Ulimwengu ampa rais ajaye - Dr Slaa - ushauri murua

Kwani mtu aliyepata div 3 hawezi hata siku moja kumshauri aliyepata div 1? Wewe unadhani ukipewa hata ubalozi wa nyumba10 utaweza? Wenye kujua uongozi tunajua mazingira yanavyoathiri leadership contingently,judge the made advice regardless the adviser is impared or otherwise

Anywy,Ukubwa dawa na kuishi kwingi kuona mengi,naamini ushauri umetolewa kwa mda muafaka na kwa mlengwa muafaka.
 
Comrades, Ulimwengu kanena, tena kanena maneno ambayo akili zetu iyaweke rohoni. Duh! Katoa picha halisi siasa kisiasa Tz tulivyo.
Rais tulitarajia 'angetutoa' kumbe alitaka kutoka yeye na washkaji wake wa Laibon (au aliutaka urais bila kufahamu nini maana yake).

Tumaini letu jipya limezungukwa na maswaibu ya ya kupakaziwa, lakini pia ni wagumu. Ulimwengu kasisitiza umuhimu wa katiba mpya itayotokana na wananchi.
 
Ulimwengu ni mmoja wa wazalendo wachache ambaye ana fikra huru na hafungwi na itikadi za chama lake la magamba!
 
ukweli mnaoukubali ni ule unaowafurahisha.slaa hana uwezo wa kuongoza nchi,hana elimu itakayowanufaisha wananchi zaidi ya kisomo cha sheria za dini
 
hata kama Generali Ulimwengu katumwa (kama wewe unavyotaka tuamini) mbona ushauri wenyewe ni mzuri? Hacha chuki zako zisizo na msingi.
 
Kwanza kabisa ninapenda kumpongeza Generali kwa maoni yake mazuri na wala sina la kumkosoa, ila na la kuongeza kuhusu hali ya kisiasa nchini. kwanza kabisa ningependa kutahadharisha kwamba elimu ya uraia haitoshi.

Ili wanachi waweze kutoa maoni yao mbalimbali, pamoja hata na yale yahusuyo katiba inabidi wapate elimu ya uraia. Kwa sababu kwa makusudi kabisa, kwa kutumia USSR style taifa letu limekuwa likitumia vyombo vyake kuhakikisha raia hawajua hata haki zao za kimsingi kikatiba, hata ukitaka kukusanya maoni yao yatakuwa finyu sana ukiondoa wasomi wachache sana.

Hivyo kazi anayofanya Dr slaa na wenzake kwa sasa ni muhimu sana, yaani kuwaeleza wananchi kwamba wako wapi, tulitoka wapi na muelekeo wa serikali iliyopo madarakani ikikinzana na haki za msingi za wana wa nchi.

Mfano kwanini mrahaba ni asilimia 3%, na hii ina maana gani kwa maisha yetu ya kawaida. Kwanini ccm inagawa kanga wakati wa uchaguzi na hii ina maana gani kwetu. kwanini makampuni kama Kagoda hayagusiki licha ya kula mabilioni ya uma. Kwanza katiba yenyewe ni nini. Serikali ni nini.

Baada ya wananchi kuelewa mambo ya msingi, ambayo hawawezi kuyapata kupitia TBC wala TV nyingine, wala radio zilizojaa uoga, mikutano ya kuelimisha umma Tanzania nzima inahitajika sana mwanzo.

Hii ikiambatana na maneno ambayo sihamini hata kidogo kama serikali ya sasa ingependa. Halafu sasa naamini tutapa maoni ya umma kuhusu mustakabali wa taifa letu.

Nasikitika kusema kwamba Dk Slaa na wenzake wanahitaji kuanda semina hata ya bunge zima, kuwajenga katika uzalendo hasa katika mambo waliyokuwa wakisema (Ndio na sio bungeni).

Watanzani tuko chini mno, kufikia kiwango cha kutoa maoni tija. Labda watu wachache kama Generali.

Kinachosikitisha ni kwamba kwa sasa CDM wameachwa peke yao katika kutoa elimu ya uraia. Kumbukeni tuna vyombo vingi vinavyoweza kutoa elimu hiyo lakini vimejaa uoga au kukosa uwezo wa kuwafikia wananchi.

Tujiulize wananchi wangapi wanajua tunaibiwa katika migodi. Wangapi wanajua waliokufa Nyamongo ni mashujaa. Wangapi wana soma magazeti kama mwanahalisi, au Tanzania daima. Dawa ni kuwafuata huko huko vijijini na kutoa elimu hiyo.

CDM imeshagundua kwa sasa kutegemea TBC hamna kitu. Inahitaji kuunda miondombinu ili kuweza hata kupokea hayo maoni.

