Umbali kutoka Dar kwenda Mwanza {km}

Kuanzia ubungo mataa mpaka mwanza airport kupitia njia ya dodoma - singida - shinyanga ni around kilometa 1200. Kama gari lako ni linajaza litre 80, utajaza mafuta dodoma na nzega kutegemeana na consumption. Kama halibugii sana wese, utajaza singida peke yake. Nakushauri usikimbie sana, epuka ajali. Watakaokucheka au kukudharau kuwa unaenda taratibu, hawapendi maisha yako. Be safe!
 
By MULANGILA:
Mkuu hata mimi ni shuhuda. Nimeendesha peke yangu bila kupumzika kutoka Dar(Segerea) hadi Bukoba(Kanyigo) Km 1542 bila kupumzika na nilitumia masaa 18.

Hajasimamishwa na trafic?? Yani Jamaa ni liongo la waziwazi kweupeeee.......alafu anafikiria ni sifa kufanyahivyo.
Taratibu za udereva kwa safari ndefu inatakiwa usiendeshe gari zaidi ya masaa 8, pasipo kupumzika ndio maana bongo kuna ajali kibao zinazosababishwa na dereva kusinzia, kumbe watu wenyewe ndio kama huyo jamaaa.

Kaka, kwa taratibu za udereva, hutakiwi kuendesha gari zaidi ya masaa 2 au KM 200 bila kupumzika japo kwa dakika tano. Waweza kunywa japo maji kidogo ukia umwpumzika. Refer kanuni za usalama za OSHA. Ki ukweli, ukizingatia hayo, ajali ni chache. Nilishazarau, yakanikuta, sasa nayaheshimu sana.
 
Hahaha duh! kwa hiyo kwa hiyo Bunda then Musoma then sijui Kisorya safari yote ya nini au unatumia gari la kampuni mafuta unachanja kadi tu....halafu umesahau kuwa gari ukiliweka kwenye pantoni linakua katika mwendokasi wa 0km/hr?

Ungekua umeizunguka nchi ungetoa alternative fupi na wala si hiyo miumbali ya kwenda hadi Musoma

Unadandia treni kwa mbele,lengo langu ilikuwa ni kuonyesha kuwa Ukerewe kunafikika kwa gari no matter utalivusha kwa pantoni au utalibeba kichwani.
 
Kwa umbali wa 1154km, lita moja kwa kila km 6 na bei ya petroli ya sasa ya 2183 utahitaji kutenga shilingi 419,864 (1154/6*2183) kwa ajili ya mafuta pekee ya kutosha huo umbali.

Kwa uhakika zaidi piga mahesabu ya 1200 km
 
kila siku mwanza mwanza kulikoni?
mana hata uwekezaji wa maana haupo,utalii ndo kabisaa
 
shilingi 419,864 (1154/6*2183) kwa ajili ya mafuta pekee ya kutosha huo umbali.[/QUOTE]

hahaha wanoko wa ofisini utawajua tu
 
Mkuu, hii chati umeitoa wapi?

Katika safari zangu mara nyingi huwa nasoma vibao vinaoonyesha umbali vilivyo kando ya barabara.Naamini vibao hivi vinawekwa na watu waliojenga hizo barabara (Tanroad au Halmashauri husika). Kwa mujibu wa vibao hivyo umbali wa DSM-Morogoro ni 193km (chati inaonyesha 200km) umbali wa Morogoro-Dodoma ni 254 (chati inaonyesha 258)!
 
Unadandia treni kwa mbele,lengo langu ilikuwa ni kuonyesha kuwa Ukerewe kunafikika kwa gari no matter utalivusha kwa pantoni au utalibeba kichwani.

mkuu naona "yo trippin" wewe ndio ulikua unadandia Apollo 11 kwa nyuma wakati wa take off, laiti kama ungesoma post tokea mwanzo wala ulisingeanzisha malumbano...am off period!!!
 
We unaleta fani yako ya umbumbumbu kwenye barabara. Mimi sioni alichokosea hapo. Hivi kama yeye ni dereva wa masafa ana haja ya kutaja source?

Wewe unapenda source au uhalisia kutoka kwa wanaoitumia barabara?

Mtu anaposema umbali ni km kadhaa na wote tupo hapa Tanzania, ukiwa na akili kidogo utajua tunazungumzia allowed maximum speed ambayo ni 80km/h +/- 10 na huo ni wastani kwani kuna milima na dharura za hapa na pale.

Wewe ulitaka tu kuleta ujuzi na kujifanya wewe ndio unajua saana. Pasiansi, Igoma na Isamilo hiyo yote ni Mwanza na sidhani mtu akishafika Nyegezi au Nyakato bado atauliza namna ya kufika Mwanza na ungekuwa na akili kidogo ungejua muanzisha mada anataka msaada wa kufika Mwanza na sio Pasiansi. Na ndio maana yeye aliuliza Mwanza na hakutuuliza kijijini kwake anakokwenda

Kama bado unabisha, karibu ila ujiandae. Mimi ni mjuaji kuliko wewe na muda ninao

Kwi kwi kwi ndugu yangu una hasira, duuh! Sasa sijui umejibu nini, aisee.. We ni kati ya watu wanaotuaibisha watanzania na kuonekana kama vile hatuwezi ku'argue in a logical manner! Usiishi kwa assumptions ukaita wastani, mimi safari ndefu huendesha at 110km/hr kwenye high way, na wengi ninaowajua huwa ndio spidi.. Hata ukiweka factor gani average yangu haitakuwa 80km/hr kwnye high way mjomba.. Kwa hlo tu umechemka (narrow perspective)..

Pili japo umesema wewe ni mjuaji kuliko mimi, Ninakubali. Lakini mimi ni muelewa kuliko wewe, avatar isikusumbue sana. Kama una akili kidogo utagundua mtu anayekaa Pugu kajiungeni na anayekaa Kibamba hawatatumia umbali sawa kwenda Mwanza, the same kwa mtu atakayeishia Buhongwa au yule atakayeenda Buswelu kwa Mwanza, tofauti ni zaidi ya kilomita hamsini, je hizi zote ziwe negligible?? Haujui hapo kuna fuel consumption na time spend.. Au unatumia miguu kufikiri!! Don't u knw a slight change gives big variance.. Ndg husisha ubongo.. Ndo maana nikaulizia starting point na finish point, ili hata kama makadirio yaendane na uhalisia.. Tofauti ya km 50 ni kubwa sana.. Vip huyu mtu akiwa anatoka goba au gezaulole?? Let's sometimes be specific and smart not too general in response.. Tufikirie japo kidogo! Mimi ninajua zero km ya Dar huanzia clock tower (sijui hata kama unakujua, maana unategemea habari za net kupata maendeleo yako binafsi au kuijua nchi yako) na kwa Mwanza ni hapa round about ya benki kuu (pia hukujui).. We unapost link sijui ya nani, skutaka ata kuifungua. Hujui zero-point wala end-point ya mwenyd thread..

Mimi sijamtajia km kwa sababu mbili
1. Sijui zero na end point Yake
2. Sina uhakika nazo sitaki kuhisia

Kifupi usiwe too general kwenye kujibu utaonekana masaburi.. Jaribu kuwa unafikiria na kugundua technique zote za maswali sio kuvamia tu na kuanza kujibu.
UTAFELI WEWE!

Mbumbumbu intelligent.
 
Mkuu, hii chati umeitoa wapi?

Katika safari zangu mara nyingi huwa nasoma vibao vinaoonyesha umbali vilivyo kando ya barabara.Naamini vibao hivi vinawekwa na watu waliojenga hizo barabara (Tanroad au Halmashauri husika). Kwa mujibu wa vibao hivyo umbali wa DSM-Morogoro ni 193km (chati inaonyesha 200km) umbali wa Morogoro-Dodoma ni 254 (chati inaonyesha 258)!

Inategemea na mpimaji kaanzia wapi kupima na kamalizia wapi(soma post #47).........wengine huanzia Ubungo na wengine huanzia pale clock tower na wengine huanzia hata Kiluvya!
 
Ni kweli isipokuwa unategemea unapima kutumia barabara gani? Morogoro ukliingilia Old Dar es salaam road (Bigwa) ni 198km na ukiingilia Tanzam Highway(Msamvu) ni 200km

Hiyo barabara ya zamani sidhani kama inatumiwa kwenye vipimo vya umbali vya either SUMATRA au TANROADS maana si barabara kuu...mi nilidhani Msamvu umbali ungepungua ukilinganisha na kule stand ilikuwa zamani
 
Umbali official ni mpaka kile kiplefti cha stand ya zamani(MOR) toka Clock tower pale Samora(DAR)......ukipitia old Dar es Salaam road panakuwa pafuti zaidi ya Msamvu.....Hao TANROADS/SUMATRA hawajawahi kufanya vipimo vyo bali wanaendelea kutumia vilivyoachwa na mkoloni ambe aliitumia hiyo Old Dar es Salaam road wakati huo ni barabara kuu. TANZAM highway haikujengwa na mkoloni
 
mhh mkuu hiyo chat mbona kama siiamii Dar - Moro, kilomita 200???

Mkuu, hii chati umeitoa wapi?

Katika safari zangu mara nyingi huwa nasoma vibao vinaoonyesha umbali vilivyo kando ya barabara.Naamini vibao hivi vinawekwa na watu waliojenga hizo barabara (Tanroad au Halmashauri husika). Kwa mujibu wa vibao hivyo umbali wa DSM-Morogoro ni 193km (chati inaonyesha 200km) umbali wa Morogoro-Dodoma ni 254 (chati inaonyesha 258)!

Nimeitoa kwa mkuu tajwa hapo juu
 
Inategemea na mpimaji kaanzia wapi kupima na kamalizia wapi(soma post #47).........wengine huanzia Ubungo na wengine huanzia pale clock tower na wengine huanzia hata Kiluvya!

Umbali official ni mpaka kile kiplefti cha stand ya zamani(MOR) toka Clock tower pale Samora(DAR)......ukipitia old Dar es Salaam road panakuwa pafuti zaidi ya Msamvu.....Hao TANROADS/SUMATRA hawajawahi kufanya vipimo vyo bali wanaendelea kutumia vilivyoachwa na mkoloni ambe aliitumia hiyo Old Dar es Salaam road wakati huo ni barabara kuu. TANZAM highway haikujengwa na mkoloni

Umbali wa DSM-Morogoro wa 193km unaonekana kwenye barabara ya sasa (sio old DSM road)!
 
Inategemea na mpimaji kaanzia wapi kupima na kamalizia wapi(soma post #47).........wengine huanzia Ubungo na wengine huanzia pale clock tower na wengine huanzia hata Kiluvya!

Umbali official ni mpaka kile kiplefti cha stand ya zamani(MOR) toka Clock tower pale Samora(DAR)......ukipitia old Dar es Salaam road panakuwa pafuti zaidi ya Msamvu.....Hao TANROADS/SUMATRA hawajawahi kufanya vipimo vyo bali wanaendelea kutumia vilivyoachwa na mkoloni ambe aliitumia hiyo Old Dar es Salaam road wakati huo ni barabara kuu. TANZAM highway haikujengwa na mkoloni

Huo Umbali wa DSM-Morogoro wa 193km unaonekana kwenye barabara ya sasa (sio old DSM road)!
 
Back
Top Bottom