Umalaika wa CHADEMA Utaiua

Wallah wewe u mbali ningekupiga na Castle Lite bee, hayo anayoona ni mawazo mazuri ayawasilishe kwenye Chama Dume fake aone atakavyotolewa baruti na Riz 1 achilia mbali Makamba.Hapo ndo utajua hakuna kitu wala udume wowote isipokuwa ni JAMARI Group of Company.Note JAMARI (Jakaya, January, Makamba,Riz 1)
CCM imefikia hapo ilipo kwa kuwa na kulea tabia ya kudhani chenyewe hakiwezi kukosolewa. kuna wengine wanadai kuwa "constructive Criticism" ndiyo inayotakiwa na siyo "Destructive Criticism"

Lakini ni nani anapima kama ukosoaji huu ni wa kujenga au kubomoa? Wengine hatutaki kuwa " kondoo" kwenye kila kitu kinachofanywa na vyama tunavyovipenda. Kama CHADEMA inafikiri kwamba kukosolewa huja kwa hiyari ya anayekosolewa itakuwa imekosea sana.

Dhana ya ukosoaji imejijenga kwenye msingi wa kuonyesha upande wa pili wa mawazo kwa jambo husika. Wengi wetu tunakerwa sana kwa tabia ya CCM kukataa kukosolewa na tutazuia kwa nguvu zetu zote jambo hilo lisijijenge ndani ya CHADEMA.Kwani wao CHADEMA ni malaika toka mbingu gani hadi wasikosolewe?

we have to think positively!!
 
Wewe kiherehere wa mambo ya chadema ndio tatizo!
Tulikataa kuwa na mawazo ya kusema "Zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa CCM" na hatutakubali kuwa mashabiki wa "Zidumu fikra sahihi za CHADEMA"

Dhahabu safi husafishwa kwa moto mkali na si vinginevyo.
 
Si bure umetumwa na karamagi na mshenga wake mkubwa lowasa..... Aliyekutuma mwambie atufi ng'o; uliona wapi malaika kafa...!!!?
 
Si bure umetumwa na karamagi na mshenga wake mkubwa lowasa..... Aliyekutuma mwambie atufi ng'o; uliona wapi malaika kafa...!!!?
Ukizoea kutumwa kila mara utadhani na wenzio wametumwa.
 
Kama mtoto anayedekezwa alivyo ndivyo taasisi yoyote ile isiyokosolewa au kukubali kukosolewa ndivyo inavyoharibika. Taasisi zote duniani zinaongozwa na wanadamu na si malaika.

Kwa kipindi kirefu sana humu ndani ya JF au CHADEMA kwenyewe inaonekana kukosoa mambo mabaya yanayofanywa na chama hicho kama ni kupinga mabadiliko. Mtu akimkosoa Mbowe anaitwa kibaraka wa mafisadi.

Watu wakihoji busara ya kutajataja watu kwa kuwatuhumu (bila sababu za msingi, siyo mafisadi) anaitwa mbumbumbu au fisadi. CHADEMA lazima ikubali kwamba hata wao kama binadamu wanaoongoza taasisi kubwa na inayokubalika kwa jamii na katika kuongoza kwao wakati mwingine huwa wanakosea.

Mwalimu Nyerere wengi tunamkubali kama alikuwa ni Genius lakini hata yeye aliwahi kuandika kitabu kinaitwa "tujisahihishe" lengo likiwa ni kuwazindua viongozi kwamba hata wao wanakosea. CHADEMA ijisahihishe.

You have nailed it!!! tutasema kwenye jukwaa mbao asilimia 90 ni wanachadema, tutawatoa tongotongo, tutawakosoa, tutawaonya , tutawapa tactics za ushindi! ili kuijenga Tanzania na kujenga wapinzani in general.

wakikataa tutasema tu, wakikataa ukweli ulio dhahiri we will then start to question their intentions for this country

congrats!!!!
 
Ukizoea kutumwa kila mara utadhani na wenzio wametumwa.

aaaaaargh....wewe ndo walewale tu. Lakini usijali; mawazo yako tupa kule na mwendo ni ule ule, haturudi nyuma kamwe!! tuache na UMALAIKA wetu. Ila ndo kama ulivyoona this October; huo ni mwanzo tu na bado.
 
You have nailed it!!! tutasema kwenye jukwaa mbao asilimia 90 ni wanachadema, tutawatoa tongotongo, tutawakosoa, tutawaonya , tutawapa tactics za ushindi! ili kuijenga Tanzania na kujenga wapinzani in general.

wakikataa tutasema tu, wakikataa ukweli ulio dhahiri we will then start to question their intentions for this country

congrats!!!!
Nashukuru Waberoya umenielewa. Kuna watu wanadhani wao ndiyo CHADEMA "yenyewe" na wamebeba vichwani mwao mawazo yote yatakayoleta mabadiliko yanayotakiwa kwenye nchi hii. Lazima tukubali kwamba CHADEMA inaongozwa na wanadamu na wanadamu kukosea ndiyo sehemu ya uanadamu wenyewe. Lazima wakubali kukosolewa.

Enzi zile za Vita baridi, ukitaka kummaliza mwanasiasa wa marekani Mwite "Mjamaa" na ukitaka kummaliza mwanasiasa wa Kirusi mwite "bepari". Kuna watu hoja za kuikosoa CHADEMA kwa wema zikija humu ndani wanawapachika wenzao "umesenja" kwa Kina Karamagi na Lowassa. Kumbe wengine tukisia majina hayo yanatajwa tunasikia kufakufa.
 
aaaaaargh....wewe ndo walewale tu... Haturudi nyuma kamwe!!
Utapata shida sana kwenye hii dunia kama unaishi kwa kuhisihisi. Na nani kakwambia urudi nyuma. Au wewe mwenyewe umezoea kurudi nyuma??
 
lakini mbona ya ccm hayaachwi! Yameng'ang'aniwa tu!
yanayosemwa ya serikali wala si ya ccm ufisadi na wizi mnaiba mali ya uma na si za chama, mbona ufisadi mnaofanya ndani ya chama hatuingilii!
 
yanayosemwa ya serikali wala si ya ccm ufisadi na wizi mnaiba mali ya uma na si za chama, mbona ufisadi mnaofanya ndani ya chama hatuingilii!
Hapo ndipo patamu. Ufisadi unaofnayka kwenye serikali yetu ulianzia kwenye ufisadi wa CCM. Walipochukua SUKITA tukanyamaza,wakachukua viwanja wa Michezo tukawaangalia. Mwisho wakajenga imani wao wana haki ya kuchukua hata vya umma.
 
Mtoa mada sijakupata give us facts, ili tujue unazungumzia lipi hasa la hawa chadema kujisahihisha. Umekuwa too general.
 
ndugu yangu chadema kama chama cha upinzani kimeelekeza nguvu zake kwenye kupambana na uzembe, utendaji mbovu na ufisadi uliotamalaki serikalini (unaweza sema serikali ya ccm). Tatizo la wengi wa wakosoajii wa chadema huelekea kutetea mapungufu hayo serikalini pamoja na watuhumiwa wake. Kama unakosa raha watuhumiwa wakitajwa kwa majina basi jiulize kwa nini hawajaenda mahakamani kudai "haki" yao? Wewe kweli unaamini kwamba viongozi wa chadema ni wajinga kiasi cha kutaja mafisadi bila sababu za msingi? Hapa tulipofikishwa na serikali isiyotaka kusimamia maadili kwenye utumishi wa umma basi "naming and shaming" ni hatua muafaka tu kwa upinzani. And it works! Wananchi wanazidi kuuona ukweli. I tell you ccm and its govt have to wake up and smell ze coffee. Nchi inabadilika!
niliwahi kumsikia mwalimu nyerere akisema kuwa iwapo mtu mzima atafanya jambo la kuvunnja maadili na mkashindwa kumchukulia hatua, mpigieni hata kelele tuu. Big up!!!!!
 
Kigarama, Tatizo kubwa kwenye kukosoana kibongo bongo ni pale ambapo the first sentence or else the word tayari mtu anaenda personal. Kwa mtindo huu si rahisi mtu au oganaizesheni ikakosolewa ikakosoleka.

Mtu anaikosoa CCM anaanza kuingiza maswala binafsi ya Makamba, do you think CCM na Makamba mwenyewe watakuwa tayari kusikiliza?

Ishu nyingine ni respect, mtu anaanza say kuikosoa CHADEMA,neno la kwanza Dr. Slaa mwizi wa wake za watu......... ni constructive criticism kweli hiyo?
 
Just some tips on constructive criticism!

If you want to give good constructive criticism, then…

1) focus on valid and unbiased feedback and…

2) make your criticism clear, understandable, and relevant.
Now for some examples!

The poor way of giving constructive criticism:
1. That logo design sucks, who the heck would pay for something like that!?

2. I hate red and green, why not use black and white instead!

3. I can't read the text.

The sexy way of giving constructive criticism:
1. The balloon font used in the logo seems a bit too playful for your business, do you think a serif-font might be more professional?

2. 10% of the male population has red-green colorblindness, you might want to ensure that your color scheme won't turn away potential customers.

3. There isn't much contrast between the background and text color, and the font size is a bit small, so the text is difficult to read.
In closing…

Everyone has a different idea about the way things should be done and sometimes it's not going to be possible for someone to implement a change for all the criticism you've suggested, so don't take it personal if your constructive criticism isn't implemented.


Instead, rest assured that giving good constructive criticism will serve as a future resource and guide to whomever receives your feedback.


Just remember, in all its forms, criticism is an act of finding faults with something. When done badly, criticism can be devastating to a person's self-esteem and self-worth.


Yet when done correctly, criticism can result in positive benefits for all parties involved. As long as your constructive criticism remains valid, clear, and unbiased, you can be confident that your feedback will be gold!

Source: http://theclosetentrepreneur.com/giving-criticism-the-good-the-bad-and-the-ugly
 
Kitu kikubwa nataka kukiona from Chadema ni jinsi gani wataweza kuwa na hoja za msingi bungeni. Nataka kujua wanaplan gani, au Muswaada gani watakaouleta bungeni wa kuwapatia kazi WTZ.
Pili, wanampango gani bungeni kuhusu kuwasadia Wanafunzi kuweza kupata Mikopo ya shule, au Grants.
Tatu, nataka kujua kama watapeleka bengeni muswaada gani kuhusu viwango vya kodi, ushuru. Maana yake TZ ina viwango vikubwa sana vya kodi.
Nk.
HAPA KUNA HAJA YA ELIMU YA URAIA KIDOGO
Muswaada gani watakaouleta bungeni wa kuwapatia kazi WTZ.
KATIKA UCHAGUZI WANANCHI HUKIPTIA RIDHAA CHAMA FULANI KUUNDA SERIKALI ILI KUTEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI AMBAYO WALIKUWA WAKIUUZA WAKATI WA KAMPENI. KAMA TULIVYOTANGAZIWA NA TUME YA UCHAGUZI YA TANZANANIA KUWA KWA MUJIBU WA KATIBA YETU MWAKA 2010 CCM YENYE MGOMBEA AITWAYE DR JAKAYA KIKWET NDIYE ALIYESHINDA NA HIVYO KUPATA RIDHAA YA WATANZANIA KUUNDA SERIKALI. HIVYO KISHERIA ILANI YA CCM NDIO INAYOTEKELEZWA NA SERIKALI NA BUNGE.

KAMA KAMBI YA UPINZANI CHADEMA HAIWEZI KUPELEKA MUSWADA WOWOTE BUNGENI, KWANI MISWADA HUPELEKWA NA SERIKALI TUU. WAPINZANI WANAWEZA KUPELEKA HOJA BINAFSI AMBAZO PIA HUPIMWA NA KWA IDADI YA WABUNGE WANAOUNGA MKONO AU KUKATAA.

CHADEAMKWA NAFASI YAKE KAMA KAMABI YA UPINZANIA HAINA MAMALAKA YA KUPELEKA ILANI NA MIPANGO YAKE BUNGENI, KAZI YA UPINZANI NI KUSUBIRI SERIKALI ILETE MISWADA YAKE YA SHERIA ILI IADILI KWA NIA YA KUTETEA MASLAHI YA WANANCHI NA KUIPITIA BAJETI KUONDOA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA SERIKALI. CHADEMA ITAKUWA NA UWEZO TU WA KUPENDEKEZA MAREKEBISHO AMBAYO NI LAZIMA YAKUBALIWE NA
BUNGE LOTE AMBALO IDADI KUBWA NI WABUNGE WA CCM AMBAO KWA UTAMADUNI WAO HUJALI ZAIDI MASLAHI NA HESHIMA YA CHAMA KULIKO MASLAHI YA TAIFA NA WANANCHI.

KUTOKANA NA KUISIMAMIA SERIKALI YA CCM VILIVYO CHADEMA WANAWEZA KUONGEZA NAFASI ZA AJIRA CHACHE KUTOKANA NA KUSIMAMIA MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI IPASAVYO KWA NJIA MBALI MBALI IKIWEMO YA KUTUMIA KAMATI ZA BUNGE, KUULIZA MASALI, NA KUCHANGIA KATIKA BAJETI KWA NIA YA KUPUNGUZA MATUMIZI YA SERIKALI ILI FEDHA ZITAKAZOOKOLEWA ZIELEKEZWE KWENYE SEKTA ZINZOWEZA KUTENGENEZA AJIRA. LAKINI CHAMA CHA KUPIMWA KATIKA KUWAPATIA AJIRA WATZ NI CCM YENYE RIDHAA YA KUONGOZA SERIKALI.
Pili, wanampango gani bungeni kuhusu kuwasadia Wanafunzi kuweza kupata Mikopo ya shule, au Grants. KAMA ILIVYOKUWA HAPO JUU ILANI YA CHADEMA HAIKUWEZA KUPATA BARAKA ZA WATANZANIA, KAMA NI KWELI AU KWA HILA SIJUI, HIVYO CHADEMA PIA ITALAZIMIKA KUSUBIRI CCM WALETE MIPANGO YAO KUHUSU WANAFUNZI WA VYUO WAFANYE KAZI YA KUIBANA SERIKALI YA CCM KUHAKIKISHA WANAFUNZI WANASAIDIWA KUPATA MIKOPO, GRANTAS N.K. KAMA NILIVYOELEZA HAPO JUU CHADEMA HAIWEZI KUPELEKA MIPANGO YAKE KUHUS WANAFUNZI BUNGENI KUTOKANA NA KUWA NA IDADI NDOGO YA WABUNGE KUUNDA SERIKALI NA KUKOSA NAFASI YA URAIS.

