umewahi ishi mazingira haya

Hizo ndo zetu, bado tunahangaika kujianasua kwenye nyumba hizo, Heri yenu mnaoziona kwenye picha, sisi bado tumo humo ingawa kwa sasa nipo mbele ya computer hapa cafe, jioni nazama humo.
 
Nimegundua kuwa humu kuna watu wa dot com, hii ni nyumba ya maana sana, ebu nenda Dom, Singida nk, mbona hii ni ya kitajiri sana tena ina bati!!!!!! we vipi?????
za dom singida nshaziona mkuu zile soo kabisa zimepigwa dongo juu chini.
 
Hii kwetu lazima uwe mwalimu enzi hizo, nyumba juu nyasi, mvua ikinyesha mnajikinga sehemu pasipovuja.
 
Mnatuumiza tu wenzenu, maana nyumbani kwetu nilikozaliwa nyumba nzuri kama hiyo ilikuwa ya katekista wa kanisa katoliki tu (kanisa lenyewe limeezekwa kwa manyasi!). Nyumba niliyozaliwa imejengwa kwa matofali ya tope na kkuezekwa kwa majani na matope (tembe), tulikuwa tukilalia ngozi za ngombe, tunajifunika kitenge cha mama, ikifika alfajiri mama anakuja kuchukua kitenge chake aende kufuatilia maji mtoni!! Acheni masihara nyie watoto!
 
Sasa hiyo haitoshi, mlango wa choo Gunia halafu juu kiko wazi. usiombe upepo usukume gunia na wewe ndo una.... Jamani tukumbuke tulikotoka
 
mkuu hizo nyumba za kawaida sana....

wiki mbili zilizopita nilikwenda kwetu mpwapwa....njiani kuna watanzania wenzetu wanaishi kwenye nyumba full udongo...zinaitwa tembe...bali hata hiyo nyumba yetu huko mpwapwa haina tofauti kubwa sana na hiyo kwenye picha..
 
mkuu hizo nyumba za kawaida sana....

wiki mbili zilizopita nilikwenda kwetu mpwapwa....njiani kuna watanzania wenzetu wanaishi kwenye nyumba full udongo...zinaitwa tembe...bali hata hiyo nyumba yetu huko mpwapwa haina tofauti kubwa sana na hiyo kwenye picha..
he hee,mzee atakuwa mwalimu mkuu,au mwenyekiti wa kijiji au lodi fulani hivi
 
Duuh umenikumbusha mbali Enzi ya Marehemu Babu yangu anaishi Mkuranga miaka ya Sabini iliyopita Ehh kazi kweli je akija Simba itakuwaje? mimi humo ndani siwezi hata kupata Usingizi Ama kweli Mzarau kwao ni mtumwa ehhhh (MIAFRIKA BWANA NDIVYO ILIVYO)
 
unajua kwann tunafell mitihani?hatufati instruction"tumeulizwa umewahi kuishi mazingira hay?sio kutembelea

Ndio nilikuwa na maana hiyo kuonesha vipi mnafeli, hata kama umekaa hapo kwa siku moja basi kwa mana hiyo ndio umesha onja maisha ya hapo .;)
 
Duh, mzee hizi si ndiyo nyumba ambazo tumezaliwa na kukulia. Tena hii ipo bomba sana mkuu. Inaelekea mwenzetu matawi ya juu eheee??!
 
mbona pako bomba sana mazee bati haya ni maendeleo ati?
ebo huyu katokea wapi huyu ..........
 
mbona y akawaida tu, kuna watu wanaishi kwenye vibanda ukikion huwezi amnini hata kuku anaweza kulala humo......
 
Hapo pako poa sana tu na tumishi sana maeneo hayo ukiwa na amani ya roho hakuna kibya ndugu.
 
Naona hapo kidogo unakosea mh.. .. mh sema nimetoka mbali .... ..... teh teh teh .... Sio wote waliokulia katika mazingira kama hayo.
Kama ungekuwa umesoma michango ya wengi humu, ungekuwa umegundua kuwa wengi tumetoka katika mazingira yanayofanana na hayo au duni zaidi ya hayo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom