FURSA YA ZAO LA MDALASINI

Karibu
Nehemia One Pvt Co Ltd. wataalamu wenye uzoefu wa masoko na uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Tunapenda kukukaribisha kwenye fursa ya uzalishaji wa "MDALASINI "

tunazalisha miche ya mdalasini na kuhamasisha watu kupanda zao hili kwasababu tunafahamu soko lake jinsi lilivo kubwa na linazidi kukua Kwa kasi. Ni zao lenye matumizi mengi hasa kama kiungo kwenye Aina mbalimbali za vyakula. Jambo jema ni kuwa soko lake ni kubwa mnoo katika nchi zote duniani lakini uzalishaji wake ni mdogo mno!

MASOKO NA UHITAJI

Kwa mujibu wa taaasisi ya utafiti ya persistance market research, thamani ya soko la MDALASINI duniani itafikia Dola za kimarekani bilioni 1.15 mwaka 2030. Matumizi kwenye viwanda vya dawa na vipodozi, viwanda vya chakula ndio ambayo yanafanya uhitaji wake kua mkubwa. Yako makampuni mengi kama Csi na mengine mengi ambayo yanahitaji mdalasini kutoka Tanzania Kwa bei kubwa kwenda nchi za falme za kiarabu, ulaya, na America lakini upatikanaji wake ni wa chini.

Uhitaji kwenye soko la kimataifa unaongezeka Kwa kasi kwasababu ya matumizi yake kama kiungo cha chakula, dawa chenye antioxidants, ant inflammatory properties, also helping in heart and stroke, blood sugar, diabetes etc.

Kampuni yetu yenye muunganiko na makampuni zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani huwa inapokea oda nyingi za magome ya mdalasini zaidi ya tani 20 Hadi 500 mara Kwa mara lakini tunakosa mdalasini wa kutosha kutimiza oda hizo.

SOKO LAKE KWA TANZANIA

Mdalasini unaozalishwa Tanzania haukidhi kabisa mahitaji ambapo ni kiasi cha asilimia 20 Hadi 28 ya uhitaji hivyo kufanya asilimia kubwa ya mdalasini kuagizwa kutoka nchi za bara la Asia kama India, Vietnam, Malaysia na China.
Baadhi ya wawekezaji kwenye viwanda vya chakula wameonesha nia ya kujenga viwanda Vya kuchakata zao hili lakini ukosefu wa MDALASINI wa kutosha imekua kikwazo.

Licha ya viwanda. Kuna makampuni zaidi ya 100 ambayo yanahitaji zao hili ili kusafirisha kwenda nchi za ulaya, America lakini wanakosa kwasababu ya uzalishaji ni mdogo mnoo!.

Aina ya miche ya mdalasini inayooteshwa na kampuni ni (Cinnamomum verum) picha ziko mwishoni baada ya maelezo.

UZALISHAJI NA MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO HIKI

✓Mdalasini ni jamii ya mti ambao hukua Kwa urefu wa kuanzia Mita 8 Hadi 15 kutegemeana na eneo mmea ulipooteshwa.
✓Hupendelea eneo la wazi kwenye kiasi cha wastani cha jua.
✓huoteshwa kwenye udongo wenye rutuba ya asili na maji ya wastani. Eneo lenye maji mengi au lenye asili ya kutuamisha maji halifai Kwa uzalishaji wa MDALASINI.
✓zao hili halihitaji mbolea wala dawa katika ukanda wa kitropiki kama Tanzania
✓udongo wa tifutifu, kichanga -tifutifu wenye wastani wa unyevu nyevu unafaa saana,
Na maeneo yenye wastani wa mvua wa mm 2000 mpaka mm 2600 Kwa mwaka. Hustawi kwenye mwinuko kuanzia Mita 10 Hadi 1500 kutoka usawa wa bahari na joto kiasi cha wastani wa digrii 27 za sentigredi
✓mmea hustawi au unaweza kustawi kwenye mikoa ya Morogoro, tanga, pwani, mtwara, Lindi, rukwa, tabora, rukwa, tabora, Kagera, mara, (maeneo yanayo zunguka ziwa Viktoria) mbeya, katavi, kigoma na Zanzibar.
✓ ekari moja hupandwa miche 380 mpaka 400