Tatu, nataka kujua kama watapeleka bengeni muswaada gani kuhusu viwango vya kodi, ushuru. Maana yake TZ ina viwango vikubwa sana vya kodi KWA KAWAIDA KAMBI YA UPINZANI HAIWASILISHI MUSWADA BUNGENI. BADALA YAKE KILA MWAKA BAADA YA SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI, HAPA NI CCM KUTAYARISHA BAJETI YAKE KWA KUWASILISHWA BUNGENI; KAMBI YA UPINZANI PIA HUTAYARISHA BAJETI KIVULI. NI HAPA CHADEMA AMBAPO WATAKUWA WAMEWEKA MAMBO YOTE DR SLAA ALIYOKUWA AKIWAAHAIDI WANANCHI KATIKA KAMPENI NA KUPENDEKEZA VYANZO VIPYA VYA MAPATO-jitahidi uwe unasoma bajeti kivuli huwa zinachapwa magazetini pia.

KAMA ILIVYOKUWA MIAKA YA NYUMA KAMBI YA UPINZANI HUSOMA BAJETI KIVULI NA KISHA WABUNGE WA CCM AMBAO NI WENGI HUiIWEKA PEMBENI NA KUPITISHA BAJETI YA SERIKALI YAO PASIPO MAREKEBISHO YOYOTE.


KIFUPI WATAZNANIA TUTAWEZA KUPUNGUZA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA SERIKALI KAMA ILIVYOKUWA MIAKA YA NYUMA KWA KUWA NA WABUNGE 45 WA CHADEMA NA KUUNDA KAMBI YA UPINZANI. ILI KUFIKIA UKOMBOZI WA KWELI KAZI ILIYOKO MBELE YETU NI VIJANA KUJITAYARISHA KWA UCHAGUZI WA 2015 ILI KISIWEPO CCM ISIPATE WABUNGE WA KUTOSHA KUUNDA SERIKALI LABDA ISHIRIKIANE NA CHAMA KINGINE. HUO NDIO UTAKUWA MWANZO WA UKOMBZI KAMILI. IN THE MEAN TIME ILI KUZUIA UCHAKACHUJAI WA 2015 NI LAZIMA KILA MTANZANIA AENDELEE KUDIA MAREKEBISHO YA KATIBA NA TUME HURU YA UCHAGUZI.

Iam SURE YOUR COMMENT WILL BE USEFUL TO MANY OTHERS RATHER THAN WASTING TIME POSTING ALOT OF NONSENSE.
 
Well said, kama ana mawazo mazuri awapelekee kina Makamba waache kuiendesha CCM kifamilia.

kama kuendesha chama kifamilia ni kosa!!! basi CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTO(CHADEMA) wanapitia njia ileile ya CCM,HUJAONA MAJINA YA WABUNGE WA VITI MAALUM???? kalagabaho,, msiojua endeleeni kushika pembe, wenye chama wanakunywa maziwa,, wajinga endeleeni kuumwa na nyuki lakini wenye chama wanangoja asali mezani. LOL
 
Hili ndilo tatizo nililokuwa nalizungumzia!!

hahahaha,mkuu uko right!
kwa kweli tusipo taka kuchukua challenge tutaisha ila wengi humu sio viongozi ndani ya chadema ingawa najua wamo na kama wanasoma kwa makini hizi comments basi wanazifanyia kazi.

Jukumu letu kubwa ni kutoa challenge kwao wasipo fuata ni shauri zao
 
you have nailed it!!! Tutasema kwenye jukwaa mbao asilimia 90 ni wanachadema, tutawatoa tongotongo, tutawakosoa, tutawaonya , tutawapa tactics za ushindi! Ili kuijenga tanzania na kujenga wapinzani in general.

Wakikataa tutasema tu, wakikataa ukweli ulio dhahiri we will then start to question their intentions for this country

congrats!!!!
tunawasubiri waberoya na kigarama mlete hizo hoja zenu za kukosoa lakini naona mnashabikiana wenyewe kwa wenyewe tuu, vipi hamna kazi zingine!!!! Tunawasubiri
 
Kazi yenu Makada wa ccm kwa sasa imeisha, maana mshastukiwa na kilichobaki ni kudhalilika mbele ya wananchi...Kawshauri ccm wasimchague chenge, chadema hakuna tatizo!
 
Back
Top Bottom