bullet
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 1,047
- 537
Mambo ya kuangalia unapotaka kunua mfumo wa sola.
Watu wengi wametamani kuwa na nyumba nzuri na yenye umeme wa uhakika .Tatizo linakuja kwamba Tanesco imeshindwa na pengine kwa miaka 10 ijao itaendelea kushindwa ku supply umeme wa kutosha wa kukidhi mahitaji yaliopo na yatakayo ongezeka , hili limeweka familia nyingi- ukiachilia mbali viwanda katika power nightmare.
Wengi wanajiuliza nini wafanye kwanza waweze pata umeme kama hawajafungiwa umeme[ hapa sitaki kuelezea usumbufu uatakao upata wa kufuatilia wafanyakazi wa Tanesco pesa utakayolipa kulobby na hata muda kwa kweli ni kizungumkuti] pili wale waliofungiwa ni kama hawana umeme kwani muda mwingi wamekuwa kwenye giza na hata ratiba ya mgao wenyewe haieleweki labda kwa taneso pekee.
Wengi wamezunguka huku na huku na hata kwenda kwenye maduka mbalimbali ya umeme mbadala kama magenereta na sola. wale wa majenereta kama wemeweza pata generta nzuri nyingi ziko kati ya Mil 2.5- mpaka 12. kwa saizi ya nyumba ya kawaida lakini pia hii itaambatana na ununuzi wa mafuta kila siku[ bei yake nayo haieleki kama umeme wa tanesko], pia umeme huu umbatana na kelele na maintenence isiyoisha.
wale walioweza nunua za bei raisi nazungumzia kati ya laki 1.5-mill 2 basi nyingi labda hazifanyo kazi ndani ya miezi miwili au mitatu na hapa baada ya maintenenace cost ya kila wk kumwita fundi. bila kusahau kelele na matumizi makubwa ya mafuta bila kujai kupanda kwa gharama za mafuta.
Kwa wale walioweka sola na kubahatika kukutana na bora sale dealer basi wame hesabu maumivu kwani nyingi pia zimeacha kufanya kazi ndani ya miezi miwili mpaka mitano bila kujali gharama kiasi gani ulilipia hasa unafuu ulipotumika kama kigezo cha manunuzi.
Kwa wale waliobahatika kuwapata wataalam thabit wanaothamini kazi zao na mteja basi walipata maumuvu ya mwanzoni ya kutoa pesa lakini wameendelea kupata furaha ya muda mrefu ya system inayofanya kazi vizuri na bila kuhitaji tena kuingia mfukoni kumtafuta fundi wala kunua mafuta .
Sasa basi wengi mtajiuliza ni nini tufanye kuondoka na adha hii ......
Majibu ni marefu na kwa leo nitawaletea kiasi kwa kadri nitakavyoweza.Nitarejea kesho kwa maelezo zaidi.... mnaopitia forum hii msichokee kupitia kila siku ili kuelimika zaidi......
- Kununua sola inahitaji maandalizi na kupanga kwa muda mrefu ikiwezekana kabla ya kuanza kujenga nyumba. kumbuka sola nzuri intosha kuendesha shughuli zote za nyumbani na ksuiwe na haja ya umeme wa tanesco tena.
- Unahitaji kuzunguka na kuwaona wataalamu wanaoweza kukufanyia makadilio mazuri ya mahitaji yako na kukupa option mbalimbali ili kukusaidia kufanya uamuzi.
- Unahitaji kujua maduka yenye uzoefu na biashara hiyo na hata kwenda online kupata uelewa zaidi. kumbuka usije ukajisumbua kununua online, unaweza pata kanyanga ni vizuri ununue kwa certified registered solar contractor ili upate guantee ya vifaa vyako. kwani kumbuka sola ni investment kubwa inayoitaji guarantee.
- Unahitaji kujua sifa na specification na kuweza kutafsiri kwa lugha rahisi hasa manufaa yake kwako. Nitawaletea taratibu somo hili kila nitakapokuwa napata nafasi kwani nahamini mteja anapofahamu zaidi anakuwa katika wakati mzuri wa kufanaya maamuzi hata kutunza kifaa chake.
- Unahitaji kujua upatikanaji wa spea kwani kifaa kimoja tu kikiharibika cha sola na ukishindwa kuki replace basi mfumo mzima utazimika na investment yako kwenda bure.
- Unahitaji kuwa na dealer amabaye atakuwa anakupa ushauri pindi utakapohisi mfumo wako unatatizo na ndio maana nasisistiza kunua hapa ncini ili muaazaji wake awe ndio mshauri wako.
Mie ni nayo solar system nimeitumia mwaka wa pili sasa. Zipo panels mbili, battery mbili njaa inventor. Inawasha taa muda wote (nyumba yangu ina taa zaidi ya 20), vile vile Anaweza kuonesha TV kwa saa nne mpaka tano. Pamoja na mambo madogo madogo kama kucharge simu nk.
Swali langu ni je naweza kui upgrade iweze kurun fridge kwa mfano au hata kunyoosha nguo? Ninahitaji kununua nini zaidi?