Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,796
Naona kuna mwamko mkubwa sana wa nchi za kiafrika ambazo ni wanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kujitoa kwa kisingizio cha kuwa eti wanaoandamwa ni viongozi wa kiafrika tu.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 huku nchi nyingi za kiafrika zikishadadia kwa nguvu sana kati ya kesi 12 zilizotolewa maamuzi 9 ni za viongozi wa Afrika.
Naita ni unafiki kwakuwa viongozi hawa hawawaambii ukweli hao pimbi bwana wakubwa wanaowapeleka watakavyo viongozi wetu haya wenye akili finyu sana.
Wanapopambana kubaki madarakani hata kwa gharama ya damu isiyo na hatia! Wanapominya demokrasia, wanapoua kwa kisingizio cha kuzima uasi na kulinda nchi misaada ya hali na mali miundombinu silaha na vifaa vya kijeshi vyote hivi hupata toka kwa hao hao pimbi waanzilishi wa hiyo mahakama ya uhalifu wa kivita ambayo makao yake makuu yako The Hague nchini Uholanzi.
Leo anakuuzia silaha kwa mlango wa nyuma unapaisha uchumi wake, kisha unatumia hizo silaha kuangamiza wananchi wako na ustawi wa nchi halafu wanakuja mbele kukukamata na kukufungulia mashtaka ya uhalifu wa kivita kwa silaha alizokuuzia mwenyewe na washirikina wake...hovyo kweli hii.
Kwanini wasiwaambie ukweli kwenye hili wanaogopa nini ?kilichotokea Liberia tumekiona Tailor yuko the Hague sasa! Al Bashir wa Sudan wamemkosakosa lakini bado wanamtafuta, kilichotokea Congo kinajulikana Pierre Bemba yuko nyuma ya vyuma, waliobaki wanaendeleza ukatili ule ule! Burundi Rwanda nk nk hali si shwari.
Kujitoa kwenye hii mahakama ni jambo la kinafiki mno lakini pia lenye kutisha kabisa! Hii mahakama iliwapunguza spidi sasa wanajitoa ngoja tuone mwisho wake.