Unafiki wa TBC kwa jitihada za CHADEMA katika ujenzi wa Tanzania

Mkuu mpaka leo hujajua kilicho nyuma ya tbc? Nafikiri unipashwa kujua kuwa tbc ni sasa iko kulinda mafisadi sasa sisi tunachokifanya ni kumobulaizi the majority ili siku tukiwatokea watuachie chombo chetu waanzishe chombo cha magamba!!! Kwa hiyo wapenda maendeleo wote tushirikiane kuhamasisha umma ili tukianza kufanya maamuzi magumu tusiwe na wakutuzuia.
Kwa CDM msianzishe tv yenu acheni kulalamika
 
Naona watakuwa wamepigwa mkwala...tbc ya leo, sio kama ile ya tido.
na ndo maana walimuondoa tigo, jamaa alikwa anafanyia kazi ile moto ya TBC ki ukweli (UKWELI NAUHAKIKA) , utakumbuka mshanA alipokuwa anaongea siku ya kukalibishwa alisema, TBC inatakiwa iwe na uzalendo katika kutoa habari .. i doubt the word "uzalendo" ... alikuwa ana maana gani hasa....!!!
 
Chadema nanyie anzisheni chombo chen cha hbr mbona ccm wanaradio mie naona mda ni huu tutawatumia hata mpesa katika kufanikisha ilo.
 
Sina shaka TBC TV itakufa kama Radio Tanzania.
Majibu ya huu upuuzi ni kwa Chadema wangeamua kuingia mkataba na Private TV yoyote yenye ujasiri kurusha maandamano na vipindi vingine mpaka pale itakapokuja TV ya Chadema. Chadema lazima wafanye hivyo maana bila kuyaonyesha haya maandamano na vipindi vingine itachukuwa muda mrefu kuwafikia watu wote.

Nakumbuka mama yangu alikuwa hataki kusikia habari za chadema maana hata alikuwa haijui lakini baada ya kuja mjini na kuona jinsi watu walivyokuwa wanajaa kwenye mikutano ya chadema alikili kumbe huko kijijini huwa tunadanganywa tu na CCM

Pia mikanda ya maandamano inaweza kupelekwa kwenye ofisi za matawi ya sehemu ile ili watu wawe wananunua wakaangalie majumbani kwao.

Pia watu ambao ni wajasiria mali wanaweza kutengeneza collection ya matukio makubwa ya maandamano na kuuza hiyo mikanda na CD mitaani. Itakuwa ni biashara lakini pia itasaidia kuwafikia watu wengine.
 
Nashukuru sana Tbc kwa hicho kidogo mlichoonesha. Kama mnakumbuka niliandika kuhusu hilo swala, Inaonekana Mshana amepata ujumbe ktoka hapa JF. Big up Mshana now you are coming on truck. Lengo letu sio kuchukia chombo chetu cha habari cha umma, bali tunarekebisha pale tupapoona akitendi haki kwa Walipa kodi wa nchi hii.https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/132515-tbc-mnaibagua-chadema-mpaka-lini.html?highlight. Tutapiga kelele pale tutakaona Jamii fulani inaonewa kwa pesa zetu wenyewe,
 
Wanajamvi kwa mara nyingine naleta maoni yangu hapa jamvini kuhusu shirika letu la
utangazaji TBC.


Mengi yamezungumzwa na tutaendelea kuyakemea mpaka kieleweke.
Baada ya kuzungumza sana na kuonesha kukerwa sana,leo tbc wamejitutumua
kuonesha mkutano wa CHADEMA ikiwa imechakachuliwa sana,na kilichonishangaza
mimi ni kuchagua na kurusha sehemu ambazo hazikuwa na mguso kwa jamii

Na chakushangaza zaidi hotuba ya Dr Slaa kuhusu upotevu wa bil 200 ilikatwa na hauoneshwa kabisa.
Wakati huo huo katika muhtasari wa habari,uchaguzi wa mwenyekiti wa uvccm uliwekwa katika habari zilizopewa uzito.

Wadau nauliza tena ninini kilicho nyuma ya tbc?

