Ulipataje Scholarship kusoma Abroad? Karibu tupeane experience namna ya kupata scholarship broad

EEM M

Senior Member
May 20, 2022
132
285
Wasalaam wana JF!

Bila shaka wote ni wazima na ambao hawapo sawa basi Mungu atawaponya soon, Amen.

Baada ya salamu naomba niende straight kwenye Mada.

Ni ndoto ya vijana wengi nikiwemo mimi kuvuka border na kwenda kuongeza elimu ikiambatana na kupata changamoto nyingine katika nchi za wenzetu waliotuzidi technology pamoja na level ya elimu.

Je, wewe ulishawahi kupata scholarship au ulishawahi kumsaidia mtu akapata scholarship?

Umekuwa ukipambana sana kupata scholarship bila mafanikio?,... Basi tukutane hapa maana naamini umoja ni nguvu na sharing is caring.

Kama ulishawahi kupata scholarship au una knowledge juu ya namna, techniques au hata ujanja wa kupata scholarship ya kusoma Abroad basi karibu u-share na sisi pia hapa.

Binafsi nilishawahi kujaribu ile ya INDIA ya SII lakini nilipata 25% on tuition fee so ikabidi niipige chini.

Nimefungua huu uzi ili tupeane maujanja na techniques za kutoboa Abroad kupitia elimu.
 
Ukimaliza form 4, 6, (sijajuwa kwa degree) unaweza kufanya mitihani ya SAT inayosimamiwa chini ya ubalozi wa Marekani .

SAT ndio mtihani wa taifa wa Marekani, kwa bahati nzuri wanaruhusu na nchi zingine kuufanya na wanaofaulu wanaweza kufadhiliwa kujiunga na vyuo marekani.

Kwa hapa Tanzania gharama huwa ni laki 2 na nusu hivi, ukilipia unapewa na material kama pastpapers kwajili ya maandalizi.

Mitihani kama hesabu ni mirahisi sana, Mmarekani ukimpa paper ya hesabu ya Necta yetu anaweza kuikimbia.

Mitihani huwa inafanyika shule ya International school of Tanganyika , ipo Masaki.

Nawajua marafiki wawili wa mdogo wangu walipita njia hii, moja alienda Yale university mwengine Miami huko.

Tatizo hii ni siri ya familia chache hawapendi isambae na sitashangaa kule ubalozi watakupa ushirikiano ila ukifika pale IST kuna wabongo wanaweza kukukatisha tamaa ama kufanya figisu maana unaingilia nafasi za watoto / ndugu zao, ikitokea hivi wewe waambie ubalozi wamekuruhusu upige pepa wasikusumbue na kama ni kulalamika uende kwa ubalozi sio kwa wabongo hao utaowakuta.

Binafsi watoto ntawapambania huku watesti zali maana nimeshuhudia kwa macho yangu watu wameenda kusoma vyuo Marekani kwa njia hii.

Tembelea ukurasa huu kwenye tovuti ya ubalozi wa Marekani ujue zaidi kuhusu Sat, sehemu za kufanya pepa, gharama, sifa, n.k.

Ukimaliza form 4 hata ukiwa tayari umeanza 5 ama upo 6, unaweza kufanya mitihani ya SAT inayosimamiwa chini ya ubalozi wa Marekani .

gharama huwa ni laki 2 na nusu hivi.

Mitihani huwa inafanyika shule ya International school of Tanganyika , ipo Masaki.

Nawajua marafiki wawili wa mdogo wangu walipita njia hii, moja alienda Yale university mwengine Miami huko.

Tatizo hii ni siri ya familia chache hawapendi isambae na sitashangaa kule ubalozi watakupa ushirikiano ila ukifika pale IST kuna wabongo wanaweza kukukatisha tamaa ama kufanya figisu maana unaingilia nafasi za watoto / ndugu zao, ikitokea hivi wewe waambie ubalozi wamekuruhusu upige pepa wasikusumbue na kama ni kulalamika uende kwa ubalozi sio kwa wabongo hao utaowakuta.

Mitihani kama hesabu ni mirahisi sana, Mmarekani ukimpa paper ya hesabu za Necta anaweza kuikimbia.

Tembelea ukurasa huu kwenye tovuti ya ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ujue zaidi kuhusu Sat, sehemu za kufanya pepa, gharama, sifa, n.k.

Hao wadogo zako walipata vipi scholarship? Hilo ndio swali la mtoa mada. Utakuwa umemsaidia sana ukielezea kwa urefu.
 
Unaweza kufaulu mtihani lakini ukakosa mfadhili wa kukusomesha chuoni kama ilivyo kwetu unaweza kupata division 1 ila ukakosa mkopo.

Ukipiga hio pepa utatumia matokea yake kufanya maombi ya vyuo, lakini sasa vyuo vya wenzetu gharama ni kubwa, ibabidi upambaen upate ufadhili wa kusomeshwa na ndio hapa sasa huwa kuna kitu cha ziada kinaitwa extracurricular activies, hapa ni vitu kama kutoa misaada kwenye jamii, kuvolunteer kufanya shughuli za kijamii, kufanya tafiti, kuwahi kuwepo kwenye serikali ya shuleni, n.k.

inabidi uwe una ushahidi kwamba umeshawahi kufanya chochote chenye kuonyesha utasaidia jamii kwa elimu yako, kama unataka kozi za jamii tembelea kijijini uwe na ushahidi wa picha unawapa neti za mbu kuonesha unaumizwa na malaria inayoua waafrika wengi na wewe upo katika harakati za kupiga vita Malaria, kama wataka kozi za sayansi fanya project yoyote, n.k. hii inakuwa inashawishi zaidi kupata mfadhili wa kukusomesha aone kwamba hata ukisomeshwa elimu yako itakuwa na msaada kwenye jamii ukihitimu masomo yako.

Kufanya paper ya SAT pekee unaweza kufaulu lakini hakikisha kwenye extracurricular activities usiwe mtupu,

kuhusu hio sat fika ubalozi wa marekani ukiwa na kama laki 2 na nusu hivi (makadirio), utasajiliwa, utapewa material kama pastpapers, kuungwa kwenye system yao kwajili ya updates na pia mambo ya form za kufadhiliwa gharama za kusoma nje.
 
Nadhani ukishafanya na kufahulu Mitihani automatic unapata ufadhili ila acha tusubir mdau atueleze vzr
 
Shukran sana kwa mchango wako mkuu
 
Back
Top Bottom