Umoja trust fund (utt)

Kaka Kapo

JF-Expert Member
Nov 23, 2012
535
330
Wanajamvi naomba nijuzwe kitu kuhusu hizi units za UTT leo nimepita pale sukari house kufuatilia status ya units zangu tangu mwaka 2005 nlivonunua nilinunua units 100 by then kwa gharama ya shs 7000 lengo ni kujua status afu niendelee either kununua au kujitoa!

Baada ya kuangalia ile statement nimeona wamepost mwaka ulofuatia yani 2006 gawiwo langu lilikuwa shs 900 na kwa sababu mie nliomba badala ya kugawiwa pesa wanipe units wakaziconvert sh 900 Kuwa units 8 sasa jumla Nina units 108 zenye thaman ya shs 28000 sijaona gawiwo la kuanzia mwaka 2007 - 2012. Naombeni kujuzwa je kwa hiyo miaka ni kwa nini sijapata units au gawiwo?

Na je ni sahihi nikiendelea kuwekeza kwa hii kitu kuna faida yoyote! Kwa sababu nafikiria kuanzisha utaratibu wa kuwekeza kwa style ya kununua hisa je ni uamuzi sahihi.

Kwa yeyote mwenye utaalamu au mwanahisa wa UTT naomba msaada wako katika hili! Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa mchango wako.
 
Swali hili unauliza hapa JF kwani ni ofisi ya UTT?? Ulitakiwa umuulize ofisa husika wa hayo masuala ungepata msaada zaidi kuliko hapa, tena wa uhakika usiokuwa na chenga!!!
 
Nadhani kwakuwa mtaji wako ni mdogo jaribu kuendelea kuwekeza kwenye hivyo vipande vya UTT . Kwa kiasi cha pesa ulichonacho ni very risk ku invest kwenye shares. Unahitaji diversified portfolio na mpaka uwe na mtaji mkubwa lakini kwa kutumia vipande wana kuwa tayari wame diversified. Jaribu kufatilia kipindi ambacho hawajaonnyesha kwenye statement.
 
Kwanin hukuuliza hapo hapo

Boss sikuwa na ujuzi wa kuisoma ile statement kwa haraka haraka si unajua mambo ya taaluma! Afu vile vile nilifika pale nikiwa nimechelewa walikuwa wanafunga. Naatarajia kwenda tena week hii mapema tu!
 
Nadhani kwakuwa mtaji wako ni mdogo jaribu kuendelea kuwekeza kwenye hivyo vipande vya UTT . Kwa kiasi cha pesa ulichonacho ni very risk ku invest kwenye shares. Unahitaji diversified portfolio na mpaka uwe na mtaji mkubwa lakini kwa kutumia vipande wana kuwa tayari wame diversified. Jaribu kufatilia kipindi ambacho hawajaonnyesha kwenye statement.

Kaka kwa sasa nawaza kufanya hii kitu serious ndo maana nafanya utafiti ili niingie nikiwa nauelewa wa kutosha! Nipo katika position ya kuweza kununua vipande 10000 every month!
 
Mkuu uliwekeza 7000 after 6 years 24000,,zaidi ya mara tatu faida! Imagine ungekua uliwekeza 10M!!..Thats paying bussiness. Fuatilia hizo figure zilizomiss kwenye statement tu.

Actually hiyo figure ni ya mwaka mmoja ambao ni 2005-2006 mingine haionekani ndo natakanifuatilie nijue why? Nadhani ni aina nzuri ya uwekezaji though hamna elimu nzuri ya uwekezaji wa njia ya share unatolewa!
 
Wadau mwenye kujua hawa utt wanafanyaje kazi anipe elimu kama nataka kuwekeza huko??

Sent from my iPhone 5 using JamiiForums
 
Mkuu hopaje, huu ni mfuko wa pamoja wa uwekezaji. Katika hali ya kawaida ni vigumu kwa mtu mmoja mmoja kuwa na uwezo wa kununua hisa za kutosha kwenye kampuni zitakazomwezesha kupata faida ya kutosha kutokana na kupata gawio. Wanachokifanya UTT ni kukusanya hela hizi kidogo kidogo kutoka kwa watu wengi na kutengeneza mfuko mmoja mkubwa ambao utakuwa na uwezo wa kuwekeza kwenye makampuni tofauti tofauti. Hawa wawekezaji wadogo wadogo wengi ndo watakaokuwa wanagawiwa faida itakayokuwa inapatikana kutokana na uwekezaji huo wa UTT.

Hawa jamaa wana mifuko tofauti tofauti kama umoja, mfuko wa watoto, mfuko wa kujikimu na mingineyo ambayo kila mmoja una malengo yake kwa hiyo ni uamuzi wako wewe unayetaka kuwekeza kuchagua mfuko unaoutaka katika hiyo kutegemeana na malengo yako. Waweza tembelea hapa kwa maelezo zaidi: Utt home page
 
vipi ukiwalinganisha na benki za kawaida.. wana unafuu wowote?
 