MAVUNO

1. Mdalasini huanza kuvunwa kuanzia umri wa miaka miwili. Jambo zuri ni kuwa, baada ya kuvuna, mmea unachipua tena na huvunwa Kwa mwendelezo Kwa kila baada ya miaka miwili Hadi mitatu mpaka baada ya miaka 30 Hadi 45
2. Majani, na mbegu hutumika kuzalisha mafuta ambayo Yana thamani kubwa. Magome hutumika kutengeneza viungo vya chakula, dawa na hata vipodozi.
3.jinsi mmea unavo kaa shambani miaka mingi ndivo ambavyo thamani yake inapanda kutokana na uwingi wa magome yatakayo patikana, kuongezeka Kwa ladha na harufu nzuri ya magome.
4. Kama ikiwekezwa Kwa miaka kuanzia 8 hutoa mapato makubwa Sana kama ifuatavyo .
Mti mmoja hutoa kilo 40 za magome yaliyo komaa , majani kiasi cha kilo 200 ambayo pia unaweza kuvuna kila mwaka baada ya mwaka wa tatu tangu kupanda, pamoja na mbegu zake.

Kwa idadi ya miti 380 Kwa ekari, kiasi cha magome ni kilo 15200 (tani 15.2).
5. Bei Kwa kilo moja ya magome ya mdalasini ni shilingi za kitanzania 8500/kg (bei ya wanunuzi wa ndani) bei huwa ni 9500/kg Kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi ambao ni wengi na wa uhakika.
6. Makadirio ya mapato ghafi Kwa ekari ni shilingi milioni miamoja na ishirini na tisa (129,000,000 Tshs).

Gharama za miche ni shs 2600 Kwa kila mche ambayo huuzwa Kwa oda.

Tunatoa huduma bure (Kwa wateja wa miche) Kwa msaada wa namna ya kuotesha shambani, kuhudumia, kuvuna na MASOKO ambayo yanasuburi Kwa hamu kubwa.

Wasiliana nasi kupata miche Kwa namba
+255762967548
+255699589177

Email. nehemiahedward7@gmail.com
Morogoro mjini.
 
Pole mdogo wangu karibu JF
tafadhali nitake radhi, mtoto wangu alimaliza chuo kitambo na nilimfundisha kwenda kujisomea library.. hii ilinipunguzia maswali mengi ya kitoto, sasa nyinyi ambao mnataka materials kwa kumeza bila kutafuna unajaribu niita mdogo wako? asee madogo wa siku hizi inabidi tuwa send off somewhere till you expire.
 
Wewe jamaa jam sana:D:D:D
 
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KILIMO CHA MIEMBE (Tanzania)

Pole na hongera kwa Majukumu, nimeona niandike mwendelezo huu maana shida ya kutovuna kabisa matunda imekithiri au kupata matunda machache sana. Kuna mambo kadhaa ambayo tunaweza kujifunza kwa pamoja ili kutafuta matokeo bora huko mbele.

i. Muda na Mazingira yanayosababisha Maua na Matunda.
a/ Maua yanahitaji msimu kame (Kipindi kikavu) mara nyingi ni miezi 2 hadi mitatu baada ya kuisha mvua za mwaka, mara nyingi maua hutokea kuanzia June hadi Oktoba, kutegemea na mwisho wa mvua na msimu wa baridi kwa mwaka husika.

b/ Matunda huhitaji joto ili yatungwe na yakomae walau 20°c hadi 27°c, hili joto mara nyingi ni kuanzia mwezi Oktoba hadi february. Joto likizidi kufikia wastani wa 38°c hupelekea matunda kuungua, ladha kupungua na kasi ya ukuaji kwa mmea kupungua.

