Umewahi pata adhabu hizi??

Kwani hapo ni shule au depo?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Tosamaganga High School miaka ya tisini wakati Mavika ndiyo mwl. wa nidhamu, kosa la kutoroka au kutofikisha wastani unaotakiwa, adhabu ilikuwa kuchimbua mti. Pata picha ardhi ya tosa ilivyokuwa na mawe tupu, unaanza kukata mti mpaka unabakia shina halafu unaanza kupangua mawe yote mpaka ukute mizizi. Hapo hakuna kuingia darasani mpaka umalize adhabu.

Enzi za huyo mwalimu ukibahatika sana adhabu ndogo kwa kosa dogo ni 'suspension' wiki mbili halafu uje na mzazi, hata kama kwenu ni Tanga utakwenda tu bila kujali kama anamuongezea mzigo mwanafunzi na mzazi wake ambao wote ni walala hoi. Alikuja kuvunjwa nguvu na Mkuu wa Shule mpya Mr. Mkangwa, Intellectual huyu alisema yeye amekuja kuhakikisha vijana wanasoma na wanafaulu na sio kuwafanya wakose masomo eti kwa kisingizio cha adhabu, kama ni kosa limefanyika mwanafunzi alipata adhabu stahiki hapo hapo na kuruhusiwa kuendelea na masomo. Hureee Mr. Mkagwa popote ulipo nchini Tanzania, mungu akubariki sana. Ulinifanya mimi nifikie level hii nilipo, najivunia kuwa mwanafunzi wako.

Huyo Mavika mnoko mpaka siku anateuliwa kuwa Afisa Taaluma wa Mkoa wa Iringa wanafunzi walifanya sherehe sio kwa kumuaga bali kufurahi kuondoka kwake.

Muulizeni Naibu Mkurugenzi wa Wizara moja nyeti, ambaye jina lake la pili ukiongeza herufi 'a' baada ya herufi ya kwanza linafana na eneo mmoja expensive sana hapa DSM atawaambia.

Big up to all Ex- Tosa Guys of 90's
 
Back
Top Bottom