supermarket
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 7,451
- 10,933
Baada ya kujitoa kesi zetu Africa kisheria tunatakiwa kuzipeleka mahakama ipi?
Hiyo elimu itatoka huko huko kwa njia ya ufadhili na misaadaKwanza kabisa Africa inatakiwa ipatiwe elimu ili ielimike.
Pili, tuwe na demokrasia, uzalendo na utu baina yetu.Halafu tupigane kujipatia uhuru wa kiuchumi ili sisi tuwe na uwezo wa kufanya maamuzi yetu sisi wenyewe.
Kuna haja ya Afrika kuwa wabishi kama NK na Russia, tofauti na hapo hakuna namna.Hiyo elimu itatoka huko huko kwa njia ya ufadhili na misaada
Wazungu hawako tayari hata siku moja kuona Afrika iko huru kiuchumi kifikra na hata mitazamo, bado wanapenda sisi tuwasikilize na kuwategemea wao kwenye kila kitu. ndio maana wako tayari kutupa misaada ya vitu visivyo na tija na vyenye madhara kama silaha lakini sio elimu yenye ukombozi wa kifikra
Hizi tawala magumashi na katili za kiafrika zote zina mkono wa ngozi ya kitimoto. .jamaa wanacheza na akili zetu watakavyo
North korea serikali Yao inawekeza zaidi kwa watu wake na hamna brah brah. Hao russia hakuna ubaguzi wa kutoa elimu kwa watu wake kama sisi hapa. Wao hawatoi mkopo wa elimu wao wanatoa elimu. Sisi hata mikopo ni siasa tu. Vyuo vimefungua, serikali wanadai uhakiki wa mikopo siku zote walikuwa wapi.? Haya watoto watasoma mda gani? Afrika haiwezi kukomaa.Kuna haja ya Afrika kuwa wabishi kama NK na Russia, tofauti na hapo hakuna namna.
Ukisoma historia za mataifa/jamii zilizofanikiwa kimaendeleo utagundua hakuna waliopita njia tunazopita/tumia.North korea serikali Yao inawekeza zaidi kwa watu wake na hamna brah brah. Hao russia hakuna ubaguzi wa kutoa elimu kwa watu wake kama sisi hapa. Wao hawatoi mkopo wa elimu wao wanatoa elimu. Sisi hata mikopo ni siasa tu. Vyuo vimefungua, serikali wanadai uhakiki wa mikopo siku zote walikuwa wapi.? Haya watoto watasoma mda gani? Afrika haiwezi kukomaa.
Kuna haja ya Afrika kuwa wabishi kama NK na Russia, tofauti na hapo hakuna namna.
Ningependa sana kama USSR ingekuwa hai ili tuwe na dola mbili kubwa, pengine tungekuwa na option.Ili uwe mbishi
1. Uwe na bajeti yako isiyoteteleka 100%
kwetu Africa sidhali hili kuwezekana au la kwa maifa machache sana.
2. Uwe na Sayansi na Teknolojia yako kujitoshereza kiuchumi kwa kila jambo
3. Uwe na masoko yako ilikukidhi mahitaji yako kisera, kiuchumi nk
Hayo yoote kwetu Afrika hayapo.