Nani hajui kwamba serikali za mtaa haziwezi kusogeza mbele maoni ya wananchi. tunakaa nao hawa ni walaji tu wakitumia udhaifu wa elimu ya uraia ya wananchi, angalia report ya mrema na zito.

Pamoja na maoni mazuri ya General, kuna preliminary work to be done before the Gen recommendation find a foundation to stand. But all in all it was exellent contribution.:hatari:
 
Spanner,
Mkuu acha siasa za majitaka. sasa unapomvua nguo Ulimwengu ni ktk kuonyesha kwamba hawezi kuwa mshauri mzuri au unayakana maelezo yaliyoandikwa kwa sababu unafikiri Dr.Slaa amekomaa kisiasa. Na sijui kama unaweza kutuambia ni vigezo gani unavyotumia maanake napomsoma Ulimwengu yeye ameandika kutokana na matukio yaliyokwisha tokea na kwa kuzingatia siasa za Tanzania..

Tahadhali na mameno ni muhimu sana na hakika Dr.Slaa aliposema kuiondoa serikali ya JK sio Uhaini inaweza tafsirika vibaya...Kumbuka tu kwamba siasa za Tanzania ni majungu ambayo siku zote hayakosi Ukoko. Ni muhimu sana kuhamasisha wananchi ktk jambo ikiwa chama kimeshachukua mkondo huo. Hapa nikiwa na maana hao kina Mandela, Castro na wengineo walikwisha amua kwamba Mapinduzi na uhuru wa nchi zao hautapatikana kwa kupitia sanduku la kura..

Hivyo, kwa zitatumika nguvu nyinginezo za Umma ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya utawala kuhakikisha unang'olewa..Na alichoasa Ulimwengu ni kauli zinazopelekea watnanchi kufikiri kwamba chama kimefikia maamuzi hayo na hivyo wapo tayari kupambana na chama tawala kwa kupitia nguvu nyingine nje ya sanduku la kura..

Kwa hiyo nadhani Ushauri wa Ulimwengu ni mzuri tu kama hutautazama kwa jazba maanake siku hizi CCM usimtaje JK na Chadema usimtaje Dr.Slaa kuwa na makosa fulani. hawa ni binadamu kama sisi na wanaweza kabisa kutumiahisia zao nje kabisa ya mila na desturi za siasa ktk kutafuta demokrasia ya kweli..
 
Ulimwengu katumwa na Kikwete. DK. Slaa alishajifunza sana miaka kingi iliyopita. Kwanza, ninyi mnaotaka kumpa heshima huyu kibaka mnaitoa wapi? Unajua huyu akiwa mkuu wa wilaya ndiye aliyezuia mkutano wa kwanza wa mageuzi, hadi pale wanaharakati kama Mabere Marando, Ndimara Tegambage, Anthony Komu walipojitokeza na kupinmga udhalimu wake?

Wanaharakati hao waliandika waraka kwenda nchi za Magharibu na nakumbuka rais wa wakati huo, Ali Hassani Mwinyi aliruhusu wanamageuzi kukutana alipokuwa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akienda ulaya kuomba misaaada baada ya kubanwa na wafadhiri. Sasa huyu Ulimwengu analipi la kujivunia.

Pili, Ulimwengu alikuwa mwenyekiti wa kampuni kubwa - Habari Copr - ikamshinda na badala yake akaiuza kwa fisadi Rostam. Sasa mtu aliyeshimdwa kuongoza watu 200 atawezaje kumshauri rais ajaye?

Anachotaka kukionyesha Ulimwengu hapa ni kwamba Slaa hajakomaa kwa urais hivyo ajifunze. Hili si kweli. CV ya Slaa ni kubwa kuliko yeye na kimsingi Slaa amekuwa kiongozi mkubwa wa madhehebu ya dini, mbumge na katbu mkuu.

Ulimwengu aondoke na pumba zake arudishe jibu kwa Kikkwete - Hatudanganyiki. Angekuwa mrtu wa maana Mkapa asingemvua uraia.

