winnerian
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 335
- 530
Watu wanafurahia kuhusu uwekezaji angali wengine wanabeza na wengine hawajui ni nini kinaendelea
Kwenye jamii kuna makundi matatu ya watu.
1. Kundi la wengi, wale wanatumia nguvu akili, jasho na damu kutengeneza mkate wa siku.
2. Kundi la wastani, wale wanaotumia akili nyingi kutafuta mkate wa siku
3. Kundi la wachache, wale ambao PESA INAFANYA KAZI KWA NIABA YAO. Hapa hakuna akili nyingi, nguvu wala jasho lolote.
Sasa turejee kwenye uwekezaji wa pesa kwenye hisa, mifuko ya pamoja na hati fungani.
A. Wewe kama bado haujatengeneza kiasi flani cha pesa ambacho ukiwekeza kinarudisha pesa ndefu usibeze wanaowekeza kwasababu wao tayari wameshaona mbali na wapo tayari kuwekeza,endapo kuna chaguo kati ya kutumia nguvu na akili kupata hela au ikatokea hela ikafanya kazi kwa niaba yako basi utakimbiloa pesa ikufanyie kazi na sio kusumbuka huku na kule. Pamoja na biashara wawekezaji wanajua pesa ndio inayotakiwa kubebeshwa mzigo mkubwa wa kufanya kazi.
B. Kuna watu tayari wameona fursa katika uwekezaji na wanazitumia ipasavyo. Mfano mtu ana 500m na bado yupo kwenye biashara inayojiendesha bila stress unataka huyo mtu akatunze 500m halafu mwisho wa mwaka aikute 500m au akawekeze mahali 500m halafu mwisho wa mwaka anaikuta ipo 550m?
C. Watanzania ni warahisi sana kulisemea jambo kwa hasi kabla hata ya kufanya tathumini sahihi na kulitazama kwa pande zaidi ya tatu hadi nne. Wawekezaji wengi leo hii wana akiba ya kutumia na inajiongeza kila hadi watakapoondoka duniani na hatimae kuwarithisha watoto wao na wajukuu.
D. Kama bado upo kundi namba moja (1) hapo juu pambana sana na usiwe mlalamishi. Fanya kazi kwa akili, nguvu, jasho na damu hadi uwe kundi namba tatu (3) hapo juu.
Mfano wa Hisa
Mwaka 2020 hisa za CRDB zilishuka hadi shilingi 90 kwa hisa moja.
Mwaka 2023 hisa moja ya CRD ni shilingi 460
Ikiwa mwaka 2020 mtu mwenye 500m alinunua hisa za 500m atakuwa alipata hiaa =5,555,555.56
Sasa kutoka shilingi 90 hadi 460 kuna ongezeko la =370
Mtu huyu angeuza hisa zake zote mwaka 2023 angepata =5,555,555.56x370 sawa na =2,055,555,557.2 (bilioni mbili)
Ukichukua bilioni 2 toa 500m unapata faida ya 1.5billioni. Ndani ya miaka mitatu net.
Gawanya 1.5bilion kwa miezi 36 ni sawa na =41,666,666.67 kwa mwezi.
Ni biashara gani mtu utafanya bila nguvu, akili wala jasho na ukapata 41m kwa mwezi?
JAPO KUNA HASARA NDIO lakini hii ni hisa tu. Kuna mifuko ya pamoja (UTT Amis na hatifungani ambazo loss kutokea ni nadra sana.
Hivyo usibeze wanaotaka kuwekeza. Wewe kama hujafikia level ya muwekezaji pambana na level yako ya kutumia misuli na akili.