Umalaika wa CHADEMA Utaiua

Just some tips on constructive criticism!

If you want to give good constructive criticism, then…

1) focus on valid and unbiased feedback and…

2) make your criticism clear, understandable, and relevant.
Now for some examples!

The poor way of giving constructive criticism:
1. That logo design sucks, who the heck would pay for something like that!?

2. I hate red and green, why not use black and white instead!

3. I can't read the text.

The sexy way of giving constructive criticism:
1. The balloon font used in the logo seems a bit too playful for your business, do you think a serif-font might be more professional?

2. 10% of the male population has red-green colorblindness, you might want to ensure that your color scheme won't turn away potential customers.

3. There isn't much contrast between the background and text color, and the font size is a bit small, so the text is difficult to read.
In closing…

Everyone has a different idea about the way things should be done and sometimes it's not going to be possible for someone to implement a change for all the criticism you've suggested, so don't take it personal if your constructive criticism isn't implemented.


Instead, rest assured that giving good constructive criticism will serve as a future resource and guide to whomever receives your feedback.


Just remember, in all its forms, criticism is an act of finding faults with something. When done badly, criticism can be devastating to a person's self-esteem and self-worth.


Yet when done correctly, criticism can result in positive benefits for all parties involved. As long as your constructive criticism remains valid, clear, and unbiased, you can be confident that your feedback will be gold!

Source: How to give constructive criticism

Je wanachadema mnafanya haya kwa wapinzani wenu i.e CCM na CUF?
 
mmpa ukweli kwanza asahihishe ssm waache ujuma na kufanya chama cha familia, Mkuu na wanae, M-fundo na wanae, halafu tunaweza tafuta siku tuyasikilize mawazo yake, na asahihishe RA, EL kuacha kukifanya chama kama sehemu ya ulithi wao wakati cha wote
 
kama kuendesha chama kifamilia ni kosa!!! basi CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTO(CHADEMA) wanapitia njia ileile ya CCM,HUJAONA MAJINA YA WABUNGE WA VITI MAALUM???? kalagabaho,, msiojua endeleeni kushika pembe, wenye chama wanakunywa maziwa,, wajinga endeleeni kuumwa na nyuki lakini wenye chama wanangoja asali mezani. LOL
Kukosoa kunahitaji utafiti na kuwa makini pamoja na ufahamu wa kutosha kwa jambo husika, si kukurupuka kukosoa jambo ambalo hamnalo na kueleza upuuzi wako kuwa ndiyo ukosoaji.
Katika kuchagua wabunge wa viti maalum CHADEMA wamefanya jambo a kuigwa na vyama vingine kwa kutoa value ya uwezo wa makada wake ki-elimu, uongozi na ufahamu wa malengo na mahitaji ya nchi. Pia CHADEMA imetoa value ya jinsi kada huyo alivyoshiriki kujenga chama katika eneo lake na kwa wanachi wote, kama vile kushiriki kampeni za uchaguzi na za operation Sangara n.k.
Wabunge wote wa viti maalum walipangwa hivyo bila kujali mahusiano yake na viongozi wa chama. Tukumbuke kuwa CHADEMA kimefikia hapo kilipo kwa baadhi ya wanachama kujitolea sana kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na wengine kukatwa mishahara yao kuchangia chama na uwezo wanao, sasa leo uwaache tu kwa sababu wana mahusiano na baadhi ya viongozi!
Tutafute mambo yenye msingi ya kukosoa na tukosoe baada ya kutafakari kwa undani, ingawa ni kweli kuna mambo ambayo yanaweza kufanyika isivyokupendeza wewe ila kama inakidhi taratibu na kuleta mafanikio tuyaunge mkono.
 
