Hii kolabo ya kijasusi kati ya mama na binti zao inakatisha sana tamaa vijana waoaji

Teslarati

JF-Expert Member
Nov 21, 2019
1,735
6,796
Wanajamvi habari za muda huu.

Wanaume wenzangu tuwe makini sana kuna aina mpya ya ujasusi unaendelea yan binti anakutambulisha hadi kwa mama yake kumbe wana lao jambo ili wakuaminishe na uchunwe zaidi ukiwa huna hofu yyt. Na kumbe behind the scenes mko zaidi ya watatu na wote mmetambulishwa kwa mama mtu. Mama mkwe nae akipata shida anakucheki moja kwa moja na wewe unatoa tu kumbe majasusi wakubwa

Yamemkuta rafiki yangu na nikamuuliza kama naweza andika hii story JF akasema niandike tu.

Iko hivi, Ijumaa jioni iliyopita nilikutana na mdau wangu mmoja mpambanaji halafu mjanja sana ila huwa ana kidemu kilimpa nini sijui akakiganda sana. Sababu kila baada ya gambe hajawahi kutoka na malaya pale. Sasa jana tumepiga gambe akaja barmaid mpya maeneo yale nikashangaa jamaa kaniwahi kuanza ku-flirt na kale kabinti hadi akakaambia kaagize kaje pale.

Baadae dem akatoka kwenda kuhudumia wateja ikabidi nimuulize jamaa yangu kwanini leo kaniwah wakati anajua hizo ni nyama zangu kabisa na sio kawaida yake. Jamaa si ndo akaanza kufunguka. Jamaa anasimulia
......

Kaka bwana yule dem si alituchezesha akili wanaume watatu akishirikiana na mama yake. Dem nikiwa nae alikuwa ananipa mapenzi sio ya dunia hii, nilikuwa najiona peponi. Baada ya mwezi akasema akanitambulishe kwa mama yake nami kwa kuwa nilishakolea nikasema sio mbaya, dem tukapanga weekend moja nikaenda alipopanga mama yake nikaandaliwa msosi mkali na bahati nzuri alikuwepo mdogo wake wa kiume likizo(huyu dogo ndo alichoresha game bila kujua) so ikawa shangwe sana kama vile ndo natoa mahali kumbe ni kutambulishana tu.

Basi bwana hio siku jioni nikawasha chuma tukarudi nyumbani na huyo dem vzr tu. Baada ya wiki mama mtu akanipigia simu ameenda kuchukua mzigo wa vitenge ila kapungukiwa laki 7 anaomba nimsaidie hata kdg, sasa kidume kwa sifa zote ili kujenga uhusiano mzuri na mama mkwe nikatuma laki nane kabisa na ya kutolea.

Mama mtu akafurahi na kumbe alimwambia mtoto wake (hapa baadae akajua walipanga hii njama toka mwanzo) jion yake binti katoka kazini akaja kwangu na shangwe kibao, alinipeti, tukapika, yaan tukawa kama wahindi kwa masaa yale. Game lake kaka nilokuwa napewa hata ukipewa wewe naapia hutomuacha yule dem.

Baada ya mwezi nilipigwa tena kizinga cha 1m nikatoa. Kuanzia hapo vikawa vizinga kona zote, sio kwa mama mtu, sio kwa mtoto mtu. Nikazoea anyway sababu najua vizuri vina gharama na si unamjua yule dem alivyokuwa mzr na kabarikiwa kila kitu.

Sasa bwana kaka nimekaa hivyo mwaka na nusu nikaachana na mamalaya kabisa nikiwa najua nikimaliza kale kamjengo kangu nitangaze ndoa kwa huyu binti, si ndo mwezi February mwaka huu nikapata tips.

(mimi: enhee master ikawaje ukapata tips)

Si unakumbuka nilisema ana mdogo wake wa kiume alikuwa likizo siku naenda kutambulishwa, sasa huyo dogo alimaliza chuo mwaka jana akanicheki nimpe mchongo ila nikamwambia sina kwa sasa labda ntamuangalizia kwa wadau. Mwaka jana mwezi wa 12 zikatoka chance mahala nikamtafuta dogo nikamconnect hadi akapata kazi na mshahara mzr tu. Hapo hatuongelei kitu chochote khs dada yake.

Sasa dogo akaja kuchomesha mchezo, unajua pale analipwa laki 6 kwa mwezi, ni mshahara mzr kwa anaeanza maisha na fresh diploma graduate. Kumbe dogo roho ikawa inamsuta akijua mimi nilishaachana na dada yake(kumbe bado) lkn bado namsaidia na ndo maana hata hakuwahi kuongelea khs dada yake muda wote namtafutia kazi.

Kumbe mimi bado sijaachana na dada yake, dogo alifikiria nimeachana na dada ake sababu mwaka jana huo mwezi wa kumi jamaa mwingine alitambulishwa pale na dogo akiwepo na akashuhudia.

Sasa dogo siku moja nikapita anapofanyia kazi ilikuwa jioni nikawa na ishu pale, nlipomaliza nae akawa anatoka anarudi kwa mama yake nikamwambie achukue lift akaweka visingizio, sijui ni nn tu kikanilazimisha nikamwambia nitampitisha huko anakoenda, dogo akaingia kwenye gari.

