Ulifanya nini au unafanya nini kupambana na kutokuwa na kazi au ajira ili maisha yaendelee?

Hao pornstars uliowataja wanaishi waisha ya dhiki sana nafsini mwao!! Fuatilia zaidi ulikuwaje mwisho wa waliopita kabla yao! Wengi wamekufa kwa kujiua kupitia drug overdose, STDs, n.k

Wengi wao wanaishi maisha ya sonona! Nje wanaonekana wamefanikiwa ila nafsini mwao hawana amani...mfano mzuri ni Firauni ,nje alikuwa akionekana mtu tajiri ,mwenye kila kitu ila ndani ya nafsi ni mtu aliyeishi hali ya kuwa hana amani.
Firauni gani unayemzungumzia wewe? Maana walikuepo wengi.
 
Kuna jamaa yangu alikuwa anastudio kubwa yenye Camera zaidi ya moja na vifaa vingine kwa ajili ya kurekodi matukio mbali mbali ya watu, kama sherehe na misiba.

Basi bwana, maisha yalinipiga mpaka nikaona isiwe tabu, acha nijiingize kwenye masuala ya upiga picha. Nikajifunza google vitu vya msingi vya kuzingatia wakati wa upigaji picha za matukio ya aina mbali mbali, kama vile picha za kiofisi, picha za kibiashara, na picha za maeneo ya starehe.

Nikaona hiyo haitoshi, nikimfuata jamaa anifundishe jinsi ya kutumia Camera nitamtia uvivu, nikaingia google nikajifunza jinsi ya kutumia Camera za Canon na Nikon. Kipindi kile MB angalau zina unafuu wa gharama, nikipata pesa naingia YouTube najifunza kufanya settings ndogo ndogo na kueidit picha na video. Ilifika mahala mpaka nikawa naongea kingereza cha wahindi (Wanaojifunza Adobe kwa YouTube videos watanielewa).

Nilipojiridhisha nimejua vitu vya msingi, nikamfuata jamaa kumwambia anikodishe Camera nikazunguke ninavyojua jioni tutagawana nitakachopata, jamaa alicheka sana akidhani sijui hata namna ya kushika Camera ila akaniambia jioni nisirudi na chini ya elfu kumi. Kweli nikatoka nikatembea mjini, kumbe ulikuwa ni msimu wa mahafali ya vyuo, nikakuta mdada anasherehe yake, muda wa kuanza umefika na Camera man aliyekubaliana naye hapokei simu.

Akapata tetesi kwamba jamaa alipata dili lenye pesa zaidi akaona aibu namna ya kutoa taarifa, kwa hiyo ameenda kufanya kazi kwa mtu mwingine akiamini atawahi kurudi amfanyie nayeye ila amechelewa.

Sasa muda huo mimi ndiye niko eneo la tukio peke yangu na Camera kubwa, wengine wanapiga picha kwa simu. Watu wake walivyoona yule dada machozi yanamlenga lenga kwa hasira, ikabidi waniite kando tuongee.

Hapo mimi moyo unanienda mbio nikijiuliza sijui niwaambie ukweli kwamba mimi ni mgeni kwenye hii industry, halafu hata hivyo lile tukio ni kumbukumbu ya mtu maishani mwake nikipiga picha mbaya nitamueleza nini anielewe, ila nikajisemea moyoni nikilikosa hili tukio njaa ya ujobless itaniua. Hata sijui ile confidence ilitoka wapi, niliwapa majibu kama vile nina uzoefu wa miaka mingi sana na ile kazi.

Wakanitaka niwatajie package zangu, kipindi hicho hata sikuwa najua kwamba huwa kuna mambo ya package ikimaanisha idadi ya picha ngapi utampa mteja, je zitakuwa kwenye softcopy au hardcopy na ni za size gani kisha utaje na bei.

Nikashtuka ila nikawajibu kisiasa kwamba kutokana na hali ya yule dada alivyoumizwa na ana huzuni mimi ni binadamu na nina utu, nitaifanya kazi yao kiundugu zaidi, kwa hiyo kwenye pesa hatutashindwana tutaelewana mwisho wa kazi.

Hapo ninawaza tuwahi kabla jua halijazama kwa sababu sina taa wala sijui namna ya kubadili settings za rangi kuendana na mabadiliko ya mwanga. Basi nikapewa jukumu la kupiga picha kila tukio, mpaka ile shughuli ikaisha.

Aisee ujobless ukikukanda kisawa sawa ni lazima uwe na akili mpaka unajishangaa, nilipiga picha nzuri yule dada alifurahi mpaka akakiri kwamba bora yule Camera man wake hajaja maana aliwahi kufanya naye kazi ila picha alizopewa hazikufika kiwango cha picha zangu.

Kwa kile kiwango cha furaha ya mwenye shughuli nikaona hapa nisitaje bei nitajipunja, nikamwambia kwa kuwa ubora wa kazi yangu ameuona nadhani sasa ameshajua kwamba mimi viwango vyangu sio vya hawa wapiga picha wa mtaani, ataje yeye atanilipa kiasi gani.

Aisee wakuu, huyu Mungu ni wa ajabu sana, yule dada alisema hali yake ya kifedha si nzuri sana na bajeti yake kwa yule Camera man wa mwanzo ilikuwa laki na nusu, ila kwa alivyoona kazi yangu nitakuwa ni mpiga picha wa gharama sana, hivyo anaomba sana ajikaze anipe laki mbili na nisimkatalie niipokee kwa makubaliano ya soft copies picha 20 na picha 3 size ya A3 kwenye frame.

Kiuhalisia nakumbuka nilipanga nimtajie laki moja, nikidhani ni pesa kubwa sana, hivyo akitaka mazungumzo zaidi yawepo. Basi nikajidai kama nimekubali kinyonge ila moyoni nikasema leo nimecheza bingo bora nilivyokaa kimya kuliko ningeropoka.

Kurudi nikaona nisijekuleta ujuaji wa kuedit nikaharibu kazi na nimeshajijengea jina, jamaa nikampoza kumi yake na tukaongea bei ya kuedit na inshu ya kupata picha za frame, kisha kilichobaki nikaweka mfukoni.

Kazi niliifanya kwa muda kidogo, ila mbeleni nilikuja kuiacha baada ya kuona ni ya msimu sana, inanihitaji muda mrefu kutengeneza jina ndipo watu waniamini kunipa matukio yao ya muhimu na hata hivyo sikuipenda.

All in all ni aina ya kazi kama ukiiwezea inalipa sana, unaweza hata ukaachana na mambo ya kusubiri Utumishi watoe matangazo.
Thanks GOD has done!

Thanks GOD has done.
 
Hata kama ni jobless, bado maisha inabidi yaendelee. Pengine muda huu, kuna jobless wa Mungu anakaribia kukata tamaa au ameshakata tamaa kwa sababu hajui afanye nini au mishe mishe gani kusukuma siku kukiwa na mchongo anausikilizia au kufanya maisha tofauti na kushinda nyumbani amejifungia.

Nitaelezea baadhi ya niliyoyafanya kwa nyakati tofauti tofauti kipindi hicho napambana nitokee kwenye unafuu.

1. Kuna kipindi maisha yalibana sana, ikabidi nirudishe mpira kwa kipa (nyumbani kwa wazazi), lakini baadae nafsi ikawa inanisuta sana hasa nikikumbuka wazee walivyo pambana kunifikisha nilipo, nikaona bora niondoke nikaugulie shida nikiwa najitegemea.

2. Niliwahi kuanzisha biashara ya kukopesha wafanya biashara wadogo wadogo mtaani ninapoishi. Kwa mfano, asubuhi nampa mtu elfu tano, jioni anarudisha sita au elfu kumi kwa kumi na mbili. Biashara ilinoga sana, nikaanza kuwa na amani. Ndugu zangu jobless hii biashara unaweza kuidharau ila inaweza kukupa unafuu mkubwa wa maisha. Kwa wale wenye misimamo ya kiimani kuhusu riba, naomba nisiwaingilie kwenye hili.

Hahaha, shida ikaanzia kwa kiumbe mwanamke, hawa ndugu zetu Mungu awabariki sana, asilimia kubwa ya niliokuwa nakutana nao walikuwa ni waaminifu sana, hawakutaka dhulma ila waliamini wanaweza kunilipa kwa njia nyingine tofauti na pesa. Baada ya kuona hela hazirudi na ujana mwingi nikajikuta nimeingia kwenye mtego wao angalau nipate nusu hasara kuliko kupoteza vyote. Ndio hivyo ndugu zangu biashara ikafa kirahisi sana.

Ujobless uko serious zaidi ya tunavyodhani, kuliko kupambana nao tukiwa mmoja mmoja, nadhani mbinu nzuri ni kuuchangia, tukusanye nguvu angalau kwa kupitia kupeana faraja na mawazo ya pamoja.

Karibu na wewe ueleze makabiliano yako dhidi ya kutokuwa na kazi au ajira kwa nyakati tofauti tofauti iwe tayari umetokea peupe au bado unaendelea kupigana. Angalau kuna wenzetu wanaweza wakapata inshu za kufanya kipitia uzi huu.
Kuwa jobless ni maisha flan ambayo yanakatisha tamaa Sana. Na kuvunja moyoo

Japo bado ni jobless naomba Mungu anikutanishe na watu sahihi ili maisha yangu yabadilikee nahangaika Sana

Nakumbuka nikiwa dar nipo Jobless hata Mia ya kula Sina mshikaji wangu mmoja akanipigia simu anatafuta mteja wa asalii na kipindi hiko soko la asali lilikuwa gumu Sana

Nimehangaika kariakoo humo kutafuta wateja lakn sikufanikiwa. Nilirudi ghetto nikiwa sielew Kuna mshikaji wangu akanipa buku nikaishi

Kesho yake nikatafuta chupa ndogo ndogo ziliikuwepo ghetto maana nilikuwa nimejifunza ujasiliamali kwahiy nilikuwa najua kutengeneza sabunii za majii na materials nilikuwa nishanunua ikabidi chupa zile nizijaze asalii

Kwa kipimo Cha Nusu Lita kwa Lita moja nikaingia mtaani target yangu nikiuza chupa moja nipate hela ya msosi nikitoka uhasibu nikazunguka mpk keko ,kariakooo , buguruni, tabta mpk ubungoo matokeo zero ni jamaa mmoja tyu alichukua namba yangu

Nikarudi ghetto njaa kalii Sana na mchoko wa Hali ya juu maana mgongoni nilibeba chupa tano za Lita moja na tano nusu Lita kwahiy jumla mgongoni nilikuwa na Lita Kama 8 nazunguka nazo

Nikarudi ghetto Sina hata Mia na njaa kalii nikilala njaa siku hiyo ,kesho yake asubuhii nikaamka nazo Tena nashukuru Mungu sikufika mbali jamaa akanipigia simu nimpelekee moja ilikuwa mida ya saa Saba

Aisee nilikuwa hata sisikiii njaa japo sikula siku moja na ya pili ndio muda unasoma saa nane bila kuweka kitu kinywanii

Mungu ni mwema Niko mwanza bado napambana na ujobless lkn at least maisha yanaenda sio Kama kipindi hiko
 
Miaka hiyo nilipanga kwenye nyumba ambayo kila mpangaji ana mishe mishe ya kufanya, kwa hiyo watu wanaamka asubuhi sana kujiandaa kutoka.

Mimi muda huo sina hata usingizi, natamani hata ningepata inshu ya kunifanya nitoke asubuhi na kurudi jioni.

Kitu kilichokuja kunipa nguvu niligundua kwa namna nilivyokuwa najiweka, japo ni jobless najitahidi kuvaa vizuri, msafi na ninanukia angalau vispray vya elfu nne, wapangaji wote au wake wa wapangaji walikuwa wananichukulia mimi kama mtu fulani wa matawi sana. Na walifika mbali wakadhani labda kuna shughuli zangu binafsi ambazo nafanya hazinibani, kumbe hamna lolote.

Kuna siku niko ndani bila ya watu kujua, nikasikia wanawake kwenye stori zao kuna mmoja anawaambia wenzie kwamba amegundua mimi ni Usalama wa Taifa na ushahidi anao, nilicheka sana.

Basi na mimi nikaona nisiwakatishe tamaa, kila ikifika asubuhi sana na mimi najiandaa natoka kama naenda kazini, kumbe naenda kuzunguka kwenye maofisi kutafuta kazi. Nikiona njaa tu imezidi nawahi kurudi nisijenikaangukia njiani, bora nikaangukie kwangu.
😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom