Unaijua historia ya ASP na rangi ya sura yake?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,786
Hivi karibuni tutaadhimisha miaka 39 ya kuasisiwa chama kitukufu na tawala cha CCM . Ni tukio la kihistoria llofanyika nchini kwetu baada ya nchi mbili zetu kuungana kiserikali na kuukata mzizi wa fitina tukaunganisha vyama vyetu na kuzaliwa chama cha Mapinduzi. Jina ambalo linajaribu kuweka kumbukumbu na kuyalinda Mapinduzi matukufu.

Lakini ni wachache sana wanayoijua historia ya mwenza huyu wa TANU , nae ni ASP. Chama hiki kimeundwa pia na muungano wa vyama viwili Shirazi Aassociation (SA) kichokuwa kinaongozwa na Rais wake Thabit bin Kombo bin Jecha al-Shirazy (1904-1988), ni mzaliwa wa kijiji cha Kizimkazi, Zanzibar, na African Association (AS) kilichokuwa kinaongozwa na Abeid Amani Karume (1905-1972), mzaliwa wa Nyasaland (Malawi)

Muungano wa vyama hivi haukuwa rahisi kwa vile wengi wa viongozi wa SA walikuwa wanapinga kuungana AS kwa vile wote ni wahamiaji na hawana asili ya visiwa hivi na ni chama cha makuli na mbaharia tu. Lakini kubwa zaidi na baya walikuwa wanahubiri ubaguzi. Soma kijipande cha nukuu ya Gazeti la AS liliokuwa linajuulikana Afrika kwetu, uijue sura yao

"We wish to assure all the so called Zanzibaris that anything short of an African state will never be accepted when self-government is achieved in this Protectorate. We are also opposed to multi-racial government in these islands. It is against all this Association stands for. We want Zanzibar to become an African state like the Gold Coast" (Afrika Kwetu, May 5, 1955).

Kwa ushawishi mkubwa, Nyerere aliweza kumshawishi (Ami) Thabit Kombo kukubali kuungana na SA kwa hasara yakuwapoteza viongozi wake wakuu ambao walikataa katakata, kama vile Sheikh Ameir Tajo al-Shirazy

ASP ilizaliwa tarehe 5 Februaru 1957.

Waliojengua na SA na wao walianzisha Chama chao kilichokuwa kinaitwa ZPPP ambacho ndicho kilichoweza kuunda UKAWA na ZNP na kuishinda ASP na hivyo kutoa Waziri mkuu Sheikh Muhammad bin Shamte bin Hamad al-Shirazy, Mwalimu wa Shule, na mzaliwa wa Chambani, Pemba.

Kwenye sherehe za Mpinduzi zilizo pita vjana wa CCM walionekana kupita mbele ya kadamunasi wa kubeba mabango yalioandikwa maneno ya kibaguzi ambayo hayana tofauti na msimamo wa chama na waanzilishi wa ASP kama ilivyonukuliwa kwenye gazeti la chama Afrika kwetu 1955

Hichi ndio chama kilichoungana na TANU na kuzaliwa CCM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom