Morg
JF-Expert Member
- Oct 20, 2018
- 1,301
- 1,767
Habari za muda huu, ni siku tulivu sana hapa. Jiji la Dar es Salaam kumekucha salama, ingawa kulikuwa na upepo wa baridi sana, poleni na natumaini kila mmoja wetu ni mzima kabisa. Nawatakia kila la kheri katika pilika za kuijenga Tanzania kuwa kubwa tena, yenye amani na upendo. Twende kwenye mada.
Kuna kipindi kwenye Life cycle ya kimaisha ilinifanya nihamie kwa uncle wangu kuishi nae ili kuangalia uwezekano wa kufanya maisha. Enzi zile ndio nimemaliza masomo nipo home tu nikapata mchong huo, nilikuwa very excited sana na hili, maana nilikuwa ninavuta picha fulani hivi kabla ya kufika kwa uncle Dar.
Siku mbili baada ya kupewa taarifa ya safari nilijiandaa lakini ilikuwa ghafla sana kutokana na uchu wa safari ya kuja huku hata watu niliokuwa nawadai pesa zangu wengi niliwapotezea, kitu ninachojutia sana.
Siku ya safari ikawadia, panda nikapanda basi safari mpaka Dar, nifika mida ya saa moja hivi enzi za ubungo terminal pale, akaja mshakaji aliyekuwa anakaa kwa huyo uncle, wakanichukua freshi mpaka home.
Hapo nipo so excited na wishes nying sana how it's going to be in the up coming day's, nikachil, nikafika home. Yale mapokezi tuu yakanidropisha point. Yule mke wake alikuwa anagubu sana, nilivyofika nikaona hapa chakike.
Picha linaanza kulipokucha tunaamshwa saa kumi na moja tufanye usafi, duuhh nilichoka. Kumbe wanafuga mbwa, sehemu padogo mbwa wanajisaidia, morning ni kuzoa na kusafisha kumwaga maji, nilichoka. Ila nikajikaza kumbe bado kuna kuosha magari usiku unaamshwa uoshe, kibaya zaidi ni kila siku iwe mvua au jua.
Kibaya zaidi ni huyo mke wake alikuwa na visa na maneno ya shombo, mara hataki watu watoke nje ya geti anafunga, mara hataki watu wakae sebuleni, hata kunywa maji ya kwenye friji jau, akinunua matunda mpaka akupe yeye na atakupa wakati linaanza kuharibika ukila atakuja kuongea mpaka ujute.
Kwa kipindi kile ilikuwa ni mateso sana, sabuni ya kuogea unajinunilia, mafuta ya kujipaka pia, tulikuwa tunajitegemea kama tumepanga hata kipindi tunaenda K/Koo ilikuwa ni taabu sana.
Ilinipasa kuishi kama mtoto wa miaka kumi kushuka chini, maana ni kama sikuwa najielewa. Maana watu walikuwa wanakuja pale wanashangaa tunawezaje kuishi na hawa, hata wadogo zake na yule mama walishindwa kukaa nae, wengine walikimbia na kutoroka. Ila ndo changamoto tunazokutana nazo katika maisha ya wengi wetu.
Sent using Jamii Forums mobile app