101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,040
- 2,121
Harakati za maisha ya kujitegemea zinamambo mengi sana na tunapitia mengi sana hususani kwenye nyumba za kupanga.
Kwa ujumla Mpaka hivi sasa tangu nimeanza kupanga nyumba Kwa miaka 10 nimefanikiwa kuhama nyumba zaidi ya Saba ikiwa Kwa sababu mbalimbali
Nyumba ya Kwanza
Nakumbuka nyumba ya Kwa kuishi ni maeneo ya tabata BIMA Karibu na Kota za nssf ambapo nilipanga chumba kimoja kama msela Tu sina mke, mwenye nyumba ni mama mjane wa kichaga nilikaa Kwa muda wa Mwaka mmoja tukashindwana Baada ya kunipandishia Kodi kiholela nikahama
Nyumba ya pili
Liwiti tabata Karibu na barakuda hii nyumba ilikuwa ya urithi nayo Ila wamiliki ni watoto wa Marehemu nyumba ilikuwa nzuri Tu na sio mbali na road Ila Shida ilikuwa haina msimamizi kila mtoto anakudai Kodi wew ukishindwa kuwabananisha ndugu utalipa Kodi mara mbili sijui walikuwa wanafanya makusudi au la.
Nyumba ya tatu
Hii ilikuwa maeneo ya tabata shule Kwa nyuma mwenye nyumba ni mtu wa dini sana nakumbuka hii nyumba nilikaa miezi miwili Tu nikapewa notes ya kuhama Kwa kigezo cha Mimi kuingiza mwanamke ndani ya nyumba
Mwenye nyumba alikuwa hataki uzinzi ndani ya nyumba yake nikahama.
Nyumba ya nne
Hii nilikaa Kwa siku 6 nikashindwa nakaomba niludishiwe hela yangu nikaambiwa na mwenye nyumba hela Hana nikaongea na dalali akaleta mpangaji mwingine akanilipa pesa nikaondoka Shida chumba kilikuwa kidogo kupelekea baadhi ya vitu vyangu kubaki nje.ingawa nyumba ni mzuri maana hii nilionyeshewa kwenye WhatsApp na dalali Baada ya Mimi kuwa bize na kazi
Nyumba ya tano
Hii nilikaa maeneo ya tabata BIMA pale nyuma ya st Mary nyumba hii nilihamia Wakati wa kiangazi bila ya kujua kuwa nimeingia cha kike Kwa sababu Wakati kiangazi ni sehemu nzuri sana Ila ikinyesha mvua Bana maji yote ya barabarani yanaingia ndani kipindi hiko Ile Njia haijapigwa lami na haina mitaro yaani kufumba na kufumbua unaamka asubuhi maji yamejaa chumbani. Hii nyumba nilikaa miezi minne nikasamehe Kodi ya miezi miwili
Nyumba ya sita
Hii nyumba nilihamia Baada ya kutoka kwenye mafuriko nikakaa hapa Kwa muda ya miezi sita ya Kwanza ilikuwa na Amani tatizo lilikuja Baada ya binti ya mwenye nyumba kuhamia hapo ndani yeye maisha yalimpiga pamoja na Bwana wake ikabidi warudishe mpira Kwa kipa .akatengeneza mazingira ya kunizoea akafanikiwa sasa ikawa mazoea yamepita mipaka maana alikuwa anapenda kitonga mnoo anakuja kuomba chumvi,sabuni mara sukari ikawa maisha Yao Mie ndio nayaendesha na akiazima kitu harudishi nikapiaga hesabu nikaona hii nyumba hainifai nikahama
Nyumba ya Saba
Nyumba hii nilikaa Kwa Mwaka mmoja na nusu mwenye nyumba jamaa mmoja anapiga mishe kariakoo Ila mkewe ni mganga hili sikujua Wakati nahamia,nilikuja kujua Baada ya kusikia harufu za ubani na udi zilizokuwa zinafukizwa ndani ya nyumba nikajua labda ni dawa za mbu,Kumbe mama alikuwa anapandisha maruhani
Nakumbuka kwenye hii nyumba niliishi Kwa misukosuko sana na màmbo yangu mengi yalikuwa hayaendi huyu mwenye nyumba hapendi mpangaji awe na maendeleo nilikuja na friji akataka nimuuzie nikagoma akanipandishia hela ya umeme Wakati na yeye Pia anafriji mbili na anauza barafu,juice na ice cream ndipo nikashikwa sikio na wadau wa mtaa nikaambiwa huyo mama mwenye nyumba ni jau na anatabia ya kuroga wapangaji. Duh nikahama
Nyumba ya mwisho
Hii nyumba ilikuwa ni mpya kabisa wapangaji tulikuwa watatu tu na mwenye nyumba haishi na Sisi. nimeishi Kwa Amani sana tena ilikuwa kama yangu nakumbuka Wakati nahamia dalali aliniambia hapa utaishi kama kwako na ukitoka hapa utahamia kwako na kweli nilikaa hii nyumba takribani miaka minne na nusu nikafamikiwa kujenga yangu na kuoa na kupata na mtoto mpaka nahama kuna watu walijua pale ni kwangu Kumbe ni nyumba ya kupanga Tu.
Hii ndio experience yangu kwenye nyumba za kupanga sijui kwako mdau ikoje
Nawasilisha