Mgao wa umeme, January Makamba umejipima, unatosha?

Apr 24, 2011
29
542
Matarajio ya watanzania wengi, haswa waliounganishwa katika gridi ya Taifa ilikuwa ni kusahau kabisa adha ya mgao wa umeme, Baada ya kujengwa kwa bomba la gesi kutoka Mtwara Dar es Salaam lililogharimu TZS 2.3 Trilioni. Lakini hadi sasa mgao wa umeme umekuwa mkali sana.

Mwaka 2015, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa kwanza wa umeme unaotokana na bomba la gesi Mtwara - Dar es Salaam (Kinyerezi I) alisema alianza na tatizo la mgao wa umeme mwaka 2010 na analimaliza akimaanisha mradi wa gesi kutoka Mtwara ni komesha ya tatizo la umeme.

Januari 29, 2022 Mkurugenzi mkuu wa TANESCO, Maharage Chande alipotembelea maboresho ya upanuzi wa huduma ya gesi katika mradi wa Kinyerezi I, alisema Mpaka sasa uzalishaji kutoka katika mitambo ya Ubungo III umefika 60MW ambazo tayari zimeunganishwa katika gridi ya Taifa.

Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande akasema kazi ya upanuzi wa Kituo cha Kinyerezi I imewezesha 70MW kupatikana na kwamba kufikia Agosti 2022 kazi hiyo itakuwa imekamilika na kufikia uzalishaji wa 335MW kutoka 150MW. Kwa mantiki hii, watanzania hatutegemei kupitishwa katika makali ya mgao wa umeme, labda tuelezwe, maneno haya ni uongo mtupu.

Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande akasema kazi ya upanuzi wa Kituo cha Kinyerezi I imewezesha 70MW kupatikana na kwamba kufikia Agosti 2022 kazi hiyo itakuwa imekamilika na kufikia uzalishaji wa 335MW kutoka 150MW. Kwa mantiki hii, watanzania hatutegemei kupitishwa katika makali ya mgao wa umeme, labda tuelezwe, maneno haya ni uongo mtupu.

Ingawa TANESCO wanasema siyo mgao, ni matengenezo tu. Novemba 18, 2021 TANESCO ilitangaza kupungua kwa umeme, wakatoa sababu za mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha kupungua kwa maji katika vyanzo vya uzalishaji umeme wa maji hivyo kutakuwa na upungufu wa 345MW

Oktoba 21, 2022 Waziri wa Nishati, January Makamba akihojiwa na Kituo cha habari cha Clouds TV alikaririwa akisema "tunazalisha umeme megawatts 1,700. Umeme unaohitajika kwa kiwango cha juu ni megawatts 1,500. Kwa uhalisia umeme tunaozalisha unatutosha".

Hapa waziri wa Nishati, January Makamba akawa amefuta taarifa ya TANESCO ya November 18, 2021 kwamba kuna upungufu wa 345MW kutokana na maji kupungua katika vyanzo vya uzalishaji umeme. Wateja wa TANESCO tunajiuliza, tuchukue kauli ya TANESCO au kauli ya Waziri wa Nishati kuhusu masuala ya umeme?

Siku 9 baadae, Oktoba 30, 2022: TANESCO wakatoa taarifa kwa umma wakisema kuna upungufu wa 232MW zinazoathiri upatikanaji wa umeme kutokana na ukame unaotokana na kukosekana kwa mvua hivyo mabwawa ya kuzalisha umeme ya Hale, Kihansi, Nyumba ya Mungu na Pangani yenye uwezo wa kuzalisha 266MW za umeme sasa yanazalisha 34MW

Kauli hizi mbili ndani ya siku tisa katika mwezi mmoja kutoka kwa waziri wa nishati na TANESCO zinatosha kukuonyesha watu hawa ni waongo na wameshindwa kabisa kutatua kero ya mgao wa umeme na wanatunga hadithi za kuvutia tu watanzania wakiendelea kuishi bila umeme.

