Uliwezaje kuachana na mtu uliyempenda?

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
May 30, 2021
333
673
Habari wakuu mm nisingependa kuwachosha naomba niingie moja kwa moja mada husika:

Mwaka 2020 mwezi wa kwanza nilitongoza kadem( 20 age)ka mtaa ambapo nilikua nafanyia biashara zangu, wakati ndo tumeanza mahusiano nikaja kugundua kua huyu binti alikua anatoka na kwenda club usiku, kwakua alikua anaishi na dada yake tu kwenye nyumba za kupanga hivyo alikua na uhuru japo kua dada yake hakua na tabia kama zake.

Nilipo gundua nilikaa nae chini na kumwambia maisha anayo ishi si mazuri hasa kwa mwanamke ambaye anaplan za kupata mume bora, sisi wanaume hua tunachagua sana yupi dem wa kuoa yupi wa kumla tu. Offcouse alinielewa.

Baadae nimeishi nae kama miezi mitatu akaanza kunigusia mambo ya kumtoa out, kwakua mwanzo wiki ya kwanza ya mahusiano alikua anatolewa out na jamaa mmoja hivi ambaye aliondoka mtaa ule kwa baadae, nilipo gundua nikamwambia maisha ya uongo siyapend kwenye mahusiano kama huwezi kua na mie ni bora kmya kmya unipotezee akanielewa.

So kwa sababu hiyo nikaona ni bora mala moja moja niwe nakatoa out tunaenjoy maisha.

Nilikatoa out na siku hiyo ikawa siku ya kwanza mm kufundishwa mambo ya kwenda club na mwanamke pamoja na kunywa pombe, mm binafsi skufurahia maisha hayo ila nilifanya kumfurahisha huyu mpenzi wangu, hata nilipo kua pekeyangu niliapia kua hakika huyu si mwanamke wa ndoto zangu lazima nitaaachana nae, tumeishi wote hatimaye dada ake akahamia kalibu na getoni kwangu.

Dada yake alikua na boyfriend ambaye alikua anakuja kula na kupiga mbunye kwa sisita na kuondoka, baada ya mm kuishi na mdogo wake dada ake akachukulia kama chance ya kumvuta huyo boy wake kwake na wakaanza kuishi wote.

Dem wangu hakua na namna ikabid awe analala kwangu tukaanza maisha akawa akuja jion anapika asubuh anaenda kwa dada ake mwishoe akaonekana kama mke wangu hata kwa wapangaji wenzangu, lakin mm na yeye tulitambua kua tupoje.

Maisha yakaenda mikasa na changamoto tukapitia + kusaidiana mpaka mwaka ukaisha tukiwa ote kwenye mahusiano na mwezi wa kwanza mwkaa 2022 tunakamilisha miaka miwili ya mahusiano. Bado naapa hata leo hakika huyu si mke wangu kwakua bado anapenda kunywa pombe.

Sifa za huyu dem mbaya na nzuri.

1: Ni msafi sana anajua kupika na ana nijali ila hapendi kukosolewa.

2: Hajasoma kaishia darasa la saba.

3: Hajui biashara yoyote tofauti wala hana future na maisha yake.

4:Hasali.

5: Sio mchoyo kwa upande wa chakula na

6 : Mcheshi sana na nchangamfu hata kwa wageni.

7: Kutokana na maisha yake ya uhuru sana hana tabia ya kunipelekea maji ya kuoga bafuni ila nilimfindisha akawa anapeleka.

Hizo hapo juu ni sifa zake baadhi ambazo mimi naona hazitoshi kua mama wa watoto wangu.

Kwasasa mimi nimeanza kuyumba kiuchumi, na nimeyumba kweli sababu kubwa ni wezi, na biashara kukosa wateja ni (m.pesa na tigo pesa) nazani hii biashara kwa sasa mawakala wanajua inavyo waumiza akili.

Kutokana na sababu ya kiuchumi nimekusudia kuhama mkoa na kwenda mbali kiutafutaji, nikajipange upya lakini pia sababu ya kiuchumi inanipa nguvu na kunikumbusha huyu si mke wa ndoto zangu hivyo natakiwa nimuache mala moja.

Sasa wadau mda umefika na nilimuweka wazi hali ya kiuchumi niliyo nayo kwa sasa na yeye mwenyewe anaona uhalisia ila jana nimemwambia kua mda wa mm kuondoka umefika naona kaishiwa raha na mda wote analia, anaonekana ni mtu wa mawazo sana na kiukweli ananipunguzia nguvu ya kuamua kuondoka na kwenda kupambania maisha yangu huko ninako kwenda.

Nimedhamilia kumuachia hela ya mtaji, na nitaondoka nitamwachia geto ambapo nimekusudia nisipo rudi litakua ni sadaka kwake yeye aanzie maisha yake hapa, nitamuachia chakula cha kutosha ndani.

Nafanya hivyo ili iwe kama kulipa fadhira ya wema alio nitendea kwangu(kunipikia,kufua uaminifu wake kwangu) hivyo yani.

Ila nimeanua kumuacha kwakua hawezi kuacha pombe kwakua nilisha muonya ila bado anakunywa kmya kmya na kumpiga siwezi, nilimwambia aanze kwenda kanisani ila hatekelezi, hana maarifa hivyo nahofia kumuoa akiwa mama watoto wangu tutagombana juu ya kulea watoto kwakua mm nataka watoto wangu wapate malezi wawe na maadili ya kidini, ila yeye hayupo hivyo.

Wadau naombeni ushauri na experience uliwezaje kuachana na mtu unaye mpenda?
 
Sema ni ngumu sana kupata mwanamke alie kamilika idara zote, Unaweza kumuacha huyo ukaja kupata mwanamke mwingine ambae utadhani yeye ndo chaguo lako kumbe umeingia cha kike! Em jaribu kumfundisha mengi zaidi yaliyokua mema naamini ataelewa tu kama ulivyosema kuna mambo kama mwanamke anatakiwa kuyafanya kwa mwanaume umemfunza na akaanza kufanya.

Mfundishe biashara nashangaa eti wataka kumkimbia na kumwachia mtaji wakati hata biashara yenyewe hujamfunza sijui ndiyo plan gani hizo unafanya bro, mkalishe chini na mpe mipango yako na yeye ya baadae mpe nafasi akupe mawazo yake uskie anasemaje, alafu mimi naona wakati huu unadai umeyumba ki uchumi ndio muda sahihi wa kumpima uvumilivu wake na upeo wake ki akili, yastajaabisha ww ndo unataka kumkimbia ati badala yeye ndo tungetegemea aanze harakati za kukukimbia au aseme anataka kuondoka. Mwanamke siku zote ni kama mtoto tu anapaswa kuelekezwa wakati mwingine jinsi ya kufanya lifestyle inayofaa.

Ogopa sana kuishi na mwanamke ambae ni mkimya, mpole na anakuskiza tu kila kitu unachomwambia unaona anatekeleza naww unafurahi na kumuamini zaidi, Huwa wabaya sana na wana hesabu kali, wajanja sana anaweza kukupiga tukio la kushangaza ambalo hutakaa huamini au unakuja gundua ana mambo anafanya undercover pasipo ww kujua..
 
Nashukuru Sana kwa USHAURI wako Mkuu. Nimewaza kuto muacha ila nitatoka kwenda KUTIMIZA moja ya plan zangu ili kubust uchumi baadae nitamuita niishi nae.
 
Nilijikuta namtoa Moyoni mdogomdogo pasi yeye kujua na hatimaye nikamove on
Ingawa alinitafuta ila sikuwa na hisia naye Tena kama mwanzo siyo Siri kipindi yupo Moyoni mwangu hata angenambia nilipe mahari 7m ningekopa equity ili nimuoe
 
Back
Top Bottom