Hawa ni wezi wakubwa. Wakati wanaanza, walikuwa na lugha laini, kiasi cha kushawishi wengi wetu tukajiunga kwa ahadi nzuri kuwa tutakuwa tunapata gawio. Kinyume chake wamekusanya mamilioni ya Watanzania na kuishia mitini, hakuna cha gawio, na hata ukitaka kuuza hisa zako, wao hawaruhusu, kinyume na ahadi zao za awali. HAWA NI WEZI, SAWA NA UMOJA FUND.
 
kaka mimi mwenyewe ni mteja utt na hakuna gawio la faida ila wa reinvest faida inayopatikana hvyo pesa uliyo wekeza inapanda na uki hitaji toa faida unaomba statement unaangalia pesa iliozidi unaitoa kwa kujaza form na pesa huingizwa kwenye akaunt yako ndani ya siku kumi..hvyo unakosea sana unaposema utt ni wezi.
 
Wadau hata mimi ninampango wa kuwekeza huko. ila baada ya miaka kama mitatu hivi nataka nichukue hela yote nje hii inawezekana
 
Hawa sio wezi. ukitaka pesa yako unaweza toa ndani ya siku kumi. Mi ni mmojawapo wa wawekezaji. Nami nilipata gawio mwaka mmoja huo uliotaja. Baadae walibadailisha utaratibu kwamba mtu anayehitaji pesa anaweza uza vipande kulingana na pesa unazohitaji ambazo unazipata ndani ya siku kumi. kwahiyo badala ya gawio hizi pesa huziwekeza mpaka unapozihitaji.

kuhusu hisa ni kwamba unaweza pata sana au ukapoteza sana kwasababu zinabadilika sana kwa bei. Vipande vina return ambayo kidogo ina uhakika kuliko hisa.
 
vipi ukiwalinganisha na benki za kawaida.. wana unafuu wowote?

Mkuu kwa uelewa wangu kwa hawa jamaa huwa hawana makato mengi ukilinganisha na yale yaliyopo kwenye mabenki. Makato pekee ninayoyafahamu kwa mfano kwenye mfuko wa Umoja ni 1% pale utakapokuwa unauza vipande. Kwa mfano ukinunua kipande leo kwa bei ya shilingi 200 (huu ni mfano) na ukaja kukiuza kipande hicho labda baada ya mwaka 1 ambapo bei itakuwa shilingi 250, hutauza kipande chako kwa shilingi 250 bali itakuwa shilingi 247.5 (asilimia 1 pungufu).
 
Wadau hata mimi ninampango wa kuwekeza huko. ila baada ya miaka kama mitatu hivi nataka nichukue hela yote nje hii inawezekana

Hilo linawezekana mkuu, unaruhusiwa kuchukua hela yako wakati wowote. Unaweza kuamua kuuza idadi yoyote ya vipande wakati wowote utakaotaka na wanasema unalipwa pesa yako ndani ya siku kumi. Gharama pekee waliyonayo ni 1% pale utakapokuwa unauza vipande vyako.
 
Mkuu kwa uelewa wangu kwa hawa jamaa huwa hawana makato mengi ukilinganisha na yale yaliyopo kwenye mabenki. Makato pekee ninayoyafahamu kwa mfano kwenye mfuko wa Umoja ni 1% pale utakapokuwa unauza vipande. Kwa mfano ukinunua kipande leo kwa bei ya shilingi 200 (huu ni mfano) na ukaja kukiuza kipande hicho labda baada ya mwaka 1 ambapo bei itakuwa shilingi 250, hutauza kipande chako kwa shilingi 250 bali itakuwa shilingi 247.5 (asilimia 1 pungufu).
Nashukuru... ni kweli waweza tumia vipande vyako kama dhamana kupata huduma za kifedha kama mikopo na kadhalika?
 
Nashukuru... ni kweli waweza tumia vipande vyako kama dhamana kupata huduma za kifedha kama mikopo na kadhalika?

Mkuu sina hakika kama hilo linawezekana kwamba ukatumia vipande vyako kama dhamana kukopa kwenye taasisi zingine lakini ninachojua ni kwamba wao wenyewe wana microfinance yao na wanaweza kukukopesha hadi asilimia 85 ya thamani ya vipande vyako lakini unarejesha kwa riba. Ni kwa muda gani unarejesha hilo nalo bado sijalifanyia uchunguzi.

Kama unaweza jaribu tu mkuu kwa sababu wakati mwingine ni kuchukua risk pia. Hawa jamaa wakati wanaanza watu walinunua kipande kwa shilingi 70 kama sikosei na nimeangalia kwenye tovuti yao leo, kipande kinauzwa shilingi 338 na senti kadhaa. Hebu piga mahesabu wewe mwenyewe halafu utaona waliowekeza wakati huo wana shilingi ngapi kama faida endapo wataamua kuviuza vipande vyao leo!
 
Mkuu asante kwa maelezo, ningependa kujua zaidi kuhusu UTT, lakini kabla sijaenda ofisini kwao nasoma website yao naona aina tofauti nini kinasababisha bei kuwa tofauti? Idadi ya watu kwa kila fungu au? Na unaposema kwa hela ndogo ununue vipande sio hisa, kwenye web yao sioni hilo neno, vipande ndio 'chips?' na je nitawaambiaje wakati nanunua kuwa sio hisa au watatoa maelezo zaidi. Uelewa wangu kuhusu hisa ni mdogo na info nyingi zimekuwa na negativity kiasi sikuweza kufatilia kabisa.

Back
Top Bottom