Haiwezekani kabisa kujisimia sisi wenyewe
Wakifanikiwa gawa viongozi madikteta wa afrika kujitoa. Bas wananchi waafrika tujiandae kufanywa vyovyote watakavyo mana hawakuwa na wa kuwabana.Naona kuna mwamko mkubwa sana wa nchi za kiafrika ambazo ni wanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kujitoa kwa kisingizio cha kuwa eti wanaoandamwa ni viongozi wa kiafrika tu
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 huku nchi nyingi za kiafrika zikishadadia kwa nguvu sana kati ya kesi 12 zilizotolewa maamuzi 9 ni za viongozi wa Afrika
Naita ni unafiki kwakuwa viongozi hawa hawawaambii ukweli hao pimbi bwana wakubwa wanaowapeleka watakavyo viongozi wetu haya wenye akili finyu sana
Wanapopambana kubaki madarakani hata kwa gharama ya damu isiyo na hatia! Wanapominya demokrasia, wanapoua kwa kisingizio cha kuzima uasi na kulinda nchi misaada ya hali na mali miundombinu silaha na vifaa vya kijeshi vyote hivi hupata toka kwa hao hao pimbi waanzilishi wa hiyo mahakama ya uhalifu wa kivita ambayo makao yake makuu yako The Hague nchini Uholanzi
Leo anakuuzia silaha kwa mlango wa nyuma unapaisha uchumi wake, kisha unatumia hizo silaha kuangamiza wananchi wako na ustawi wa nchi halafu wanakuja mbele kukukamata na kukufungulia mashtaka ya uhalifu wa kivita kwa silaha alizokuuzia mwenyewe na washirikina wake...hovyo kweli hii
Kwanini wasiwaambie ukweli kwenye hili wanaogopa nini ?kilichotokea Liberia tumekiona Tailor yuko the Hague sasa! Al Bashir wa Sudan wamemkosakosa lakini bado wanamtafuta, kilichotokea Congo kinajulikana Pierre Bemba yuko nyuma ya vyuma, waliobaki wanaendeleza ukatili ule ule! Burundi Rwanda nk nk hali si shwari
Kujitoa kwenye hii mahakama ni jambo la kinafiki mno lakini pia lenye kutisha kabisa! Hii mahakama iliwapunguza spidi sasa wanajitoa ngoja tuone mwisho wake
Na kama Nchi zote hapa Africa zimejitoa hivyo vikwazo vitamwathili nani....??Ona Burundi alivyokurupuka akataka kujitoa haraka haraka lakini akaambiwa asome katiba ya ICC kwanza (kumbe hata walikuwa hawajaisoma) kwamba unatakiwa kwanza utoe notice ya mwaka mmoja ukieleza kusudio la kujitoa ndio mchakato uanze!
Africa kusini baada ya kugundua hilo ndio nao sasa wameanza mchakato wa kujitoa
Wazungu wametutangulia kifikra kujiunga ni rahisi kujitoa sasa! Hao wanaotaka kujitoa watakumbana na vikwazo huko mbeleni vitakavyokwamisha mchakato wa kujitoa kaazi kweli kweli
Kama ni hivyo basi tutalazimika kujitoaCHARMILTON baba mwenye nyumba hashtakiwi, Ukiangalia bajeti ya ICC kwa asilimia 90 no umoja wa ulaya na miundombinu pia na hata makao makuu yako huko kwahiyo hapo unaweza kupata picha pana zaidi
Marekani na washirika wake pale Libya kaua wangapi....???Tukijadili unafiki wa viongozi unaoneka vizuri sana kwa mambo yafuatayo
1. Unafiki nipale wao wanawajibishwa nakupewa adhabu kutokana na udhalimu wao...mfano
-Burund Nkrunziza kaua wengi na bado anauwa
-Sudan Bashir ameua sana daful mpaka tukaifaham huku na bado anauwa
-Uganda, Museven anatawala kwa lazima na nguvu kubwa
-Kenya, Uhuru na makamo wake walisababisha maafa makubwa na bado.....
-Tanzania, haileweki kinachoendelea zanzibar kama ni amani au utawala wa mkono wa chuma
-Zimbabwe, Babu mgabe amepiga nakutesa kiasi kwamba ukiingia mgahawani kupata sahani ya wali uandae Zim dola zaid ya 100,000....uchumi umeharibka vibaya....above 90yrs old bado yupo ikulu...very wondeful..
-DRC, Kabira junior...Katiba anaikanyaga kanakwamba ikulu mali yake....watu wanauwawa nk
nk nk
unafiki wa hawa wakwetu wao kuuwa na kutesa saaafi ila wanapogeuziwa kibano na hiyo mahakama hawataki
Amakweli
MKUKI KWA NGURUWE....kwa mwandamu....
Wao ndio wafadhiliViongozi wa Afrika wanaweza kuwa na matatizo, tena matatizo makubwa sana lakini ICC haina utakatifu wa kuwahukumu hao viongozi wakati wanakunywa juice na Tony Blair na George Bush. Mahakama ya kihuni kabisa.