Hii itakuwa kongo. Inanikumbusha ile ajali ya ndege ya mwaka jana au juzi iliyosababishwa na mamba aliyekuwa akisafirishwa kwenye ndege usafiri wa watu. Mamba sijui alitokajs kwenye kasha lake akajichanganya na wasafiri ikawapatashika mpaka ndege ikaanguka. Loh!
Mzee ''mbuzi mzee'' pasipo shaka ni moja ya ndege zinazofanya safari zake DRC, mitaa ya Entebbe-Bunia-Beni, Bunia-Goma-Kisangani, Bukavu-kisangani-Kinshasa. kwa kifupi usafiri wa anga DRC ni hatari zaidi ya unavyoweza kufikiria. kwanza karibu ndege zote zinazofanya safari ndani ya DRC zimechoka hujapata kuona na zinapakia mzigo hakuna kipimo, korido yote huwa imejaa mizigo na mabegi na kama inavyoonekana hapo kwenye picha yako mabegi yanakua juu ya seats, yaan kwa kifupi mzee ni mawazo mno usafiri wa ndege DRC, lakin hakuna jinsi inabidi upande tu hizo ndege zao, maana hakuna barabara DRC kabisa Congo, na kama ni umasikini wa watu DRC imevuka viwango zaidi ya kawaida.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.