Ulinzi wa Watoa Taarifa za Rushwa

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Ulinzi wa Watoa Taarifa, lililopitishwa Desemba 2015 linasisitiza umuhimu wa kuwalinda Watoa taarifa na kuhakikisha wanaweza kutoa taarifa kwa Uhuru bila kuogopa mashambulizi au kisasi

Azimio hili linahimiza nchi Wanachama kuanzisha na kuboresha Mifumo ya Kisheria na Sera zinazowalinda watoa taarifa

Huku kwetu wanaotakiwa kupambana na walarushwa baadhi yao nao wanakula rushwa.
Wakipelekewa taarifa wanawaambia walengwa.
Hiyo sheria huku haiwahusu
 
Hii ni ngumu kumeza, unavaa bomu na kujilipua makusudi.

Siku zote huwezi peleka kesi ya Nyani kwa Nyani ukategemea upate matokeo chanya.

Hao unaowapelekea mashitaka ndo waandamizi wa kula rushwa tena wana mtandao ambao wewe pangu pakavu tia mchuzi hawatakuacha salama japo ulikuwa na nia njema.

Kuna mwamba mmoja alivuta pumzi ya moto sehemu "x" baada ya askari kuvujisha taarifa kuwa aliyekuchoma ni "y".
 
Kwa Tanzania ukitoa taarifa kama hizo ,usishangae night kali wanakujia "Na hapa ipo" maana polisi wetu wanasema walipopata taarifa.
 
Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Ulinzi wa Watoa Taarifa, lililopitishwa Desemba 2015 linasisitiza umuhimu wa kuwalinda Watoa taarifa na kuhakikisha wanaweza kutoa taarifa kwa Uhuru bila kuogopa mashambulizi au kisasi

Azimio hili linahimiza nchi Wanachama kuanzisha na kuboresha Mifumo ya Kisheria na Sera zinazowalinda watoa taarifa

View attachment 2924298
Tanzania inahitaji uzingativu mkubwa katika utekelezaji wa Tamko hili.

Hao wapokeaji taarifa wana maadili yanayowafanya waaminike? Nauliza hivyo kwa sababu tumeshuhudiwa Taasisi ya TAKUKURU ikitumika kisiasa kama fimbo kwa wenye mawazo na maoni tofauti kuhusu miendendo inayotia shaka ya watawala.

Tunahitaji sana sasa kuwa na mfumo unaojitegemea na unaojiendesha kwa mujib wa katiba unaodeal na haya masuala ya rushwa.
 
Back
Top Bottom