Hilo si shirika la utangazaji la taifa la Tanzania bali ni shirika la utangazaji la ccm, kwa malengo ya ccm, na mstakabali wa mafisadi.
Wanapaswa wabadili jina, ili liendane na propaganda wanazofanya. Kila wakati wanatangaza uozo mtupu.
 
Iko siku nguvu ya Umma itawalazimisha kutoa habari zetu. Uvccm wa wilaya kama bagamoyo wanapewa air time kubwa kuliko chama kikuu cha upinzani. Huu ni utani kwa kodi zetu zinazotumika hapo Tbc.
 
lakini si umeelewa hata ukirekebisha, unaacha kueleza vitu vyenye kutujenga unaongelea lugha wewe Bakita.inaelekea upo chama cha magamba.
 
Wanajamvi kwa mara nyingine naleta maoni yangu hapa jamvini kuhusu shirika letu la
utangazaji TBC.

Mengi yamezungumzwa na tutaendelea kuyakemea mpaka kieleweke.
Baada ya kuzungumza sana na kuonesha kukerwa sana,leo tbc wamejitutumua
kuonesha mkutano wa CHADEMA ikiwa imechakachuliwa sana,na kilichonishangaza
mimi ni kuchagua na kurusha sehemu ambazo hazikuwa na mguso kwa jamii

Na chakushangaza zaidi hotuba ya Dr Slaa kuhusu upotevu wa bil 200 ilikatwa na hauoneshwa kabisa.
Wakati huo huo katika muhtasari wa habari,uchaguzi wa mwenyekiti wa uvccm uliwekwa katika habari zilizopewa uzito.

Wadau nauliza tena ninini kilicho nyuma ya tbc?


TBC waelewe kwamba wao si waajiriwa wa CCM, bali umma, wanalipwa na umma, na umma una haki ya kupata habari muhimu. Sasa wachague kusuka au kunyoa. Udhalimu wa aina yeyote utawatokea puani.:A S cry:
 
hata ile habari ya wale watanganyika kule pemba waliochmewa vibanda vyao..wameitangaza kwa usanii wa hali ya juu
 
kama kweli TBC ni TV ya Tifa kwa maana ni TV ya walipa kodi wote wa Tanzania na ipo pale kuwahabarisha watanzania wote bila kujali dini au kabila au hata itikadi yake kisiasa.

Waandishi wake wanakosa maadili kwa kuficha habari. Ni lazima wajirekebishe. Kwani chombo hicho ni mali ya wote na sio baadhi.
 
Chadema nanyie anzisheni chombo chen cha hbr mbona ccm wanaradio mie naona mda ni huu tutawatumia hata mpesa katika kufanikisha ilo.

Vyombo vya habari vikitumika kupendelea upande mmoja ni hatari sana hasa ktk uvunjifu wa amani kwa nchi yoyote ile,ushauri wako Chadema na wao wafungue tv yao ni mzuri Ila utaratibu wa vyombo vya habari ufuatwe.Tbc tayari wameshajenga chuki na wananchi binafsi mimi siipendi tbc kwa vitendo vyao na kuliko niangalie tbc ni bora nikaangaia katuni za Tom 'n' Jerry kupunguza mawazo
 
Hii inasikitisha sana kwa chombo cha Umma kinapofanya ushabiki kwa chama tawala utafikiri tbc inaendeshwa kwa gharama za chama cha magamba, wanapaswa kujifunza kutoka kwy vyombo vya nje kama BBC, ambacho ni chombo cha Umma, lakini kinafanya kazi bila upendeleo, vinginevyo kitkuwa kinaangaliwa na magamba people tu na wenye mawazo mgando!
 
wadau,mi nashauri anaehusika na masuala ya habari na mawasiliano CDM atuorginize wadau tuchange tuanzishe Radio stesheni na Channel yetu ya Tv.Kwa hivi sasa nashauri tusiangalie kabisa TBC,wasije wakachochea hasira tukajichukulia sheria mikononi.watakapoporomoka kama Chama cha Magamba ndo watarealize!
 
Back
Top Bottom