGU HAIBADILIKI.
 
Ni vigumu kujadili na watu wasio wakristo mambo ya Kristo.

Wasabato bado ni watu wa Agano la Kale hawamwelewi Kristo na ukombozi alioleta. Yesu alikuja kuwakomboa watu kutoka ukandamizi wa sheria.

Kiini cha Ukristo wetu sasa ni Amri Mpya ya Upendo aliyotupa Yesu na sio tena mambo ya kale ikiwa ni pamoja na mambo ya zaka! Yesu hakuwahi kuzungumzia zaka kwani yeye ndio kila kitu zaka, sadaka, sheria na wokovu.

Pia Wasabato acheni ulevi wenu na Ukatoliki na Papa! Acheni kuishi tafsiri potofu za Ufunuo! Yesu Kristo ndiye huo Ufunuo na Uzima wa Milele, hakuna mwingine!
 
Mbona unawashambulia wasabato.

Ingependeza kama ungejega hoja zenye ushahidi wa VITABU.

Nasikitika hata AMRI za Mungu huzijui masikini

UKRISTO SI LELEMAMA.
UKRISTO NI KUJIKANA KUCHUKUA MSALABA NA KUMFUATA YESU KILA SIKU. KWA UKAMILIFU WOTE .
 
Wasabato ndio wanaotushambulia Wakatoliki kila siku. Ukatoliki na Papa ndio agenda zao! Nawaambia wakristo wote kuwa kuna mambo ya msingi katika Ukristo wetu na sio sheria za Waisrael wa kale. Amri ya upendo ndio kila kitu ndugu na sio kukremu Maandiko bila kuelewa misingi yake.
Mbona unawashambulia wasabato.

Ingependeza kama ungejega hoja zenye ushahidi wa VITABU.

Nasikitika hata AMRI za Mungu huzijui masikini

UKRISTO SI LELEMAMA.
UKRISTO NI KUJIKANA KUCHUKUA MSALABA NA KUMFUATA YESU KILA SIKU. KWA UKAMILIFU WOTE .
sa
 
Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona MWANAMKE, AMEKETI JUU YA MNYAMA mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”

Mwanamke au bibi-arusi katika unabii huwakilisha kanisa.

Ufunuo 21:2 “…Yerusalemu mpya…umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.”

Ufunuo 21:9 “…Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.”
Kwenye hizi tafsri zako hakuna sehemu imeandikwa Mwanamke ni Kanisa😅😅😅
 
UFUNUO WA YOHANA 12. 17.

Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu;....

KEY....
JOKA MEANS SHETANI.
MWANAMKE NI KANISA.
Sura hiyo hiyo ya 12 unazungumzia Joka mwenye Mkia anakokota theluthi ya nyota za mbinguni.

Je hizo Nyota ni kiti gani?
 
Asante sana Kwa swali zuri mkuu.
HAYA ndio Maswali ninayo yapenda.

UZURI WA BIBLIA HUWA INAJITETEA YENYEWE HAIITAKI MSAADA.

KWA KIFUPI SHETANI ALISHUSHWA KUTOKA MBINGUNI NA MALAIKA WAASI (MAJINI, MAPEPO NK) KWA SABABU ZIFUATAZO...

EZEKIEL 28...
14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
Ezekieli 28:14

15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.
Ezekieli 28:15

17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
Ezekieli 28:17

Shetani aliasi na akafukuzwa kutoka mbinguni. "Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!

!" (Isaya 14:12). Yesu alisema, "Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme" (Luka 10:18), na katika kitabu cha Ufunuo Shetani inaonekana kama "nyota iliyoanguka kutoka mbinguni hadi duniani" (Ufunuo 9: 1).

Pia tunaambiwa kuwa theluthi moja "na majeshi ya malaika elfu nyingi," (Waebrania 12:22) alichagua kumtukana naye. Yohana aliona ajabu hii mbinguni, "... joka kubwa jekundu, … na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi… joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote"(Ufunuo 12: 3-9).

Kwa kuwa Shetani anajulikana kama nyota iliyoanguka au kutupwa huku duniani, na Ufunuo 12: 4 inasema theluthi ya nyota zilifukuzwa nje naye, basi hitimisho ni kwamba nyota katika Ufunuo 12 zinarejelea malaika walioanguka, kikamilifu theluthi moja ya jeshi la mbinguni. Ikiwa idadi ya theluthi ni sahihi, huo ni uhakika gani! Theluthi mbili ya malaika bado wako upande wa Mungu, na kwa wafuasi wa Kristo, wao pia wako upande wetu.
 
Sura hiyo hiyo ya 12 unazungumzia Joka mwenye Mkia anakokota theluthi ya nyota za mbinguni.

Je hizo Nyota ni kiti gani?

Joka ni Shetani...

Theluthi ya Nyota ni wale MALAIKA walioamua kuasi pamoja na shetani.

Waliomuunga mkono shetani katiza zoezi Zima la kutaka kupindua MAMLAKA ya Yesu MBINGUNI.
 
Sasa mbona mambo ya nyuma yanatajwa kama ndio unabii wa mambo yajayo?
 
Back
Top Bottom