Sasa mule ndani tukawa tunapiga story, mie huwa mkimya sana, dogo akaanza kunishukuru pale eti nina moyo wa ajabu sana, mie nikasmile nikamuuliza kwanini. Bwana kaka dogo si ndo akayamwaga manyanga pale akijua mie nishaachana na dada sababu kuna mtu ashatambulishwa tena kumbe mimi jana yake nimetoka kumtomber huyo malaya kaka.

Kizuri mie ni mtoto wa mjini, ungekuwa wewe kaka ungepanic sana (nikacheka kweli hadi nikasimama watu wakaanza kushangaa), hapana kaka usicheke huo ndo ukweli. Sasa baada ya kusimuliwa pale nikamjibu huyu dogo kwamba, asiingilie haya mambo, ni kati ya mm na dada yake tu, hata kama tumeachana mie ntamsaidia kama naweza. Dogo akashukuru sana.

Sasa nikaanza kufanya upelelezi ndipo nikaja kugundua tupo watu watatu pale na wote dem anatuhudumia swaaaf kabisa kiasi kwamba kujua ni ngumu, yule dem ana simu mbili, iphone 12 (nilimnunulia) na samsung nilomkuta nayo. Kwa muda wote hakuacha weak point yyt ilionifanya nimuhisi anacheat zaidi ya kumkwepa tu baadhi ya vizinga mara chache saaaana.

Ila tu niseme kaka huyu binti kama sio jasusi basi wamuajiri huko, alinichanganya kiasi kwamba mtoto wa mjini nikanasa kabisaaaaa. Huwa nafikiria aliwezaje kucheza na wanaume watatu kwa wakati mmoja bila kuacha traces lkn nashindwa kuelewa, pia mama yake alimpa ushirikiano sana sababu kuna muda unapiga simu anakuwa nayo mama yake anasema dem kaenda kufanya so and so, nadhani hapo ndo anakuwa anakatikia bolo jingine.

Baadae nilipomaliza upelelezi nikamuita dogo nikamsimulia ili ajue tabia ya mama yake na dada yake, sababu dogo alikuwa hajui kitu na ndo alinisaidia (japo bila kujua) kusoma mchezo ulivyokuwa. Baada ya hapo nikakinukisha pale kwao nikamwambia yule mama alipe hela zote nilizompa la sivyo ntasambaza stori kwa jamaa wengine,. Na kumuharibia cv pale mtaani.

Bwana kaka yule mama kala zaidi ya 10m zangu toka nitambulishwe pale kwa kisingizio cha duka lake la nguo. Kumbe mama mjanja bwana, akasema nikithubutu hivyo watanifungulia kesi eti nilitaka kumla mama na mtoto, nikaishia kuwapotezea tu, lkn akilini nikasema hawa ni majasusi kwelikweli.
.....

Mwisho wa kunukuu.

Wanaume wenzangu nimeandika story kwa herufi kubwa ili kuonesha msisitizo, hii ni true story kutoka kwa jamaa yangu humuhumu mjini maeneo ya Tabata.

Nimeona nimalize weekend kwa kuwajulisha hii aina mpya ya ujasusi.

Sikutaka mambo ya "Itaendelea" ndo maana nimeandika ikawa ndefu sana, someni mjifunze kitu.
 
Nilishasema kama demu wangu anatarajia nitakuja kumnunulia mama yake hata vocha asahau hilo ni jukumu la baba yake sio mimi kama nililima na mama wa mzazi mwenzangu hakuambulia hata kilo ya mchele uzuri hata yy anajua sitaki anieleze shida na matatizo ya familia yao
 
Ishanikutaa hyo Dem na mama yakee walicheza mchezo ila mm nikacheza zaidi Yao nikalaa Dem na mama yake ,mpk Leo nikiwa na hamu namshtua mama mtu au mwanae wanaibuka geto nshwahi wapiga 3somee.
Hii kitu hii 🤔🤔
 
NTASAMBAZA
Wanajamvi habari za muda huu.

Wanaume wenzangu tuwe makini sana kuna aina mpya ya ujasusi unaendelea yan binti anakutambulusha hadi kwa mama yake kumbe wana lao jambo ili wakuaminishe na uchunwe zaidi ukiwa huna hofu yyt. Na kumbe behind the scenes mko zaidi ya watatu na wote mmetambulishwa kwa mama mtu...
Bora hilo ni uzembe wa mchunwaji.

Vipi pale baba fedha zako zinapotumika kufanya abortion za binti yako huku mkeo (mama yake) ndo akiwa director? Siyo 1 au 2, kila mwaka.
 
Nimetokea kanisani lakini sijaona

JamiiForums-917047017.jpg
 
10M kwa Malaya... Hivi huyo jamaa yako alishawahi kumtumia Mama yake hicho kiasi cha pesa?
10m kadumu na huyo dem kwa kama miaka miwili hv.

Gawanya hio hela kwa miaka miwili ndo utaelewa, na kama unakaa mjini itakua rahisi zaidi kuelewa.

Personally simshangai sana
 
Back
Top Bottom