Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Kama tumeamua kupambana na CCM na utawala wake basi tujipange kwa kutegemea vyama vya siasa tu.
Mambo haya ambayo naona ni mchezo unaopangwa na CCM na serikali yake ni kutumia vyombo hivi katika kuwapindisha wananchi wazalendo.CCM na serikali yake wanatoaa muelekezo kwa vyombo hivi kwa umakini kabisa pengine hata vyombo vyenyewe havielewi kuwa vinatumia kutokana na umahiri wa mashushu kuingiza hoja katika vyombo vya dini.
Vyama vya siasa na wazalendo wapenda siasa waache kabisa kutegemea hoja kutoka katika mashirika au vyombo vya kidini naa badala yake viendeleze mapambano ya ana kwa ana ,jicho kwa jicho au uso kwa uso kutoka ndani ya vyama vyao kuikabili CCM na Serikali yake.
Nasema tusitegemee kauli kutoka kwa Mashekhe au maaskofu hawa sio wanaogombea ubunge wala umeya wala uraisi ,wala sio wanaoanzisha hoja ndani ya bunge,hivyo maelekezo na makaripio yote yatoke ndani ya vyama vya siasa,ikiwa kwenye mikutano au kutoka kwenye vyombo vya habari.
Ni ukweli usiopingikaa kuwa kutegemea vyombo hivi kutavifanya vyama vya siasa kuwa dhaifu na visivyojiweza katikaa kuamsha hisia na hoja mbele ya wananchi na mwishowe hata wanachama wataviona vipo kama wasindikizaji.Ni lazima kwa hali yeyote ile vyama vya siasa vya upinzani viwe vya mwanzo na vyenye kauli kali dhidi ya CCM na serikali yake.