Kimsingi, waziri wa nishati, January Makamba, Wizara hii ni kubwa kwake, apumzishwe kwa lazima. Rais Samia Suluhu Hassan kama kweli anadhani anawapenda watanzania, amuondoe January Makamba katika eneo hilo la nishati, ampe wizara nyingine, kama bado anatamani kumuona katika vikao vya baraza la mawaziri.

Tatizo ni nini kama siyo mgao? HITILAFU? Matengenezo? TANESCO, tafuteni wataalam, au utaalam kutoka nje ya nchi, kuhusu suala la matengenezo, nchi nyingi sasa zilishatoka kwenye zama za kuzima umeme wakati wa matengenezo, huduma zinaendelea kama kawaida wakati wa matengenezo.

Kukatika kwa umeme na mgao kunasababisha kuongezeka kwa gharama za uzalishaji viwandani na kusababisha kupanda kwa bei za bidhaa sokoni kutokana na upatikanaji kuwa hafifu kuliko mahitaji. Hapa The Confederation of Tanzania Industries (CTI) wanatakiwa kusimama kwa kauli na sauti nzito kueleza serikali, jinsi watakavyoathirika.

Kukatika kwa umeme na mgao kunasababisha kuongezeka kwa gharama za uzalishaji viwandani na kusababisha kupanda kwa bei za bidhaa sokoni kutokana na upatikanaji kuwa hafifu kuliko mahitaji. Hapa The Confederation of Tanzania Industries (CTI) wanatakiwa kusimama kwa kauli na sauti nzito kueleza serikali, jinsi watakavyoathirika.

Tanzania, umeme unakatwa bila taarifa, hakuna anaejali, ni wewe mwananchi kujitetea tena ukibembeleza waurudishe. Vinyozi, wachomelea vyuma, mafundi aluminum, wachapaji, banks, etc. hasara ni zao sio vinginevyo, nani wa kuwatetea? Nani wa kuwalipa fidia kwa hasara hizi?

Mfanyabiashara wa kuchonga na kuchomelea vyuma atakosa kipato cha siku bila umeme, hivyo atawajibika kutafuta jenereta kubwa kusukuma Mashine zake afanye kazi za uzalishaji mali. Lita moja ya mafuta atatakiwa kununua shilingi 3,000 hivyo lita 10 ataweka ubaoni Sh30,000.

Muuza duka la vyakula, kwa sababu ya mgao wa umeme katika eneo lake, itabidi apunguze 'order' ya baadhi ya bidhaa zake, hususani bidhaa ambazo zinaharibika haraka, ili kuepuka hasara, kwa sababu hakuna umeme wa kusaidia kuwasha friji ili kuhifadhi. TANESCO wanawajibika kumlipa fidia?

February 2018, Kampuni za umeme, Australia zilitakiwa kulipa fidia kwa wakazi wa jimbo la Victoria, nchini Australia waliothirika kwa kukosa umeme, malipo ya $180 kutegemeana na muda ambao ‘nyumba ilikosa umeme’. Zilitengwa $5M (TZS 11.66 bilioni). Umeme ulikatika kati ya saa 3 hadi 20.

Serikali iruhusu uwekezaji wa kampuni binafsi za kutoa huduma za umeme, TANESCO ni kama wameshindwa hii kazi kabisa. Nchi inakosa umeme tangu asubuhi hadi usiku? Mnajichekesha tu.. Nchi yetu tumekabidhi kwa watu wasiokuwa na sera, mikakati na blueprint za kuendesha nchi.

Tufanye kama Singapore. Sekta ya umeme ipo chini ya Singapore Power. Wanatoa huduma za umeme na gesi, wanasambaza huduma, kwa wateja wake. Ni moja kati ya shirika kubwa Singapore. Sasa hawa SP wako na ‘mashirika tanzu’ ambao wanawasaidia kufanya huduma zao.

Mfano; PowerGas, AusNet Services, SP PowerGrid, SP powerAssets, SP Telecom, SP service, Nje ya hapo kuna SP anbao wanafanya kazi zao kwa ushirikiano na kampuni nyingine, mfano; Power Automation hawa wanahusika kutoa msaada wa huduma za uhandisi katika ulinzi wa Mifumo

Katika vituo poozo vya umeme na usimamizi wa nishati na mfumo wa Taarifa nchi nzima. Pia wapo Singapore District Cooling (SDC). Wanajihusisha na uzalishaji na usambazaji wa maji baridi kwa Majengo ya biashara. Serikali yenu ikajifunze vitu hivi kutoka Singapore na Malaysia.

November 2011, Singapore waliunganisha zaidi ya 80% ya huduma ya gesi katika kampuni za uzalishaji nguvu ambayo iliingizwa na kubadilisha gesi kwenda katika umeme na kujaza katika gridi ya taifa. 20% inayobaki inatoka kwenye mafuta na vyanzo vingine kama taka na nishati mbadala.

Mtasema Singapore ni wakongwe, tutumie mfano wa Malaysia. Nchi ambayo tunalingana nayo umri au kukaribiana kupata uhuru. Kwa mujibu wa 'tume ya nishati' kuna zaidi ya watoa huduma na wazalishaji wakubwa 18, ingawa wasambazaji wa nishati Malaysia wapo chini ya Udhibiti wa Serikali

Idara ya gesi na umeme inahusika na masuala ya kupanga na kuratibu bei na kanuni. Fedha ya mmtej inaendesha shirika la umeme Tanzania na nyingine inatumika kwenye REA na TRA huko. Tena mteja anatoa fedha ya malipo kabla ya matumizi (prepaid). Kwanini mteja adhulumiwe haki yake?

2022 India wanatafuta 175GW. Mwaka 2018 walifunga 5,000MW Solar park, Gujarat. Mradi wa TZS 8.95 trilioni ($3.84bn). Bwawa la Nyerere tulikata miti milioni 2 tukaharibu ecology Selous Game Reserve, tumetumia TZS 8.395 trilioni ($3.6bn) kutafuta 2,115MW

Umeme unakatika siku nzima wakati mteja amelipia huduma kwa ajili ya matumizi yake? Ofisi za serikali na hata Ikulu ni wateja wa TANESCO wa Post-paid, hawana shuruba hizi wanazokutana nazo wateja wa kawaida wa TANESCO wa Pre-paid. Umeme kwao haukatiki kwa sababu ya LUKU.

Miaka 60 baada ya uhuru bado kuna zaidi ya nyumba milioni 37 hazina umeme. 32% ya watanzania ndio pekee yenye kutumia umeme wa TANESCO. Vijijini 17% na mjini 65%. Zingatia, vijijini ndio kuna wakazi wengi kuliko mjini. Rural population 64.05% (taarifa ya benki ya Dunia, 2021)

Bajeti wizara ya Nishati 2022/23, waziri January Makamba anasema vitongoji 37,610 kati ya vitongoji 64,760 Tanzania havijafikiwa na umeme na watahitaji Sh6.50 trilioni na miaka 15 kuvifikia. Fikiria kuna watanzania wataishi bila umeme kwa miaka 15 mingine, Makamba akiwa wizarani!

Mfumo wa manunuzi ya umeme hauna backup? TANESCO wanapokea kodi kutoka kila transaction ya kununua umeme, waboreshe sasa mfumo huo. Hizi hasara za siku 3-4 nani atafidia kwa wananchi? Mtumiaji analipa VAT, EWURA, REA katika fedha anayonunua umeme. Sio hisani. Tunataka huduma bora

Mfano, ukinunua umeme kwa njia ya mitandao ya simu, umeme wa Tsh 1,000/- Cost (gharama) 819.68, VAT (kodi ya ongezeko la thamani) 18%—147.53, EWURA (Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji) 1%—8.20, REA (wakala wa umeme vijijini) 3%—24.59, JUMLA 1,000.00

Kwa miaka zaidi ya 60, tumetoka UTUMWANI kimwili, kiakili bado tupo UTUMWANI kwa wakoloni WEUSI. Wananchi sisi MZIGO. Tunawekwa gizani, tunakosa kununua LUKU lakini tunashindwa kuiwajibisha serikali kwa uzembe wake. Leo watu walipaswa kuwajibishwa.

#MMM, Martin Maranja Masese,
Mtikila,
November 14, 2022
 
Sasa hivi Songea umeme ukiwaka ni kama maajabu hivi maana tumezoea kukaa na giza, kusaga mahindi vijijini kwenye diesel engine, kunyoa kwa rungu max hadi kidevu kimekomaa, kuchaji simu kwenye gari na biashara ya tochi na betri za Tiger zimerudi.

Sasa hivi sundra na aborder ndio washindani wakubwa madukani.
 
Kazi bhana!!

Mtu ukiwa unafanya Kazi ambayo ki ukweli imekizidi elimu yako, ndo itakuharibia zaidi Kwa sababu utakuwa ukiifanya ilimradi liende!

Na mbaya kabisa, aliyemteua naye anakuwa anamtia moyo kwamba anaiweza na kwamba, vipi, unaona na ile mitungi ya asali? Basi pambana hivo hivo!

Basi jamaa anajikongoja tuu, lakini athari za mbele yake ndio kubwa ukilinganisha na sasa;

Siku akitaka kuomba nafasi kubwa zaidi, Kazi zake za hovyo zitakuwa zikimshitaki moyoni mwake! Na kwamba hataeleweka Kwa watu
 
Na wewe ligazeti lirefu unadhani nani anamuda wakusoma hiyo?

Chaji si itaisha kusoma hilo gazeti lako?

Watanzania wanafahamu toka uhuru serikali iliyochoka inayoongozwa na ccm kamwe haiwezi kuiletea neema hii nchi.

Huyo january anatakiwa ang’oke hapo kwa lazima.

Pia na sisi tunaoitwa wananchi ni vilaza wa wakutupwa.

Hatuna tofauti na mifugo.

Dalili ya kwanza yakuwa mfugo ni kumwita mwanasiasa mheshimiwa.

Way forward?

Tufanye kazi zinazoongeza tija kwenye familia na hapo mtaani unapokaa.

Tunza pesa ununue sola lakini pia ikiwezekana tunzeni pesa hapo mtaani mshirikiane mchimbe hata kisima cha maji kwaajili ya dharura.

Ukiwa na kaeneo basi panda hata bustani utapata pesa ya mboga kuliko kujidhalilisha kumlamba mwanasiasa makalio ili upate 5000.

Wananchi puuzie event zozote za kisiasa.

Hao kenge mnawashobokea sana.
 
Nadhani anajua hana sababu ya kujipima kwakuwa kipimo [mteuzi] hakifanyi kazi, kiliharibika.

Makamba ni muongo hilo halina ubishi, lakini kwasababu amekuwa akitoa data zake za ajabu kila wakati zisizoendana na hali halisi field, wajinga wachache wanamuamini.

Kimsingi, hana professionalism yoyote kuendana na mahitaji ya hiyo wizara, amekuwa akitumia uongo tuliouzoea kwenye siasa za CCM ili kuficha incompetence yake.

Bahati nzuri kwake aliyemteua hajielewi, basi jamaa anatamba na kujiona genious, kumbe ni mjinga mshamba, aliyejiegemeza kwenye nguzo ya urafiki wa kifamilia ili kuendelea kuiongoza wizara ya Nishati.
 
Hili jambo kama Rais Angekua Makini Bwana Makamba Angeshakalia kuti kavu. Tanesko wanakata umeme Hawatoi ratiba wanafanya wanavyotaka. Hawajui kuna watu wanategemea Umeme kuendesha maisha yao.

Wao kwa sababu wanalipwa mishahara wanadhani watanzania wote wanalipwa mwisho wa mwezi kama wao.

Haiwezekani kusiwe na ratiba za kila mkoa na watu wakatangaziwa wajue jinsi watakavyo jipanga kufanya kazi.

Leo ndoa zimeingia Migogoro watu wana kesha sehemu zao za kazi ili wafanye kazi usiku maana hawajui umeme utakuwepo Au hautakuwepe kesho.
 
TZS 2.3 Trilioni
Hivi kama Taifa tuna akili kweli. Dola bilioni kwa ajili ya kujengea bomba tu.mitambo ingewekezwa pale pale mtwara ikachakatwa ikasafirishiwa kule kule ama anko alitaka awe nayo karibu ili ajue Perce ngapi ameingiza kule kazi kwenda kukagua.

Ila kweli hii ishu watu wa mtwara walikuwa na Haki ya kugoma na kusema kuwa gesi haitoki mtwara.

Yaani bana huu mfumo wa nchi kwa hizi nchi za kiafrika tulikuwa hatujafika level ya kuishi Kama nchi. Tungeishi Ile kikabila kikabila na kila kabila raisi wao baadaye tungekuja kuungana huko mbele Kama nchi sema Sasa kila kabila likijitegemea na jeshi lake na maamuzi yake like USA.


Sasa hii kwa kyasaka anayelialia kuwa wachaga wajitenge ingekuwa kwao si wangekufa kabisa ama wangelia mpaka Leo hii. Duu kweli kusini kuendelea itakuwa Ni kazi yaani imedhulumiwa mno kwa hili.

Elewa wewe hapo huyo kaingia hapo kupiga hela unakaa unategemea akuwazie wewe afrika bado mno.
 
Boss , can you tell us what has transpired between 2016 and 2022 on developing and maintaining its infrastructure?
 
Na wewe ligazeti lirefu unadhani nani anamuda wakusoma hiyo?

Chaji si itaisha kusoma hilo gazeti lako?

Watanzania wanafahamu toka uhuru serikali iliyochoka inayoongozwa na ccm kamwe haiwezi kuiletea neema hii nchi.

Huyo january anatakiwa ang’oke hapo kwa lazima.

Pia na sisi tunaoitwa wananchi ni vilaza wa wakutupwa.

Hatuna tofauti na mifugo.

Dalili ya kwanza yakuwa mfugo ni kumwita mwanasiasa mheshimiwa.

Way forward?

Tufanye kazi zinazoongeza tija kwenye familia na hapo mtaani unapokaa.

Tunza pesa ununue sola lakini pia ikiwezekana tunzeni pesa hapo mtaani mshirikiane mchimbe hata kisima cha maji kwaajili ya dharura.

Ukiwa na kaeneo basi panda hata bustani utapata pesa ya mboga kuliko kujidhalilisha kumlamba mwanasiasa makalio ili upate 5000.

Wananchi puuzie event zozote za kisiasa.

Hao kenge mnawashobokea sana.
Nyie ndiye aina ya kenge nimewazungumzia kwenye comment yangu hapo juu.

Eti tuvushe katika hili.

Kauli za namna hii ndiyo zinawafanya wanasiasa wakuone fala.

Angalia usije kuvushwa halafu ukavuliwa.

Punguza hasira zako na acha tabia ya kubagaza wenzako...

Una uhuru wa kutoa maoni yako kama wenzako pia..

Acha kudhani kuwa maoni yako ndiyo ya thamani zaidi kuliko ya wenzako...

Heshimu wenzako na maoni yao...!!
 
Aise

Ova
IMG-20221106-WA0036.jpg
 
Nimekwenda ofisini umeme hakuna, jenereta likakorofisha. Nimekimbilia home nifanye kazi kidogo nako toka asubuhi hakuna umeme.

Pamoja na labda sisi wengine tunaonekana ni Pro JPM lakini kwa akili ya kawaida tu, mbona alifanikiwa kuthibiti hili tatizo? How comes serikali ile ile, chama kile kile lakini kifo cha mtu mmoja tu mambo yamekuwa ups and downs
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom