Ukweli wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar yakimuhusisha mtu asiye maarufu sana, John Okello

Yericko katika ubora wako, pole kwa maswahibu yaliyokukuta karibu kamanda, jasusi mbobezi katika kile chama chetu. huwa nakosa raha ya siku nikipitwa hata uzi mmoja kutoka kwako wewe Pasco Mchambuzi Nguruvi3 mungu na awe nanyi katika uchambuzi murua wa siasa uchwara wa chama kile kile zaidi ya miaka 54 na mwezi mmoja sasa na siku 4.
Leo katika mapumziko ya Mapinduzi Matukufu, sio vibaya kujikumbusha threads muhimu kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P.
 
Taifa la Zanzibar limekulia na kudumaa katika uongo, ulaghai, ghiriba, vitisho Ifahamike na kueleweka kuwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar ilipeperushwa tarehe 12 Disemba 1963.
Huu nao pia ni urongo!, Uhuru wa Zanzibar ni Desemba 10, 1963!. Ukiisha anza na factual error, you are very likely kujaza urongo mwingi humu, hivyo naomba kuwa mwangalifu sana na wewe usije kutulisha urongo!.

Na huu ndio uhalisia wa uhuru wa Zanzibar nje ya mapinduzi ya John Okello yaliyotekwa na Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume

Leo taifa la Zanzibar linaadhimisha kile kiitwacho ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar, lakini uadhimishwaji huo upo katika msingi ule ule wa kilaghai na ghiriba. Wanamapinduzi halisi wametupwa, hawatajwi wala kukumbukwa popote na zaidi wengi wamefutwa usoni pa dunia. Wamevishwa wengine taji la mapinduzi ilihali hawakujua hata kilichotokea Usiku wa tarehe 12 Januari 1964. Karume huyu Abeid hakujua hata mapinduzi hayo yaliandaliweje na nini kilitoke bali aliyajua mapinduzi yao yaliyokuwa yakiratibiwa Dar es Salaam chini ya Juius Nyerere
Huu pia ni urongo mwingine wa wazi wa mchana kweupe, Karume alijua kila kitu, ila ni kweli hakuwepo Zanzibar, sio kwa kuyakimbia Mapinduzi, bali kwa sababu hakukuwa na uhakika kama yatafanikiwa, Karume alisafiri kwa boti usiku ule akiwa na wanae, Amani na Ali kuja bara, mjane wake, Mdogo mtu amelithibitisha hili hapa
'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'-Karume Jnr
Na mama mtu pia alithibitisha hapa
Mama Fatma Karume athibitisha Karume hakushiriki Mapinduzi ya Jan, 1964! TBC Live
Hivyo sii kweli kuwa Karume hakushiriki Mapinduzi, ndio mpangaji na mratibu na kuacha utekelezaji kwa wengine!.

Paskali
 
Huu nao pia ni urongo!, Uhuru wa Zanzibar ni Desemba 10, 1963!. Ukiisha anza na factual error, you are very likely kujaza urongo mwingi humu, hivyo naomba kuwa mwangalifu sana na wewe usije kutulisha urongo!.

Huu pia ni urongo mwingine wa wazi wa mchana kweupe, Karume alijua kila kitu, ila ni kweli hakuwepo Zanzibar, sio kwa kuyakimbia Mapinduzi, bali kwa sababu hakukuwa na uhakika kama yatafanikiwa, Karume alisafiri kwa boti usiku ule akiwa na wanae, Amani na Ali kuja bara, mjane wake, Mdogo mtu amelithibitisha hili hapa
'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'-Karume Jnr
Na mama mtu pia alithibitisha hapa
Mama Fatma Karume athibitisha Karume hakushiriki Mapinduzi ya Jan, 1964! TBC Live
Hivyo sii kweli kuwa Karume hakushiriki Mapinduzi, ndio mpangaji na mratibu na kuacha utekelezaji kwa wengine!.

Paskali

Tunaomba uthibitisho wa ushiriki wa karume ndani ya mapinduzi mkuu.
 
Hawa ndio waarabu wa Zanzibar mmoja mkamata watumwa,mwingine sultani
Screenshot_20180112-215156.png
Screenshot_20180112-214720.png
 
Akielezea mzee Mohamed said humu mnamwita muongo,mchonganishi,mdini na mshamba leo akiongea kamnda ndo mnaona ukweli
Na mseme who's behind 1961 independence na si nyerere tu
 
Historia ya Zanzibar imeandikwa na watu wengi,wengine wameandika historia ya ukweli wengine za uongo,wengine wameandika kwa sababu ya manufaa yao,wengine wameandika ili wapate kujulikana na mengi mengineo

Katika historia zote za mapinduzi ya Zanzibar ni kitabu cha "Kwaheri uhuru kwaheri ukoloni" ndio kitabu peke yake kilichozungumzia ukweli kuhusu mapinduzi ya Zanzibar

https://kwaheri.files.wordpress.com/2010/05/kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf

Ukweli usiofichika wanzibari wengi wenye asili ya Mashariki ya kati na wahindi waliuliwa kinyama,yale yalikuwa sio mapinduzi yalikuwa mauaji ya kimbari (genocide).


Sababu hasa kilichowafanya wazanzibar wasiokuwa na asili ya Kiafrika kuuawa kichuki kama vile ni kuwa wale waliofanya yale mapinduzi walikuwa sio wazanzibar,walikuwa wageni,walikuwa watu ambao hawana hisia wala huruma na wazanzibari...

Zanzibar ni kisiwa,visiwa vyote duniani vina sifa moja,tabia ya wau kuchanganya(cosmopolitan),Tabu kumkuta mzanzibari halisi kuwa hachanganya damu na kabila au watu kutoka nchi nyengine...

Mndegereko kachanganya na muhindi,mwarabu kachanganya na mmanyema,mzigua kachanganya na mshirazi(wairani) nk......hiyo ndio sifa ya wazanzibari hiyo ndio sifa ya kisiwa chochoe duniani....

Hao wanaotawala sasa Zanzibar (CCM Zanzibar) ni mapandikizi ya watanganyika,mpaka mapandikizi yaishe ndio Zanzibar itaweza kujikwamua kutoka katika makucha ya wakoloni weusi

Hebu fikiri Miezi mitatu baada ya Mapinduzi,Zanzibar iliungana na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Zanzibar haijawahi kujitawala wazanizbari hawajafaidi matunda ya kuitawala wenyewe.......

 
Dinipevu et al,

Kwa uelewa wangu finyu, maana ya Zanzibar ni "Negro Coast". Hili ni jina lililotungwa na Waarabu waliofika kisiwani humo baadae kutafuta watumwa na mengineyo. 'Negroes' ndio waliokutwa kwa wingi na walikuwa ni wahamiaji kutoka sehemu mbali mbali za Tanganyika, Msumbiji, Malawi nk.

Lakwanza ufahamu, Wakati hao waarabu unaowasema wanakuja hakukua na Tanganyika. NA Faham kua Big part ya Tanganyika ilikua ni Zanzibar.
 
Taifa la Zanzibar limekulia na kudumaa katika uongo, ulaghai, ghiriba, vitisho na mauaji kwa miaka 51 sasa. Vizazi vimelishwa uongo wa uhalisia wa mapinduzi na wanamapinduzi wa kweli wa Zanzibar bila sababu za msingi, lakini kwa maslahi ya watawala wa Zanzibar kwa msaada wa watawala wa Tanganyika leo Tanzania. Ifahamike na kueleweka kuwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar ilipeperushwa tarehe 12 Disemba 1963. Na huu ndio uhalisia wa uhuru wa Zanzibar nje ya mapinduzi ya John Okello yaliyotekwa na Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume

Leo taifa la Zanzibar linaadhimisha kile kiitwacho ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar, lakini uadhimishwaji huo upo katika msingi ule ule wa kilaghai na ghiriba. Wanamapinduzi halisi wametupwa, hawatajwi wala kukumbukwa popote na zaidi wengi wamefutwa usoni pa dunia. Wamevishwa wengine taji la mapinduzi ilihali hawakujua hata kilichotokea Usiku wa tarehe 12 Januari 1964. Karume huyu Abeid hakujua hata mapinduzi hayo yaliandaliweje na nini kilitoke bali aliyajua mapinduzi yao yaliyokuwa yakiratibiwa Dar es Salaam chini ya Juius Nyerere

Lakini ukweli unaanzia kwenye kundi la watu 300 waliokitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi wa meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbalimbali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhidi ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello. Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.
Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyingine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.
John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye.

John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na PembaNafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

Huko mjini Dar es Salaam ndani ya kipindi cha mapinduzi kulikuwa kugumu sana, hata Julius aliingiwa na hofu ya utawala wa mkono wa chuma wa Okello, sasa ikaanza kusukwa mikaka ya kumpoka mamlaka Okello, Okello hakuwa na chama cha siasa hivyo Mwalimu akapendekeza liundwe baraza la mapinduzi na Okello awe ndie mkuu wa baraza hilo ambalo ndilo litakuwa na mamlaka yote ya Zanzibar.
Okello alikubali wazo hilo ambalo kikao kilifanyikia Dar es Salaam 1/2/1964, ikakubaliwa urais apewe kiongozi wa chama cha siasa yani Karume lakini asiwe na sauti yoyote katika Zanzibar. Baraza hilo lilijumuisha wapiganaji watiifu wa Okello ambao hawakuwa Wazanzibari asilia. Nao ni pamoja na Field Marshal (John Okello (Mganda) na msaidizi wake, Absalom Anwi Ingen (Mjaluo kutoka Kenya). Wengine ni Saidi Washoto (Tanganyika) sasa Tanzania Bara, Mohamed Kaujore (Mmakonde wa Msumbiji) na Hamisi Darwesh (Tanganyika). Walikuwapo pia akina Abdallah Mfaranyaki (Tanganyika), Saidi Natepe (Tanganyika), Seif Bakari (Tanganyika) na Edington Kisasi (Mchaga wa Kilimanjaro-Tanganyika).

Baada ya mgawanyo huo ilikubaliwa pia Abdulahman Babu awe mkuu wa vyombo vya habari pia akiwa ni mjumbe wa baraza la mawaziri. Walikubalikubaliana kuwa tare 1/4/1964 warejee tena Dar kwaajili ya kumalizia mipango ya kuitawala Zanzibar. Hapo ndipo siku aliyokwenda kufutwa Okello katika ardhi ya Tanganyika na Zanzibar katika msingi na muundo wa kisiasa, viongozi na wajumbe wote wa baraza la mapinduzi walipanda ndege moja kuja Dar akiwemo Mungu wa Afrika Okello, walipofika uwanja wa ndege, itifaki iligeuzwa na John Okello akaambiwa asubiri kushuka awe wa mwisho. Baada ya kushuka wajumbe wote ndani ya ndege ile, alikwende komandoo mmoja wa Kitanganyika aliyeita Mzena ambaye baadae alikuwa kuwa mkuu wa ujasusi. Alimwamuru Okello asalimishe silaha yake na kisha kumwamuru rubani aipaishe ndege kuelekea Nairobi.

Kenyatta alimuambia Nyerere kuwa mtu huyo (Okello) sio wa Kenya hivyo ndege ikaelekezwa Uganda ambako alibwagwa na historia yake ikaishia hapo. Huku nyuma kazi ya propaganda ya kubadili ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli ilisimamiwa na Babu, alipiga propaganda kupitia radio kuwa akiyefanya mapinduzi ni Karume na ASP, hata chama chake cha UMMA Party hakukisemea tena.

Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995, 2000, 2010 na mwingine unatarajiwa hapo Oct 2015. Viongozi walaghai na wenye kujali hali za siasa zao wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani kwa jicho la tatu. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe,

Katika uga huu wa kisiasa nikuwa matakwa ya Wazanzibar katika siasa mpya bado yanafinyangwa bila sababu za msingi. Tutumie mda wetu kumuenzi mwanamapinduzi wetu Che Guevara wa Afrika Field Marshal John Okello baba wa Taifa la Zanzibar.

Niwapongeze ndugu zangu Ahamed Bargash, Mohame Said, Dr Harith Ghasany na wengine wengi japo historia zao zimejaa udini angalau wapigania kurejeshwa kwa historia ya kweli ya Zanzibar

CCM ndio wanaadhimisha mapinduzi ya Zanzibar.
Wananchi walio wengi hawana mpango nayo kabisa.
 
John Okello alikwenda Zanzibar kutokea Uganda kwa lengo la kujitafutia riziki kwa kufanya vibarua mbalimbali.
Wazanzibari ambao hawakuridhishwa na Uhuru uliotolewa na Waingereza kwa Chama Cha Sultan Jamshid, wakiwemo kina Seif Bakari, Abdallah Natepe na wenzao wengi wengine walipanga kufanya Mapinduzi.
Tatizo la Wanamapinduzi hao (kwa mujibu was maelezo ya Abdallah Natepe) walikuwa hawana jeshi la kuweza kupindua wala silaha za maana, wakati Sultani alikuwa na ghala la silaha.
Hivyo walipanga kuanza kuvamia ghala la silaha kwa kutumia silaha za kijadi, mapanga, mikuki, mishale, marungu n.k. Walipanga kumtisha Sultani na utawala wake kwa kuvamia kituo cha radio na kutangaza kuwa kuna majeshi ya kigeni yamevamia Zanzibar. Kukamilisha hilo waliazimia wapate mtu mwenye lafudhi ya kigeni. Wakampata John Okello, alikuwa na sauti yenye mamlaka na kafudhi ya kigeni, wakamtanguliza mbele, na kumpa jukumu la kutangaza Mapinduzi kwa kiswahili chake kibovu, watawala wakaamini kuwa wamevamiwa na majeshi ya kigeni, wakataharuki na kukimbia.
Baada ya Mapinduzi kufanikiwa, ilikuwa wamlipe ujira wake kwa kutekeleza vizuri jukumu walilompa kisha aende zake. Okello hakutaka hivyo, bali alijitangaza pia kuwa Mapinduzi yale ni yake na aliyapanga na kuyaongoza yeye, akataka na Serikali pia aipange yeye.
Ndipo alipopewa fedha za kutosha na kuamriwa kuondoka nchini, kwanza hakuwa raia wa Zanzibar wala Tanganyika.
Huo ndio ukweli kuhusu bwana huyo na Mapinduzi ya Zanzibar. Alichokiandika katika kitabu chake cha The Zanzibar Revolution, kuna baadhi ya maelezo yalikuwa ya kweli, lakini sehemu kubwa ya maelezo yake sio ya kweli, amejipamba sana ili aonewe huruma, ambayo hakuipata hata hivyo.
Laiti angetosheka na heshima aliyopewa ya kushiriki Mapinduzi na kutekeleza majukumu aliyopangiwa, angeandikwa vizuri kwenye Historia ya Mapinduzi hayo.
Ulaghai wake wa kutaka aonekane kuwa ni yeye peke yake ndie alikuwa steringi wa Mapinduzi hayo, ndio kumemponza. Alitaka kwenda Msumbiji kupigania Uhuru wakamkataa. Alienda Kenya na huko Kenyatta akamlundika gerezani, hatimae akatokomea kusikojulikana na kufia huko.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
John Okello alikuwa mwanaume wa Shoka.msema kweli mpenzi wa mungu.
 
Nao ni pamoja na Field Marshal (John Okello (Mganda) na msaidizi wake, Absalom Anwi Ingen (Mjaluo kutoka Kenya). Wengine ni Saidi Washoto (Tanganyika) sasa Tanzania Bara, Mohamed Kaujore (Mmakonde wa Msumbiji) na Hamisi Darwesh (Tanganyika). Walikuwapo pia akina Abdallah Mfaranyaki (Tanganyika), Saidi Natepe (Tanganyika), Seif Bakari (Tanganyika) na Edington Kisasi (Mchaga wa Kilimanjaro-Tanganyika).

Mkuu nisaidie kujibu haya maswali;
Katika hawa makamanda, Je kuna aliye hai mpaka sasa?
Je kuna watoto wao ambao wapo na bado wanaushawishi kwenye jamii mpaka sasa?
Je ni nini historia ya Okello baada ya kushuka Uganda mpaka leo.......?

Aksante kwa kutuelimisha
 
Back
Top Bottom