Ulimwengu ampa rais ajaye - Dr Slaa - ushauri murua

Hapa nimeandika akamshauri ******, naona ninyi watu wa JF mnafuta. Au tayari mmelipwa na Zoka? Acheni kuingilia uhuru wa watu wa kujieleza. Leo nimeona kwa nini Mararia Sugu alilalamikia mtandao huu JF kuwa una ubaguzi.

Naamanisha jamaa aliyepanga Ikulu - Mkweere. Ukiondoa hii, wewe INVI nitajua kuwa kweli unatumiwa na ZOKA.

Wewe dogo acha usengele nyuma wakati watu wanajadili mambo ya msingi na yanayotoa mustakabali wa Taifa letu, hakutazwi kupinga na wala sisemi uunge mkono, hayo mashiko unayoyapachika katika hoja zako si mashiko bali ni makalio.

Tuache kutoa lugha zisizo na mantic kwasababu ya kupishana hoja,vinginevyo hakuna haja ya majadriano na kufikia mwafaka kwa maana kila mtu analo lijua basi liwe ni bora zaidi kuliko analolijua mtu mwingine.Huo utakuwa ni ubinafsi uliopita kiasi, ni sahihi kabisa kuwa na mawazo tofauti nanifaida pia kwawanajavi kujifunza vitu vingine.

Ulimwengu ni mtumwenye akili sana na hili nilisha lionana nanikawaambia wanajamvi kitendo cha ulimwengu kurudia kuandia barua ndefu kwa raisi kikwete ambayo aliiandika mwanzoni mwa utawala wa ****** kililenga sifa na kujipendekeza kwa rais.kama kawaida nilipingwa vikali ingawa si kwa matusi kama inavyo taka kujitokeza hapa kwa spanner.Ulimwengu kwa weredi wake na akili ninazo kili kuwa anazo ukilinganisha na makada wengine wa ccm anajambo lamsingi linalojikita kwenye manufaa yake binafsi na sifa alizonazo kwa kikwete.

Kwa kukosa umakini sifa hizi alizonazo ulimwengu kwa kikwete bila kutegemewa zina weza kuingia CDM na hatimaye kuonekana kama mtu safi wakati ni mlanguzi wa ideas/ideology kitu ambacho nikibaya kwa ustawi wa CDM.Kwamfano anamshauri Dr, Slaa asifikirie kumwondoa raisi aliyeshindwa kuliongoza taifa kabla ya uchaguzi 2015 kisa ajifunze matatizo ya wananchi na mahitaji yao.Kama huu sio uchuuzi wa idea ninini?

CDM kama chama cha siasa kimeanza kazi za siasa lini na lini kialianza kufikiria kuchukua dora? uta ona CDM kama chama chenye nia ya kuchukua dora kilianza siasa mwaka 1993 lakini kiliwaunga mkono vyama vingine katiaka swala la kuchukua nchi dora mapa kilipo ona sasa kinajua matatizo ya wananchi mwaka 2005 kikaamua sasa kuanza kuitafuta ikuru.Hata hivyo walipo shindwa kuingia ikuru mwaka 2006 wa kakaa tena nakujitathmini kama mtazamo wao uko sahii katika kulikomboa taifa hili wakaona hawako sawa kidogo wakajipanga upya na kuja na falsafa ya nguvu ya umma.

Kwa mtazamo huu CDM kama taasisi leo kwa kumtaja Dr. Slaa kama raisi mtarajiwa kupitia taasisi hii anaambiwa asitazame kuuondoa utawala huu dharimu kabla ya mwaka 2015 eti wajifunze matatizo ya wananchi. Hii ni makusudi ulimwengu anataka kumnyamazisha Dr. na chama chake wajifungie maktaba wa kasome matatizo ya wananchi waje waibuke wakati wa uchaguzi ili wawa achie CCM waendelee na propaganda chafu kuwa CDM ni chama cha katoliki, wachaga ,ukanda na waleta vurugu.

Vitu kama hivi lazima vitazamwe vizuri, ushauri wa ulimwengu lazima ukataliwe kwa misingi hiyo huwezi kushauri mambo ambayo mimi naamini ya mesha fanyika.utafiti wa matatizo ya wananchi tayari umesha fanyika na chadema na wanajua tatizo la msingi katika nchi hii ni utawa ra bora na uadilifu, mgawanyo wa keki ya taifa usio na ulinganifu, keki inaenda kwa wa chache. Ulimwengu usishauri watu wajifungie wafanye au wajia andae kwa vitu ambavyo tayari vimesha fanyika, shauri ninamnagani utawa huu uana weza kuondolewa kabla ya uchaguzi ujao.

Ulimwengu usijaribu kabisa kuondoa treni kwenye reli zake huo utakuwa nimpango wa kuifanya treni ianguke na sio mafanikio.Nchi hii inawatu wazuri sana na wenye uwezo wa kuongoza taifa hili na sio Dr. Slaa peke yake na kama una nia njema zungumzia mfumo na sio Dr. Slaa au Kikwete vinginevyo hii ni dalili ya kujipendekeza kwa wa kubwa ili uonekane mzuri.

Mtei jumapli kupitia star tiv walikuwa na Christopher Mtikila alisema wananchi wameiamini CDM hivyo kama sio 2012,2013 basi 2015 laziama utawala ubadilike hata hivyo hakuwa mchoyo wa fadhila alimshukuru Mtikila kwa harakati za kuamsha wa tanzania juu ya haki zao tangu miaka ya 1986.Hivyo kwa kauli hii na amini kabisa wananchi wanauelewa mkubwa kabisa juu ya haki zao maana elimu ilisha anza kutolewa tangu miaka ya 1986 na akina mtikila kilchopo ni wizi wa CCM kwenye kura na chama mbadala kilikuwa hakija patikana.

Ulimwengu unazungumzia swala la katiba huo sio ushauri pia nikitu ambacho kipo wazi, na hiyo milolongo mingine nimatukio halisi yaliyo tokea kwenye medani za kisiasa hapa nchini hivyo kwa mtazamo wangu hakuna kitu kizuri ulicho kifanya kwenye hii kazi yako ya uandishi huu.

kila nikimwangalia rais wa nchi namwona kama ana hofu ambayo sio easy kuitamka,nahisi anaogopa kuachia madaraka kabla ya wakati,anapenda sana ajiandae vizuri maisha ya uraiani hasa ukizingatia wake wengi bado wadogo,nafikiri gen ulimwengu ameliona hilo japo hakutamka,lakini naona ushauri wake ni wa muhimu sana,dr slaa kuna haja kubwa ya kukaa na kujiandaa vizuri,kama kuwatoa hawa kwa nguvu tutakufa wote!

Ulimwengu katumwa na Kikwete. DK. Slaa alishajifunza sana miaka kingi iliyopita. Kwanza, ninyi mnaotaka kumpa heshima huyu kibaka mnaitoa wapi? Unajua huyu akiwa mkuu wa wilaya ndiye aliyezuia mkutano wa kwanza wa mageuzi, hadi pale wanaharakati kama Mabere Marando, Ndimara Tegambage, Anthony Komu walipojitokeza na kupinmga udhalimu wake?

Wanaharakati hao waliandika waraka kwenda nchi za Magharibu na nakumbuka rais wa wakati huo, Ali Hassani Mwinyi aliruhusu wanamageuzi kukutana alipokuwa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akienda ulaya kuomba misaaada baada ya kubanwa na wafadhiri. Sasa huyu Ulimwengu analipi la kujivunia.

Pili, Ulimwengu alikuwa mwenyekiti wa kampuni kubwa - Habari Copr - ikamshinda na badala yake akaiuza kwa fisadi Rostam. Sasa mtu aliyeshimdwa kuongoza watu 200 atawezaje kumshauri rais ajaye?

Anachotaka kukionyesha Ulimwengu hapa ni kwamba Slaa hajakomaa kwa urais hivyo ajifunze. Hili si kweli. CV ya Slaa ni kubwa kuliko yeye na kimsingi Slaa amekuwa kiongozi mkubwa wa madhehebu ya dini, mbumge na katbu mkuu.

Ulimwengu aondoke na pumba zake arudishe jibu kwa Kikkwete - Hatudanganyiki. Angekuwa mrtu wa maana Mkapa asingemvua uraia.
Spanner,'
Jenerali hakushindwa kuiendesha Habari Corporation. Alizidiwa ujanja na akina Salva ambaye sasa unaona yuko wapi. He was outvoted.