Kimsingi wewe una matatizo, kama wewe ni mwanamageuzi basi upo kwa bahati mbaya, jenerali alifanya matakwa ya watawala wakati akiwa mkuu wa wilaya na yeye kama mwanasiasa makini anakwenda na mabadiliko japo wewe hukubaliani na hali hiyo, hao wasio makini wao hawataki kubadilika na mwisho ni kufutika kama sio kupotea kisiasa, Mkapa alimvua uraia kwa chuki binafsi ambazo hakuna haja kwa leo kuziorodhesha, pia hakushindwa kuendesha kampuni ya habari corp. ila baada ya kugundua kuwa sehemu ya hisa walizouza (jambo ambalo ni sawa katika mfumo wa soko huru) zina mafisadi wakaamua kuuza zilizobaki na kwenda kuanzisha kampuni nyingine ili kuwa huru katika habari na sio kutekeleza matakwa ya mtu/watu flani
 
ukweli mnaoukubali ni ule unaowafurahisha.slaa hana uwezo wa kuongoza nchi,hana elimu itakayowanufaisha wananchi zaidi ya kisomo cha sheria za dini

Hebu tutajie wenye uwezo wakuiongoza nchi? Kuongoza nchi sio vyeti ulivyokusanya mkuu, hebu tuambie tuna maprofesa wangapi na madaktari wangapi wizara tu zinawashinda? Unaweza ukasoma vitu vingi sana kwenye maisha lakini ukashindwa kuvi-apply practically. Elimu ni muhimu I agree, lakini mtu asije akaja na title ya Prof, Doctor etc tukafikiri ndio anaweza kazi. Inawezekana mtu huyo huyo akaitumia hiyo high IQ aliyonayo kutuibia rasilimali zetu (kwa manufaa yake binafsi).
 
Nimeikubali hii makala ni soo, viva ulimwengu, viva wanaharakati na wapenda maendeleo na inchi yao kama Tanzania,
 
Jibuni hoja, badala ya kunishambulia. Nimesema Ulimwengu ameshindwa kuendesha kampuni yake ya watu 200 atawezaje kumshauri rais mtarajiwa? Tatizo lenu mnashabikia watu msiowajua. Mtu mwenye uraia wa kuandikishwa atakuwaje mzalendo? Huyu jamaa namfahamu ni mbinafsi kupindukia.

Alipokuwa habari alishindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Baadaye kampuni ikazidiwa na mzigo wa madeni. Ikafilisika.

Pamoja na kupewa mtaji na Mkapa na marafiki zake - kabla ya Mkapa hajaamua kumuanika kwa kumtangaza kuwa si raia - tayari Jenerali na wenzake - Salva na Mwambo walishashindwa kuendesha kampuni.

Wafanyakazi wakawa hawalipwi kwa wakati, huku yeye akisafiri kila mwezi kwenda kwa mkewe Afrika Kusini. Naye Salva akawa anaenda Uingereza kwa mkewe. Haikuchukua muda mambo yakaenda kombo.

Alipoingia Kikwete madarakani akaanza kujipendekeza kwa kuandika maka ndefu alizozipa kichwa cha maneno, "Barua ndefu kwa Rais KIkwete." Leo eti anakuja kutaka kumshauri Slaa na kujita mwanademokrasia. Mwanadipromasia gani anayezuia mageuzi? Aaache kujipa sifa asizokuwa nazo.

, kampuni taya
 
ukweli mnaoukubali ni ule unaowafurahisha.slaa hana uwezo wa kuongoza nchi,hana elimu itakayowanufaisha wananchi zaidi ya kisomo cha sheria za dini

Safi sana Dosantos tunataka ma GreatThinker kama wewe, sasa nakushauri hebu andaa thread yako iwe na qualification za urais ili Dr Slaa na wengine wasio na uwezo tuwanyime nafasi hiyo nyeti.

Pia kwenye thread yako usisahau kuweka sifa walizokuwa nazo waliotangulia na mafanikio (outputs) ili ikibidi tutafute JeyKey mwingine wa kuliongoza jahazi salama
 
ukweli mnaoukubali ni ule unaowafurahisha.slaa hana uwezo wa kuongoza nchi,hana elimu itakayowanufaisha wananchi zaidi ya kisomo cha sheria za dini

Unaalosema ni kweli kuwa kuna watu wanapenda kusikia ushauri unaowafurahisha tu, hilo mimi ninakubaliana na wewe, lakini katika suala la elimu, hata mimi nina wasiwasi na elimu yako, nahisi huna elimu ya kukufaa kuwa mtanzania au kuishi nchi hii.
 
Muulizeni huyu Ulimwengu wenu, ni nani aliyezuia wanamageuzi kukutana pale Diamond Januari 2002? Kama si harakati za wanamageuzi, hayo maandishi yake ya leo angeandikia kwenye ukuta? Mbona yeye alikataa ujio wa vyama vingi na uhuru wa kujieleza? Akamshauri ******. siyo Dk wa ukweli. Huyu tayari amefuzu.

Pamoja na kumchakachua zaidi ya watu 2 milioni wamemuamini na kumpa kura. Ulimwengu anakura ngapi?
 
Akijipa muda wa kujifunza zaidi na kukusanya maoni, na kujenga mitandao ya utafiti itakayowahusisha wataalamu wa kumshauri na kukishauri chama chake, akichukua muda kujadili matatizo ya nchi hii na makundi mbali mbali ya kijamii katika shughuli zao mbali mbali na wakamweleza matatizo yao; naye akajadiliana nao... atakuja kugundua kwamba hakuna muda wa kutosha kwa ajili ya maandalizi hayo.

[/COLOR]
[/FONT]
[/B][/SIZE]

Maneno haya yamenikuna na yananishawishi kuamini kuwa 2015 Ikulu itakuwa wazi na kweli tutapata tumaini jipya watz. YAZINGATIWE KWA UMAKINI WAKE
 
Jibuni hoja, badala ya kunishambulia. Nimesema Ulimwengu ameshindwa kuendesha kampuni yake ya watu 200 atawezaje kumshauri rais mtarajiwa? Tatizo lenu mnashabikia watu msiowajua. Mtu mwenye uraia wa kuandikishwa atakuwaje mzalendo? Huyu jamaa namfahamu ni mbinafsi kupindukia.

Alipokuwa habari alishindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Baadaye kampuni ikazidiwa na mzigo wa madeni. Ikafilisika.

Pamoja na kupewa mtaji na Mkapa na marafiki zake - kabla ya Mkapa hajaamua kumuanika kwa kumtangaza kuwa si raia - tayari Jenerali na wenzake - Salva na Mwambo walishashindwa kuendesha kampuni.

Wafanyakazi wakawa hawalipwi kwa wakati, huku yeye akisafiri kila mwezi kwenda kwa mkewe Afrika Kusini. Naye Salva akawa anaenda Uingereza kwa mkewe. Haikuchukua muda mambo yakaenda kombo.

Alipoingia Kikwete madarakani akaanza kujipendekeza kwa kuandika maka ndefu alizozipa kichwa cha maneno, "Barua ndefu kwa Rais KIkwete." Leo eti anakuja kutaka kumshauri Slaa na kujita mwanademokrasia. Mwanadipromasia gani anayezuia mageuzi? Aaache kujipa sifa asizokuwa nazo., kampuni taya
Mkuu ndio maana nimekuomba acha siasa za majitaka. Huna tofauti na wale wanaodai kwamba DR.Slaa kafukuzwa Upadre atawezaje kuongoza nchi, hali hao hao wanaendelea kudai Dr.Slaa ni Padre hafai kuwa rais!
 
Kwangu mimi Ulimwengu ni zaidi ya wale vibaraka walioko Uhuru publication na New Habari , alichosema kamaradi(not comrade) Ulimwengu is not prediction but prophecy.....BIG UP SANA
 
Ulimwengu katumwa na Kikwete. DK. Slaa alishajifunza sana miaka kingi iliyopita. Kwanza, ninyi mnaotaka kumpa heshima huyu kibaka mnaitoa wapi? Unajua huyu akiwa mkuu wa wilaya ndiye aliyezuia mkutano wa kwanza wa mageuzi, hadi pale wanaharakati kama Mabere Marando, Ndimara Tegambage, Anthony Komu walipojitokeza na kupinmga udhalimu wake?

Wanaharakati hao waliandika waraka kwenda nchi za Magharibu na nakumbuka rais wa wakati huo, Ali Hassani Mwinyi aliruhusu wanamageuzi kukutana alipokuwa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akienda ulaya kuomba misaaada baada ya kubanwa na wafadhiri. Sasa huyu Ulimwengu analipi la kujivunia.

Pili, Ulimwengu alikuwa mwenyekiti wa kampuni kubwa - Habari Copr - ikamshinda na badala yake akaiuza kwa fisadi Rostam. Sasa mtu aliyeshimdwa kuongoza watu 200 atawezaje kumshauri rais ajaye?

Anachotaka kukionyesha Ulimwengu hapa ni kwamba Slaa hajakomaa kwa urais hivyo ajifunze. Hili si kweli. CV ya Slaa ni kubwa kuliko yeye na kimsingi Slaa amekuwa kiongozi mkubwa wa madhehebu ya dini, mbumge na katbu mkuu.

Ulimwengu aondoke na pumba zake arudishe jibu kwa Kikkwete - Hatudanganyiki. Angekuwa mrtu wa maana Mkapa asingemvua uraia.

Acha umbwiga Bwana kama hujui kusoma na kuelewa facts ni wewe, sifa ya kiongozi ni yule anayepokea ushauri, anauchuja na kuchanganya na akili yake ndo afanye maamuzi! aliyekwambia wa kukushauri lazima awe amekupita au awe na cv kubwa nani??? hujui hata mwanao wa mwisho (kama unaye) anaweza kukushauri kitu cha maana?
 
Back
Top Bottom