Wananchi wa Katavi wadai wanakerwa na migogoro ya Ardhi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Wananchi wa Kijiji cha Songambele kilichopo Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wametoa kero mbalimbali ikiwemo migogoro ya Wakulima na Wafugaji sambamba na huduma ya umeme kutokidhi viwango.

Kero hizi zimetolewa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mara baada ya kufika katika kijiji hicho na kusikiliza kero za Wananchi ambapo wamesema changamoto ya migongano ya Wakulima na Wafugaji bado ni tatizo katika maisha yao ya kila siku huku huduma ya umeme katika makazi yao ikiendelea kukatwa kila wakati pasipo taarifa.

Kaimu Mkurugenzi katika Halmashauri ya Nsimbo, Adolf Semindu amesema changamoto ya huduma ya umeme inasababishwa na matumizi ya jenereta huku Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf akisisitiza upendo katika matumizi ya ardhi ili kuondoa mgongano wa Wakulima na Wafugaji.

Aidha, Jamila amewataka Wakulima na Wafugaji kufanya shughuli za kisasa zaidi ili kuondokana na mwingiliano usio na tija katika maisha yao.
 
Back
Top Bottom