NINI HASA HUPELEKEA KUWA NA UTOFAUTI WA MISIMU KWA AINA ZA EMBE?
Katika makundi ya embe tuna aina tatu kwa majira ya uzalishaji embe,yaani yale ya:
-Mzao wa kwanza wa maua (1st flush)
-Mzao wa kati (Medium flush)
-Mzao wa Mwisho (Late flush)

Hapo juu ndio hutoa aina zinazotofautiana majira ya mwaka na ndio hupelekea aina fulani kuonekana mtaani na nyingine kutokea muda mwingine.
Sababu kuu ni muda na mazingira kama navyoendelea

Mazingira yana athari katika kukua kwa mti wa mwembe, mashambulizi ya magonjwa na wadudu, ladha ya embe na muda wa kukomaa kwa embe. Hapa kitu kikuu ni mwinuko kutoka usawa wa bahari, haka kaeneo kanachangia mtofautiano katika msimu wa uzalishaji sana sana. Wale wa mwinuko wa chini kutoka usawa wa bahari wana nafasi ya kuanza kupata maua na matunda kuanzia mwezi Oktoba mpaka January wakati wale wa maeneo ya mwinukoni zaidi hupata matunda kuanzia Disemba hadi Machi, kwa aina za embe zetu. Udongo nao unachangia yaani tabia ya kutoka eneo moja kwenda lingine kutokana na asilia ya udongo huupelekea kuleta tofauti katika uzalishaji wa maua na matunda kwa ujumla.

*KUMBUKA.

Mwinuko kadri unavyozidi kutoka usawa wa bahari, kuna aina zinasumbua kuanzia kukua hadi kuzaa lakini hata swala la ladha pia linazingatiwa sana na sio embe zote zinastawi, embe ambazo zinakubali hadi maeneo yanayozidi mita 1900 ni Sabre, Peach, Dodo na Ngowe. Ushauri ni vizuri kwa kuzingatia mwinuko wa usawa wa bahari wa eneo ulilopo.

ii. Hali ya hewa na tabia Mazingira ya eneo husika.
Kadri mwinuko unavyoongezeka au kupungua kuna tabia zinazidi kubadilika kutoka sehemu moja kwenda kwingine.

Suala la mvua au Unyevu hutofautiana kutoka eneo moja kutegemeana na mwinuko au asili ya mvua ya eneo husika. Mvua kwa kipindi kirefu katika mvua za mwaka hupelekea kuchelewa kufunga kwa maua, mvua nyingi au unyevu katika kipindi kirefu hupelekea kutokea kwa magonjwa kama vile ubwiri unga na chule lakini pia mvua ikipiga kipindi cha mvua hupelekea kutofunga vizuri kwa maua. Magonjwa ya fangasi yana kawaida kutokea kama joto liko chini na unyevu huko juu na hii ni kawaida kwa miezi ya 6 hadi 8 kwa maeneo mengi..
Tutaendelea sehemu ya Matunzo yanavyoathiri uzalishaji kwa kiasi kikubwa.

Wasiliana na Mwandishi :
Agronomist mpanzi
Shamba initiatives
Morogoro-Tanzania
0714600575
|| 0620598113

IMG_20220929_121056.jpg
IMG_20220929_121035.jpg
IMG_20220929_121143.jpg
 
Kuandaa matunzo ya awali ya miche ya matunda yenye umri wa mwaka mmoja kunaweza kuwa hatua muhimu kwa mafanikio ya miche. Hapa kuna vidokezo muhimu vya kuzingatia:

Idara ya Ushauri na matunzo ya shamba
Shamba initiatives and Agritours
Maumba strt, Boma rd
Morogoro mjini, Morogoro
0714600575 || 0620598113

1. Kupogoa/Pruning-Kata matawi yaliyokufa au yaliyoathirika kwa magonjwa na wadudu. Pia, fanya upogoleaji wa fomu ili kuunda muundo mzuri wa mmea,hii ifanyike kabla mvua za vuli au masika hazijaanza. Ili kuamsha ukuaji nzuri wa miche.

