thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Ukweli lazima usemwe, kuna tatizo gani kutambua juhudi za hayati Magufuli kwenye mradi huu wa umeme (JNHP), hasa kwenye hotuba zenu?

Wazo lilikuwa la Mwalimu Nyerere akashindwa, awamu zilizofuata kuanzia ya pili mpaka ya NNE, hawakuwa na habari na mradi huo, waliupa kisogo.

Hayati Magufuli kwa nguvu kubwa na ujasiri usio na shaka akaamua kutekeleza wazo hilo.

Miongoni mwa waliohujumu juhudi za ujenzi wa hili bwawa ni wewe waziri wa sasa wa nishati, January Makamba, kwa kisingizio cha uharibifu wa mazingira, ikapelekea mpaka kuondolewa baraza la mawaziri.

Leo hotuba ya mkurugenzi mkuu Maharage Chande na waziri wake wamejificha kwenye kichaka cha mipasho hasa waziri Makamba.

Nijielekeze kwenye usanii wa waziri Makamba kutambua juhudi za watangulizi kwenye ujenzi wa bwawa hilo, katengeneza zawadi za kutambua michango ya mzee Mwinyi ,na Jakaya, wana mchango gani ikiwa mradi waliupa kisogo?

Makamba junior kawapa medali za kinafiki sana, hata wao wamejisikia aibu sana kupewa medali za ushiriki wao kwa mradi wakati hawajashiriki hata kidogo.,dhambi kubwa sana ikiambatana na unafiki wa hali ya juu.

Huyu kijana ndio anawaza kuwa rais wa hii nchi. Tuna hasara kubwa kama taifa.

Nimpongeze rais Samia kwa kujaribu kuusema ukweli kuhusu kazi kubwa ya hayati Magufuli katika kufanikisha mradi huu.

Kumekuwa na syndicate kupoteza Juhudi za hayati Magufuli kwa kuzimeza kijumla jumla na wasiostahili. Mojawapo ni hilo tukio la kinafiki la kutambua mchango wa hao watangulizi kuhusu bwawa hili, wakati si washiriki.

Namalizia kwa kumwambia waziri Makamba na walio nyuma yake kwamba watanzania hawadanganyiki tena, Magufuli aliwafumbua macho.

Huu mchezo wa kujaza vijana mitandaoni kumdhihaki, mmeona leo jinsi likitajwa jina lake makofi na shangwe kama lote.

Nikiashiria kwamba kimwili hatuko naye ila kifikra tukonae, acheni majungu dhidi ya marehemu.
 
Ndani ya CCM hakuna mwema, wote ni wanyonya damu ya mama Tanzania, kuanzia Warioba,na huyo JPM ndio alikuwa shetani kabisa, sasa unataka mashetani wa sasa hivi wamsifu shetani aliyekufa.

Siku wabongo,wakielewa kwamba ccm ni mfumo wa wizi, wapo pale kijinufsisha wao na vizazi vyao tu,umaskini wetu unatengenezwa makusudi,hawataki kuifungua Dunia yetu,hawataki wabongo wapate mwanga wa kutosha,na kuwa na uchumi huru,wanahofia wabongo wakijitambua,ulaji wao na vizazi vyao,vitapata tabu sana,wajukuu wa Warioba,Mwinyi,Kikwete,wamejaa kila kona,wanakula mema ya nchi.

Hata siku moja utamsikia Warioba akikemea Rushwa ya waziwazi kwenye chaguzi za ccm,"you just can't bote the hand that feeds you"he knows better.Is the thief himself by association.
 
Leo wananchi wamewaonesha JPM ni nani mioyoni mwao, mwanasiasa unayetaka anguko lako kisiasa simama jukwaana umponde JPM mbele ya wananchi, huku mitandaoni wamejaza vijana na mimultiple accounts kila uchao kumdhihaki, 2025 sio mbali.
 
Ndani ya ccm hakuna mwema,wote ni wanyonya damu ya mama Tanzania,kuanzia Warioba,na huyo JPM ndio alikuwa shetani kabisa,sasa unataka mashetani wa sasa hv wamsifu shetani aliyekufa.
Siku wabongo,wakielewa kwamba ccm ni mfumo wa wizi,wapo pale kijinufsisha wao na vizazi vyao tu,umaskini wetu unatengenezwa makusudi,hawataki kuifungua Dunia yetu,hawataki wabongo wapate mwanga wa kutosha,na kuwa na uchumi huru,wanahofia wabongo wakijitambua,ulaji wao na vizazi vyao,vitapata tabu sana,wajukuu wa Warioba,Mwinyi,Kikwete,wamejaa kila kona,wanakula mema ya nchi.
Hata siku moja utamsikia Warioba akikemea Rushwa ya waziwazi kwenye chaguzi za ccm,"you just can't bote the hand that feeds you"he knows better.Is the thief himself by association.
Sawa boss, what are the way forward?,naona unalalamika tu
 
Leo wananchi wamewaonesha JPM ni nani mioyoni mwao, mwanasiasa unayetaka anguko lako kisiasa simama jukwaana umponde JPM mbele ya wananchi, huku mitandaoni wamejaza vijana na mimultiple accounts kila uchao kumdhihaki, 2025 sio mbali.
Hahaha sasa unadhani nyie chama cha mambuzi mtamfanya nini samia? Urais 2025 atashinda mtake msitake kwakua mmekubali kuwa Mbuzi.
 
Back
Top Bottom