Ulishawahi kutoka usingizini na kudhani umechelewa kwenda shule au kazini?

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
17,796
32,148
Hello,

Ushawai kulala mchana ukaamka ukaona kama umechelewa kwenda shule au kazini?

Mimi imeshawahi nitokea nikiwa nimelala mchana nikaamka nikaona mbona kama nimechelewa shule, nikaamka chap, nikakimbilia bafuni kuoga na kuvaa sale za shule.

Sasa nikiwa navaa viatu kaka akaingia chumbani, akaniuliza unaenda wapi jioni? Nikamuuliza kwani saa ngapi? Akaniambia saa kumi na moja, dah nilijitukana sana nikavua chap.

Je, wewe ishawai kutokea?
 
Mimi iliwahi kunitokea nimelala mchana kwenye saa tisa kuja kuamka saa moja usiku kigiza kama kile cha alfajiri. Kilichonizuzua zaidi nilimkuta bi mkubwa anapika chai. Mimi nikajua ndo kumekucha tena nikaenda nikaoga nikaingia chumbani. Tupia Uniform daa, natoka ndo naulizwa unaenda wapi? Usiku huu nikasema shule.. Nikaambiwa embu Acha wenge sa hivi ni saa moja usiku.. Nilijiona boya sana..
 
Mimi iliwah kunitokea nimelala mchana kwenye saa tisa kuja kuamka saa moja usiku kigiza kama kile cha alfajir. Kilichonizuzua zaid nilimkuta bi mkubwa anapika chai. Mi nikajua ndo kumekucha tena nikaenda nikaoga nikaingia chumbani.Tupia Uniform daa,natoka ndo naulizwa unaenda wapi? Usiku huu nikasema shule ..Nikaambiwa embu Acha wenge sa hivi ni saa moja usiku..Nilijiona boya sana..
Et unaenda wapi usiku uhu 🤨🤣🤣🤣
 
Pole sana mkuu
 
How was it?
Kipindi hicho niko olevel Nakumbuka kuna siku nililala ilikua jionijioni hivi nikaja kuamka kama saa moja na nusu hivi.. nikaenda kuoga fasta na kuvaa uniform na viatu na kila kitu.. nikawa nmesimama mlangoni naulizwa vipi nasema namsubiri baba aamke anipe lift niende shule...walinicheka hadi nilijiskia vibaya sikuile
 
He'll

Ushawai kulala mchana uka amka ukaona kama umechelewa kwenda shule au kazini?

Mimi ishawai nitokea nikiwa nimelala mchana nika amka nikaona mbona kama nimechelewa shule nikaamka chap nikakimbilia bafuni kuoga nikavaa sale za shule sasa nikiwa na vaa viatu kaka akaingia chumban akaniuliza unaenda wapi jioni nikamuuliza kwani saa ngapi akaniambia saa kumi na moja dah nilijitukana sana nikavua chap

Je wewe ishawai kutokea?
Usitupange we mnyakyusa ina maana uliogea chumbani?
 
Mimi iliwah kunitokea nimelala mchana kwenye saa tisa kuja kuamka saa moja usiku kigiza kama kile cha alfajir. Kilichonizuzua zaid nilimkuta bi mkubwa anapika chai. Mi nikajua ndo kumekucha tena nikaenda nikaoga nikaingia chumbani.Tupia Uniform daa,natoka ndo naulizwa unaenda wapi? Usiku huu nikasema shule ..Nikaambiwa embu Acha wenge sa hivi ni saa moja usiku..Nilijiona boya sana..
Halafu kile kigiza cha jioni jioni kinanikeraga sana yani😂😂🙈
 
we ni wa kishua yaan kwenda kuoga bafu lipo huko nje... mita 30 kutoka ulipolala....afu usishtuke kweliii!!??
 
Kipindi hicho niko olevel Nakumbuka kuna siku nililala ilikua jionijioni hivi nikaja kuamka kama saa moja na nusu hivi..nikaenda kuoga fasta na kuvaa uniform na viatu na kila kitu..nikawa nmesimama mlangoni naulizwa vipi nasema namsubiri baba aamke anipe lift niende shule...walinicheka hadi nilijiskia vibaya sikuile
Ahahahha lift lakini
 
Daah muda mrefu sana kuna siku ilikua juma mosi kulikua na maulid kwaiyo tukakesha mpaka juma pili asubuhi nikarudi home saa 3 nikafua fua kiuvivu uvivu mpaka saa 5 nikaanza kuhisi usingizi mzito nikaenda kulala nimekurupuka saa 11 jioni kijua kinaanza kuzama nikaona nishachelewa shule nilijiandaa haraka haraka nataka kuondoka marehem bibi ananiambia wee vipi kulikoni nikamuambia nawahi namba shule akaniambia mjukuu wangu hawajakuroga kweli huko ziarani ndo akili kurudi kumbe jioni aisee
 
Ahahah ulilogeka vibaya
 
Back
Top Bottom