Huko ndiko kushindwa kwenyewe. Ulimwengu alikuwa mwenyekiti wa bodi ya uhariri na mwenyekiti wa bodi ya kampuni. Atawezaje kuzidiwa ujanja na Salva ambaye alkkuwa CEO tu? Isitoshe Ulimwengu ndiye aliyekuwa na hisa nyingi kuliko huyu Rweyemamu unayedai alimzidi akili. Hapa unataka kuleta hadithi zilezile - "Kikwete si mbaya, bali watendaji wake ndiyo wanampotosha."

Jenerali ni kibaraka wa Watusi hata hilo gazeti lake la Rai kirefu chake ni Rwandazi*****. Tunajua mengi msituchokoze. Nasema tena, aache kijipendekeza hana ubavu wa kumshauri Slaa au Chadema. Akakishauri chama chake - CCM waachane na magamba.

Hali hii inatisha, lakini si mpya. Imetokea kila mahali utawala ulipozeeka, ukapoteza njia, ukasahau hata asili yake, ukapuyanga na kubahatisha, ukababaisha na kubangaiza, ukayumba na kutetereka, ukatekwa na waporaji, ukaendelea kujitutumua kwa kuonyesha ukali wa kijeshi kumbe ndani ya roho yake kiini chake kilikwisha kugugunwa na mapanya-buku kwa muda mrefu. Utawala kama huo unao uwezo mkubwa wa kusababisha maafa kutokana na udhaifu wake.

Sijui kma Nape amesoma maneno haya yenye bashishi na tashwishwi kubwa huku yakitoa tafakuri yakinifu ya hali ya kisiasa nchini na chama cha magamba kilipofikia. Asante mwanazuoni weye kwa kuyaona na kuyasemea haya bila unafiki wala woga

Jibuni hoja, badala ya kunishambulia. Nimesema Ulimwengu ameshindwa kuendesha kampuni yake ya watu 200 atawezaje kumshauri rais mtarajiwa? Tatizo lenu mnashabikia watu msiowajua. Mtu mwenye uraia wa kuandikishwa atakuwaje mzalendo? Huyu jamaa namfahamu ni mbinafsi kupindukia.

Alipokuwa habari alishindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Baadaye kampuni ikazidiwa na mzigo wa madeni. Ikafilisika.

Pamoja na kupewa mtaji na Mkapa na marafiki zake - kabla ya Mkapa hajaamua kumuanika kwa kumtangaza kuwa si raia - tayari Jenerali na wenzake - Salva na Mwambo walishashindwa kuendesha kampuni.

Wafanyakazi wakawa hawalipwi kwa wakati, huku yeye akisafiri kila mwezi kwenda kwa mkewe Afrika Kusini. Naye Salva akawa anaenda Uingereza kwa mkewe. Haikuchukua muda mambo yakaenda kombo.

Alipoingia Kikwete madarakani akaanza kujipendekeza kwa kuandika maka ndefu alizozipa kichwa cha maneno, "Barua ndefu kwa Rais KIkwete." Leo eti anakuja kutaka kumshauri Slaa na kujita mwanademokrasia. Mwanadipromasia gani anayezuia mageuzi? Aaache kujipa sifa asizokuwa nazo.

, kampuni taya

Napata picha kuwa wewe ulikuwa naye pale Habari Corporation ukifanya kazi naye huku ukimchimba na kujenga mbinu za kumwangusha.

Kila mtu anaweza kutafsriri kwa uelewa wake,binafsi namjua jenerali kupitia mijadala ya wazi na maandishi yake
Nimemsoma tangu RAI mpaka sasa RAIA MWEMA (karibu kila toleo),nakiri kwamba sijui makando kando mengine lakini kwa hoja hii hapa na zilizotangulia mfano kuhusu maandiko 12 ukutani jamaa ameandika vizuri sana

Nasema hoja zake zina uwiano unaokubalika!

Mi sina imani sana na Dr Slaa. Naona kama wote ni wale wale. Wakishapata hawakawii kutusahau wananchi.
Atafuata njia ileile ya ccm.

Katumwa na KIKWETE,DR anajua vingi sana,ULIMWENGU hana ya kumueleza DR,ULIMWENGU acha kutumika NA KUPOTOSHA UMA.

Jamani acheni ubishi jenerali yupo sahihi ameona mbali na anajua siasa za Tz,
binafsi napenda sana mabadiliko nimechoka na hawa magamba, nawachukia ccm kwa kila hali bt ukweli ni kwamba kuwatoa ndo inahitajika busara za hali ya juu na umakin mkubwa! Otherwise damu inchi itavugika hvyo tutakosa vyote uongoz bora n.k.
Kuna mwana ccm mmoja aliwah kunihakikishia kabisa kuwa wapinzani wanajidanganya kamwe hawawez kupewa nchi, akasema pia kwamba ccm ni chafu na inajua kila mbinu chafu imewekeza majeshini,usalama n.k na akasema hata wananchi wakipiga kura na kuitosa ccm bado wao ndio wataongoza nchi coz wana Tume ya uchaguz ambayo inawahakikishia ccm ushindi.
Mwana CCM huyo aliniambia hata iweje ccm haing'oki otherwise jeshi litachukua nchi, nikakaa kama wk tu jeshi likatoa tamko!
je hamkuona kauli ya Gen Shimbo?je hamkuona polisi ilivyosaidia uchakachuaji huko majimboni kwa mabomu ya machozi mf mzuri Karagwe! Je hayo hayatupi picha yoyote kwetu.
Hivyo sioni ubaya kwa Jenerali kumkumbusha Rais wangu ajae kuwa katiba mpya ni nyenzo muhimu ili kupata tume huru ya uchaguz itakayo mwezesha Dk Slaa kwenda ikulu bila mizengwe na mambo mengine,
Jenerali ametahadharisha tu kauli tata za Dk slaa juu ya kumuondoa Jk kabla ya 2015 kwa nia njema tu kuwa ccm ilivyo waovu tusishangae wakawapa mashujaa wetu kesi za uhaini na kuwasotesha magerezani ccm ni watu hatari.
hivyo Dk Slaa awe makini kuepuka mitego anayotegewa kumbuka hapa kila mmoja anawait mwengine apotee step watu wa take advantage! Tukumbue NCCR ya Mrema na CUF ya Seif Sharrif je wako wapi sasa? Lazima tuwe makini ccm wanaandaa mipango yao michafu kwa 2015

Ni hayo tu wadau tuache lawama Jenerali ameona mengi na sehemu nyingi duniani kwa kusoma na kuandika magazetini.
ushauri anaopewa Slaa una maana kubwa.
Lakini pia kama nimekosea hapa NIPO TAYARI KUKOSOLEWA.

Katumwa na KIKWETE,DR anajua vingi sana,ULIMWENGU hana ya kumueleza DR,ULIMWENGU acha kutumika NA KUPOTOSHA UMA.
Mkuu soma post yangu hapo juu, unaweza kutapata idea muhimu kuwa why Jen. ulimwengu ametoa usahauri kama huo

Peaceficky,

Mkuu wangu udhanivyo sivyo, na ndio maana nilimwambia Spanner kuacha siasa za majitaka kwa sababu zinapotosha ukweli ktk mjumuiko mzima wa kutoelewa. Ni lazima wakati mwingine uwasome watu kuelewa walichoandika kwa sababu maandiko ya Ulimwengu mwenyewe yameweza kueleweka vibaya, iweje isiwe kauli ya dr.Slaa isiweze kueleweka vibaya!.

Binafsi ujumbe wa Ulimwengu umenionyesha jinsi watu walivyoelewa vibaya sababu za maandamano ya Chadema ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe Jenerali Ulimwengu, ambaye hakuona njia nyingine ya kumuondoa rais madarakani isipokuwa kupitia maandamano. Ndivyo alivyoelewa yeye labda na wewe lakini ni jukumu letu kuwaambia ya kwamba maandamano ya Chadema hayalengi kumwondoa JK madarakani kwa sababu sio kazi ya dr.Slaa wala Chadema na ingekuwa hivyo basi Chadema wasingekuwa na sababu ya kufanya maandamano haya mkoa hadi mkoa kuhamasisha wananchi na serikali kutazama vipaumbele vya Kitaifa kwa maslahi ya taifa letu badala yake wangeandamana kwenda Ikulu wakimtaka Jk ajiuzuru.

Hata mageuzi ya Tunisia, Misri na nchi nyingine za Kiarabu hayakutokana na maandamano ya chama kimoja kuhamasisha wananchi bali wananchi wenyewe chini ya vikundi na taasisi za kijamii ndio walioshinikiza maandamano ya kutaka utawala ama mtawala kujiuzuru.
Na kama Ulimwengu aliyafuatilia vizuri haya maandamano atagundua kwamba vyama vya Upinzani viliungana na wananchi ambao hawakuwa na uchama siku hiyo. Katika maandamano ya Tunisia,Misri na hata hayo ya Libya, Yemen, na Syria wapo wananchi wanachama wa chama tawala walioshiriki maandamano ya kuwaondoa madarakani rais wao.

Tatizo la nchi hizo ni rais na sidhani kama Chadema kama chama inakusudia kumwondoa JK madarakani kabla ya uchaguzi ujao isipokuwa Dr Slaa alikuwa akijibu hoja ya viongozi na watetezi wa JK waliokuwa wakidai kwamba - Maadam uchaguzi umekwisha hakuna sheria wala mamlaka yeyote yanayoruhusu kumwondoa rais madarakani kabla ya uchaguzi ujao na tukifanya hivyo ni UHAINI..
- Statement hii sio ya kweli, na ndio Dr.Slaa kama katibu wa chama alipowajibu ya kwamba kumwondoa rais madarakani kabla ya uchaguzi sio Uhaini.

Ifahamike tu kwamba Dr.Slaa alizungumzia hili kujibu dhana iliyowekwa na wanasiasa na wapenzi wa JK ambao walitaka kuwatisha wananchi kuwa Chadema kwa kufanya maandamano, imekusudia kumwondoa JK madarakani kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 kinyume cha sheria na hilo ni kosa la Uhaini.
Jambo ambalo sii kweli bali ni siasa za kujenga hofu (fear) kwa wananchi kwamba maandamano yale yalilenga kumwondoa rais madarakani hivyo wananchi wasishiriki na kama watashiriki basi watakuwa miongoni mwa wahaini.

Kutokana na uzushi huu, Dr.Slaa alilazimika kujibu hoja hii kwa sababu haikulenga kusema ukweli bali kupunguza kasi za Chadema katika kuhamasisha wananchi kudai haki zao kama walivyoahidiwa. Na ikiwa wananchi wanataka rais aondolewe madarakani kabla ya uchaguzi ujao wananchi wanayo haki na mamlaka kisheria kuwalinda wananchi, sii lazima wasubiri uchaguzi. na hata hayo yaliyotokea Tunisia, Misri, Libya na kwingineko ni haki ya mamlaka ya wananchi ndio maana wanaungwa mkono na mataifa, japokuwa matokeo yake hayaombewi na mtu yeyote mwenye busara.

Lakini watu kama Ulimwengu na wengine wapo hata Chadema walioelewa kwamba Dr.Slaa alimaanisha kwamba wakati wa mageuzi ni sasa na Chadema kwa kupitia maandamano wamepania kumwondoa rais madarakani kabla ya uchaguzi kama ilivyotafisiwa na viongozi wa CCM - HAPANA, sii kweli. Dr Slaa na Chadema hawana uwezo huo isipokuwa wananchi (nguvu ya Umma) wanaweza kabisa kumwondoa rais madarakani.

Na sidhani wala sifikirii kama Chadema walikuwa au wana kusudia kufanya mageuzi kama ya nchi za Kiarabu kwa maandamano yao, na haitakuwa na nafuu yeyote kwa wananchi na chama kama akiondolewa JK kisha usukani ukashikwa na Bilal, Pinda au Anna Makinda. Bado hoja kubwa ya Chadema itasimama pale pale kwani hawatakuwa wamefanikisha lolote ambalo JK analifanya lakini Bilal,Pinda au Anna Kilango hatalifanya.

Isipokuwa narudia tena kusema hivi - Wananchi wasikubali kudanganywa na kutiwa hofu ya kwamba hawana mamlaka ya kumwondoa rais madarakani hadi uchaguzi ujao - Mamlaka hayo wanayo! Na Dr.Slaa kama katibu wa chama alikuwa na kila sababu ya kudhoofisha hofu hiyo ya CCM ili wananchi wapate kujiunga na maandamano ambayo yalikwisha pakwa tope na kujengewa fitna, na kwa bahati mbaya hawafahamu haki na mamlaka waliyokuwa nayo chini ya mfumo wa demokrasia....

Jamani hebu na nyie jaribuni kufanya analysis, jiulizeni ni kwa nini huyu bwana alirudia makala zake za kumsifu JK alizoandikaga miaka 6 iliyopita. Yes ni muandishi mzuri lakini wa opinion sio analyst. Naye kama waandishi wengine anahitaji kujua anasema nini wakati gani. Hiki allichoandika sio msahafu ni opinion yake haihitaji kujibiwa na Slaa. Huyu kaka yangu anajitahidi sema yuko bitter na system kwa hiyo ukimsoma unaona kabisa hiyo kitu. anatusaidia lakini anamaswali mengi ya kujibiwa, kwa mfano katika katiba hiyo hiyo hakuna panapokataza hilo analoita angalizo maana katiba ni interpretation ndio maana kwa katiba hiyo hiyo unaweza kuwa na kiongozi mzuri ama dictator, sasa si kweli kwamba tafsiri yake ya vifungu hivyo vya katiba alivyovichagua ndio necessarily tafsiri sahihi kwa kila mtu. Alichoandika hapa nilitegemea kiwe ni kionjo cha majadiliano nashangaa watu wameona ni conclusion na kuamua kusifia na kushukuru. Hatuwezi kuwa great thinkers kwa kuwa wavivu wa fikra. Ndio maana hata mimi naona labda nihamie wanabidii wanakoandika majina maana walau kuna mijadala hukujamvini mmegeuza eneo la press release kama vyombo vya habari

Peaceficky,

Mkuu wangu udhanivyo sivyo, na ndio maana nilimwambia Spanner kuacha siasa za majitaka kwa sababu zinapotosha ukweli ktk mjumuiko mzima wa kutoelewa. Ni lazima wakati mwingine uwasome watu kuelewa walichoandika kwa sababu maandiko ya Ulimwengu mwenyewe yameweza kueleweka vibaya, iweje isiwe kauli ya dr.Slaa isiweze kueleweka vibaya!.

Binafsi ujumbe wa Ulimwengu umenionyesha jinsi watu walivyoelewa vibaya sababu za maandamano ya Chadema ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe Jenerali Ulimwengu, ambaye hakuona njia nyingine ya kumuondoa rais madarakani isipokuwa kupitia maandamano. Ndivyo alivyoelewa yeye labda na wewe lakini ni jukumu letu kuwaambia ya kwamba maandamano ya Chadema hayalengi kumwondoa JK madarakani kwa sababu sio kazi ya dr.Slaa wala Chadema na ingekuwa hivyo basi Chadema wasingekuwa na sababu ya kufanya maandamano haya mkoa hadi mkoa kuhamasisha wananchi na serikali kutazama vipaumbele vya Kitaifa kwa maslahi ya taifa letu badala yake wangeandamana kwenda Ikulu wakimtaka Jk ajiuzuru.

Hata mageuzi ya Tunisia, Misri na nchi nyingine za Kiarabu hayakutokana na maandamano ya chama kimoja kuhamasisha wananchi bali wananchi wenyewe chini ya vikundi na taasisi za kijamii ndio walioshinikiza maandamano ya kutaka utawala ama mtawala kujiuzuru.
Na kama Ulimwengu aliyafuatilia vizuri haya maandamano atagundua kwamba vyama vya Upinzani viliungana na wananchi ambao hawakuwa na uchama siku hiyo. Katika maandamano ya Tunisia,Misri na hata hayo ya Libya, Yemen, na Syria wapo wananchi wanachama wa chama tawala walioshiriki maandamano ya kuwaondoa madarakani rais wao.

Tatizo la nchi hizo ni rais na sidhani kama Chadema kama chama inakusudia kumwondoa JK madarakani kabla ya uchaguzi ujao isipokuwa Dr Slaa alikuwa akijibu hoja ya viongozi na watetezi wa JK waliokuwa wakidai kwamba - Maadam uchaguzi umekwisha hakuna sheria wala mamlaka yeyote yanayoruhusu kumwondoa rais madarakani kabla ya uchaguzi ujao na tukifanya hivyo ni UHAINI..
- Statement hii sio ya kweli, na ndio Dr.Slaa kama katibu wa chama alipowajibu ya kwamba kumwondoa rais madarakani kabla ya uchaguzi sio Uhaini.

Ifahamike tu kwamba Dr.Slaa alizungumzia hili kujibu dhana iliyowekwa na wanasiasa na wapenzi wa JK ambao walitaka kuwatisha wananchi kuwa Chadema kwa kufanya maandamano, imekusudia kumwondoa JK madarakani kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 kinyume cha sheria na hilo ni kosa la Uhaini.
Jambo ambalo sii kweli bali ni siasa za kujenga hofu (fear) kwa wananchi kwamba maandamano yale yalilenga kumwondoa rais madarakani hivyo wananchi wasishiriki na kama watashiriki basi watakuwa miongoni mwa wahaini.

Kutokana na uzushi huu, Dr.Slaa alilazimika kujibu hoja hii kwa sababu haikulenga kusema ukweli bali kupunguza kasi za Chadema katika kuhamasisha wananchi kudai haki zao kama walivyoahidiwa. Na ikiwa wananchi wanataka rais aondolewe madarakani kabla ya uchaguzi ujao wananchi wanayo haki na mamlaka kisheria kuwalinda wananchi, sii lazima wasubiri uchaguzi. na hata hayo yaliyotokea Tunisia, Misri, Libya na kwingineko ni haki ya mamlaka ya wananchi ndio maana wanaungwa mkono na mataifa, japokuwa matokeo yake hayaombewi na mtu yeyote mwenye busara.

Lakini watu kama Ulimwengu na wengine wapo hata Chadema walioelewa kwamba Dr.Slaa alimaanisha kwamba wakati wa mageuzi ni sasa na Chadema kwa kupitia maandamano wamepania kumwondoa rais madarakani kabla ya uchaguzi kama ilivyotafisiwa na viongozi wa CCM - HAPANA, sii kweli. Dr Slaa na Chadema hawana uwezo huo isipokuwa wananchi (nguvu ya Umma) wanaweza kabisa kumwondoa rais madarakani.

Na sidhani wala sifikirii kama Chadema walikuwa au wana kusudia kufanya mageuzi kama ya nchi za Kiarabu kwa maandamano yao, na haitakuwa na nafuu yeyote kwa wananchi na chama kama akiondolewa JK kisha usukani ukashikwa na Bilal, Pinda au Anna Makinda. Bado hoja kubwa ya Chadema itasimama pale pale kwani hawatakuwa wamefanikisha lolote ambalo JK analifanya lakini Bilal,Pinda au Anna Kilango hatalifanya.

Isipokuwa narudia tena kusema hivi - Wananchi wasikubali kudanganywa na kutiwa hofu ya kwamba hawana mamlaka ya kumwondoa rais madarakani hadi uchaguzi ujao - Mamlaka hayo wanayo! Na Dr.Slaa kama katibu wa chama alikuwa na kila sababu ya kudhoofisha hofu hiyo ya CCM ili wananchi wapate kujiunga na maandamano ambayo yalikwisha pakwa tope na kujengewa fitna, na kwa bahati mbaya hawafahamu haki na mamlaka waliyokuwa nayo chini ya mfumo wa demokrasia....

Mkuu thnx nimekuelewa vizuri sana, then mbna mm naelewa haya yote uliyoyasema tena kwa undani mzuri tu.Cdm ni chama chama so nayafahamu haya kuwa Hatuna lengo la kumtoa Jk kwa maandamano ila majority ikiamua hvyo ni haki yao.
Post yangu nimewatahadharisha tu wote wanao mhukumu Jeneral kuwa katumwa na Jk kuwa wanakosea.
Hata ukisoma ushaur alioutoa Jen. Ulimwengu utaona kuwa hauna makosa na wala hamtetei Jk bt alicho mtahadharisha Slaa ni kwamba awe care na mitego ya CCM, Tunawajua watawala wetu wao wapo tayar kutumia mbinu zote kuhakikisha wanabaki madarakani ingawa cc wananchi tumewachoka! Ndio maana title inasema wazi vurugu ndani ya nchi zitaletwa na watawala na sio Dk slaa.
Hvyo ihitajika uangalifu mkubwa mno wa Dk slaa mana inaonyesha ccm inasubir kwa hamu Dk akosee then wa take advantage, thus y ccm wanatumia nguvu kubwa kupotosha kauli njema tu za Dk slaa kwa umma wa wa tz.
Ni hayo tu mkuu sote tunasubiri kwa hamu saa ya ukomboz wa Taifa letu i mean tunaisubir 2015 tupige kura za kutosha kumpa Dk Slaa Ushindi tena then kama watachakachua tena basi hapo tutaamua kweli kufa kwa kudai haki yetu. Pamoja sana kaka.

Umesema ukweli kabisa ila kitu kimoja ni kwamba bila ya shinikizo kabisa CCM wanataendelea kufanya hivyo wanachofanya maana kuna ulazima wakati mwengine kudai na kuona mambo ya msingi yanatimizwa katika taifa hili

16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom