Ukweli wa mapigano ya wafugaji na wakulima - Ikwiriri

Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,145
5,553
Naomba kusema kuwa mgogoro unaoendelea huko Ikwiriri baina ya wafugaji na wakulima ni muendelezo tu wa matukio kama haya ambayo tumekuwa tunayashuhudia katika wilaya nyingine kama vile Kilosa, Kilindi, Hanang, Arumeru, Mbarali na kwingineko. Tatizo hapa si ukwasi walionao wafugaji au umasikini wa wakulima. La hasa ila ni tatizo la kimfumo ambalo limesababishwa na serikali yetu yenyewe. Kuna tatizo la kauli mbovu na za kibaguzi ambazo zimekuwa zinatolewa na viongozi wa serikali kuhusiana na wafugaji. Mfano kama unakumbuka kauli ya PM Pinda kule bungeni ya kuwa wafugaji warudi walikotoka. Hii ni kauli mbaya sana ambayo ina tafsiri nyingi kwa wafugaji ikiwa ya kujihisi kubaguliwa kutokana na kazi yao. Pia kuna suala la uhamishaji wa wafugaji kutoka katika bonde la Ihefu mwaka 2006 pasipo utaratibu maalum na kuwapeleka katika mikoa ya Lindi, Pwani na Morogoro jambo ambalo ndio sasa linalozua maafa haya yote.

Ombi langu kwa serikali ni kujenga mfumo bora wa kifugaji ambao utakuwa unalinda maslahi ya mifugo na wafugaji wenyewe. Tazama kuna mikakati mingi ya kilimo ambayo kwa mtazamo wa haraka utaona kuwa hakuna nafasi kwa wafugaji kujiendeleza zaidi ya leo kuambiwa ondokeni Kilombero, ondokeni Rufiji, ondokeni Mbarali, ondokeni Arumeru. Sasa wataenda wapi?
 
Back
Top Bottom