Mnawasema kina makamba, mbona kinamtei mmewanyamazia, siasa tanzania ni kama soka tu wote wezi hamna mzima humo, wote wanatetea kamkate kao tu, ufisadi upo hadi ktk vyama na ndiomaana anayetaka kubadili chama ktk njia sahihi anfungishwa virago au anazibwa mdomo kama CHACHA WANGWE
 
Mtoa mada sijakupata give us facts, ili tujue unazungumzia lipi hasa la hawa chadema kujisahihisha. Umekuwa too general.
Hebu nikupe jambo moja la karibuni kabisa. Wakati Kampeni zinaanza watu wengi walishauri sana kwa CHADEMA kuwa na hakika ya kuwa na mawakala kwenye vituo vyote nchi nzima. Vituo vya kupigia kura vilikuwa 53,000. waulize CHADEMA walikuwa na mawakala kwenye vituo vingapi nchi nzima?

Lakini hata stahili yao ya kupiga Kampeni ilikuwa shaghala baghala. Slaa anatua kuhutubia akiondoka viongozi wake wa chama hawana uwezo wa kutoka hata kilomita mmoja kutokana na kutokuwa na hela. Hili nalo tuliwaeleza mapema kabisa kamba ni lazima ruzuku ya chama iwekwe akiba kwa uchaguzi lakini uchaguzi wa mwaka huu ni kama vile CHADEMA walistukizwa.
 
una hakika gani kuwa huyo aliyetoa kauli hiyo ni chadema, lakini si ni ukwewli kwamba ya huko shy, au una lako jambo?
Hebu jaribu kujua kwanza maudhui yaliyomo kwenye hoja ya mtoa hoja kabla ya kurukia jambo. Hoja yangu ni kwamba kukosolewa ni sehemu inayotakiwa sana kwa binadamu yeyote yule mwenye akili timamu. Anayekataa kukosolewa kama ni kiongozi basi ataishia kwenye tabia ya kuwa dikteta.
 
Kitu kikubwa nataka kukiona from Chadema ni jinsi gani wataweza kuwa na hoja za msingi bungeni. Nataka kujua wanaplan gani, au Muswaada gani watakaouleta bungeni wa kuwapatia kazi WTZ.
Pili, wanampango gani bungeni kuhusu kuwasadia Wanafunzi kuweza kupata Mikopo ya shule, au Grants.
Tatu, nataka kujua kama watapeleka bengeni muswaada gani kuhusu viwango vya kodi, ushuru. Maana yake TZ ina viwango vikubwa sana vya kodi.
Nk.
Kwa sasa nchi ina mahitaji machache sana lakini muhimu
1. Utawala bora
2. Usimamizi mzuri wa pesa za serikali
3. Udhibiti wa rushwa na ufisadi
4. Mgawanyo mbaya wa raslimali kama mikataba ya madini

Serikali ya CCM ikikubali hayo nchi kuingia kwenye neema ni suala la haraka sana. Chadema wanaenda kuanzia na hayo mengine yatakayofuata ni finishing ndogondogo tu. Na ukumbuke hayo niliyoyataja ndo yameinyima CCM kura lakini kwa aibu wakaiba kura ili matokeo yasiwe tofauti sana na REdet na synovate
 
Kama mtoto anayedekezwa alivyo ndivyo taasisi yoyote ile isiyokosolewa au kukubali kukosolewa ndivyo inavyoharibika. Taasisi zote duniani zinaongozwa na wanadamu na si malaika.

Kwa kipindi kirefu sana humu ndani ya JF au CHADEMA kwenyewe inaonekana kukosoa mambo mabaya yanayofanywa na chama hicho kama ni kupinga mabadiliko. Mtu akimkosoa Mbowe anaitwa kibaraka wa mafisadi.

Watu wakihoji busara ya kutajataja watu kwa kuwatuhumu (bila sababu za msingi, siyo mafisadi) anaitwa mbumbumbu au fisadi. CHADEMA lazima ikubali kwamba hata wao kama binadamu wanaoongoza taasisi kubwa na inayokubalika kwa jamii na katika kuongoza kwao wakati mwingine huwa wanakosea.

Mwalimu Nyerere wengi tunamkubali kama alikuwa ni Genius lakini hata yeye aliwahi kuandika kitabu kinaitwa "tujisahihishe" lengo likiwa ni kuwazindua viongozi kwamba hata wao wanakosea. CHADEMA ijisahihishe.

Pamoja na kwamba uliyoandika ni sahihi lakini FAFANUA ZAIDI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom