Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,532
- 113,667
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Leo taifa la Zanzibar linaadhimisha kile kiitwacho ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar,
Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe,
Katika uga huu wa kisiasa nikuwa matakwa ya Wazanzibar katika siasa mpya, Tutumie mda wetu kumuenzi mwanamapinduzi wetu Che Guevara wa Afrika, baba wa Taifa la Zanzibar.
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Kazi Iendelee!.
Paskali