Umasikini mkali: Mwenyekiti wa Kijiji avaa shati lililochanika, January Makamba avua lake na kumpa

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
Katika hali inayoonyesha umasikini mkali unalikabili taifa,Mwenyekiti wa Kijiji huko Chalinze alikutana na Waziri January Makamba hali ya kuwa shati lake limechanikachanika

Mwenyekiti huyo aliyesifiwa na Waziri Makamba kuwa ni mtunza mazingira mzuri,aligusa imani NA huruma ya Waziri January Makamba ambaye alilazimika kumpa shati lake,kitendo kilichomfanya Mwenyekiti huyo wa Kijiji aangue kilio kikuu

TAFSIRI YANGU

Hali ya umasikini ni mbaya sana mitaanj,mtu mzima kutembea amevaa shati lililochanika,tena yeye akiliona ni shati maalum la kumpokelea Waziri aliye katika Ofisi ya Makamu wa Rais inasikitisha

Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani imekuwa ikitamba kwamba ni serikali ya watu masikini,je hii inamaanisha kwamba haitauondoa umasikini kwa kuwa ukiondoka basi inakosa mizizi?

Kilio cha Mwenyekiti huyo wa kijiji,mtu mzima,akatoa machozi baada ya kupewa shati nadhani ana mengi katika familia yake,hatujui watoto wake wanavaa kweli? Wanakula? He hali hii iko kwa watu wangapi katika utawala huu? Je naye ni mpiga dili?

Tangu serikali iingie madarakani hakuna program yeyote ya kuondoa umasikini vijijini,matokeo ndio haya,NA utawala huu sasa una miaka miwili NA nusu,bado miaka miwili uondoke

Pia kuna tamko la kuzuia mitumba eti tutakuwa tunapeleka sisi mitumba ulaya,kwa hali hii kweli?

Japo serikali hii anasema ni ya masikini,lakini haitakiwi kuzidisha idadi ya watu
masikini

Taifa likihoji kuhusu umasikini mkali ulioletwa NA awamu hii,jibu ni MLIZOEA DILI

Badala ya kusisimua uchumi,hela zote tumeficha Benki Kuu,zilizobaki,tunawapeleka vijana wa kizungu wenye viwanda vya ndege za bombadia NA dreamliner

IMG_20170731_091103.png
 
Alafu ndio serikali inataka kuzuia mitumba sijui wanataka masikini watembee uchi huyo ni mwenyekiti wa kijiji ana nguo jua atakuwa ni mtu mwenye kiuwezo katika kijiji hicho je hao wengine watakuaje serikali isipambane na ufisadi tu lengo ni kuwe na maisha bora kwa kila mtanzania hizo pembejeo wahakikishe kila mkulima anapata bure ila kuwanyanyua wakulima kila kijiji kiwe na maafisa kilimo na ufugaji kama vilivyo na maafisa watendaji
 
Awamu watu watatembeaa na nguo zzenye virakaaa mkuu

Ova
 
Alafu ndio serikali inataka kuzuia mitumba sijui wanataka masikini watembee uchi huyo ni mwenyekiti wa kijiji ana nguo jua atakuwa ni mtu mwenye kiuwezo katika kijiji hicho je hao wengine watakuaje serikali isipambane na ufisadi tu lengo ni kuwe na maisha bora kwa kila mtanzania hizo pembejeo wahakikishe kila mkulima anapata bure ila kuwanyanyua wakulima kila kijiji kiwe na maafisa kilimo na ufugaji kama vilivyo na maafisa watendaji
Kama mwenyekiti wa kijiji ana hali hiyo,anaowaongoza wana hali gani?
 
Nilidhania kavua lake na yeye Kubaki na vest tu kumbe katoa sandukuni kwenye gari lake... rubbish news Trump husema "Wrong"
 
So kumpa shati lake ni kumuondolea umaskini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumpa shati ni kumsitiri. Huo ni Uungwana!!

Ila kama alivyosema mleta mada hali inazidi kuwa mbaya. Kwa mtazamo wangu awamu hii wanashindwa kuja na policies au strategies zinazoendana na malengo Yao.

Huwezi kufuta mitumba wakati huna viwanda vya nguo na hujaimalisha uzalishaji wa zao la pamba.

Hii mitumba inaweza kuwa anguko lako wasipoangalia!!!
 
Watu wa vijijini wametengwa sana na huduma za kijamii ambazo kwazo wangeliweza kujikwamua kutoka kwenye umasikini.

mafisadi hayana chama
 
Back
Top Bottom