2. Mbolea/Fertilizer/manure-
Samadi ni vyema itumike ila ni vizuri ikifuatana na ya kuipa nguvu ya ziada,samadi inatofautiana upatikanaji wake na nguvu pia (kuanzia mfugo mkubwa kwenda mdogo kama kuku,sungura na popo,hizi za hawa wanayama wadogo TAHADHALI KUBWA ICHUKULIWE) Za mifugo mikubwa kuanzia debe 1 mpaka 3 zinaweza kutumika.Kutokana na sababu kadhaa zinaweza kutofautisha uwingi wa matumizi.Tumia mbolea ya kiwandani hasa zenye Nitrogen au mfumo wa Nitrogen kwa kuangalia unyevu wa udongo wako,inaweza kuwa za chini au za maua kwa uwiano tofauti mfano unaweza tumia Winner,Nitrobar pamoja na Power booster,Tecamin Agriful+Tecamin raiz yaani hizi za maji. Kama miche yako ni dhaifu au ina msongo utokanao na lishe wasiliana na wataalamu kabla haujatumia mbolea.

3. Umwagiliaji-Hakikisha miche inapata maji ya kutosha. Ila ni muhimu kutomwagilia sana, kwani unyevu mwingi unaweza kusababisha magonjwa ya mizizi. Njia ya Umwagiliaji kama ni shamba kubwa vyema itumike mfano matone kwa ajili ya kuhakikisha unyevu muda wote.
Kwa miche chini ya mwaka mmoja kwenda mwaka mmoja ikiwa inatumika njia ya kawaida walau Lita 20-25 kwa kutenganisha siku kadhaa katika wiki yaani Lita kadhaa siku fulani mpaka siku fulani ili kutunza unyevu,kama maji yapo unaweza kumwagilia vizuri ila sio kwa kupitisha kiwango.

4. Kulinda dhidi ya wadudu na magonjwa:- Fuatilia miche yako kwa karibu kwa dalili za wadudu au magonjwa na uchukue hatua za haraka kama inahitajika. Matumizi ya dawa za kibaiolojia au kemikali yanaweza kufaa.
Vyema ujiridhishe dalili ya ugonjwa au namna ya uharibifu wa wadudu uliofanyika katika mche au majani.

5.Kutumia mifumo ya kusaidia:- Tumia mifumo ya kusaidia kama vile michirizi ya mmea au vifaa vya kusaidia mimea kusimama vizuri na kuenea. Hapa unaweza pia kuweka miti ya kushikia mmea au staking,kulinda mmea dhidi ya ndege au wadudu wahqribifu kama panya nk.
Hapa msaada unaweza kutofautiana kati ya eneo moja kwenda lingine

6.Kuweka ardhi safi:- Ondoa magugu karibu na miche na hakikisha ardhi inabaki safi ili kuzuia magonjwa.
Epuka kutumia sumu za magugu,epuka sana sana katika shamba la matunda.

7. Kupunguza matunda:- Mara nyingine, inaweza kuwa muhimu kupunguza matunda ili kuweka nguvu kwenye ukuaji wa mmea badala ya uzalishaji wa matunda.
Hii inaweza kuwa yenyewe au ukasaidia ikiwa mche haudondoshi maua. Ili kuruhusu nguvu ya chakula iende katika ukuaji nzuri na kwa wakati.

Kumbuka kufuatilia miche yako kwa karibu na kurekebisha matunzo kulingana na mahitaji ya kipekee ya aina ya matunda unayotamani kupata.
FB_IMG_1694553539258.jpg
 
Kumbuka kufuatilia miche yako kwa karibu na kurekebisha matunzo kulingana na mahitaji ya kipekee ya aina ya matunda unayotamani kupata.View attachment 2770444
huo mche hapo kwenye picha maua yake hutoa matunda kweli au hupuputika hadi uwe na nguvu
 
Back
Top Bottom