Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 41,983
- 12,702
Nilipoanza kazi nilionywa na wenyeji wangu juu ya huyu mama mfagizi wa hapa ofisini. Yeye ni mke wa mtu, na ni mama mtu mzima. Sijui kutokana na ugumu wa maisha au tabia tu, alikuwa na mchezo wa kutoka kimitegomitego. Kafumaniwa na mabosi wake zaidi ya watano, mwisho wa fumanizi mgoni analipa tu faini ya shilingi laki tano. Watu kuja kushtuka kuwa ulikuwa ni mchezo uliokuwa unachezwa na huyu mama kwa kushirikiana na mume wake, wakware wengi walishachomolewa pesa sana tu. Thanks God alihama mji na kazi aliacha....