Ukweli utakaojitokeza juu ya Hukumu ya Kesi ya Bernard Morrison ambao Msemaji Bumbuli na Mawakili Uchwara wa Yanga SC hawaujui

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,114
110,494
Siku zote Watu wa Simba SC ambao 99.99% si tu kwamba ni Wasomi bali pia tumebarikiwa Akili Kubwa ili tuweze kutoa Elimu kwa Mashabiki wenye bahati mbaya ya kuwa na Upeo mdogo pamoja na Uelewa mbovu kama wa Yanga SC.

Hivyo basi kwa Faida ya Watu wenye Uelewa mdogo wa Kufikiri kutoka Yanga SC wakiongozwa na Msemaji wao Hassan Bumbuli na Mawakili wao Vihiyo (Uchwara) akina Chacha na Mgongolwa bila kusahau Watangazaji wa Redio na Wachambuzi kadhaa wenye Uyanga Uyanga GENTAMYCINE naenda 'Kuwaelimisha' juu ya Sakata zima na itakayokuwa Hatima ya Kesi imhusuyo Mchezaji Bernard Morrison.

KESI ZILIZOKO CAS YANGA SC ILIZOFUNGUA NI MBILI TU
Ya Kwanza ni kuhusu Mkataba wa Yanga SC na Mchezaji Bernard Morrison.

Ya Pili ni kuhusu Viongozi wa Simba (na siyo Klabu ya Simba) Kumshawishi Mchezaji Bernard Morrison Kujiunga Simba SC kinyume na utaratibu.

KWANINI MAAMUZI YATAKAYOTOLEWA NA CAS HAYATOIATHIRI SIMBA SC?
Ukweli ni kwamba Washtakiwa wa Kimsingi huko CAS ni Mchezaji Bernard Morrison na Viongozi Wawili wa Simba SC Zackaria Hanspoppe na Poti wangu kutoka Mkoani Mara (Musoma) Crescentius Magori na siyo Klabu ya Simba kama ambavyo Watu wa Yanga SC wanavyojaribu Kupotosha na bahati mbaya Wapuuzi wanawaamini.

KWANINI TFF IKO SALAMA KATIKA KESI HII HUKO CAS?
Taarifa iwafikie kuwa Yanga SC imeshtaki CAS Maamuzi ya Kamati iliyosimamia Mwenendo wa Kesi (ambayo kwa Kanuni za TFF) hii huwa ni Kamati iliyo Huru Kimaamuzi na haiingiliwi na TFF na Yanga SC haijaishtaki TFF huko CAS kama Wapuuzi wanavyoeneza.

KWANINI MAAMUZI YA CAS HAYATOATHIRI UBINGWA WA SIMBA SC?
Ifahamike kuwa iliyoshtakiwa huko CAS siyo Simba SC wala TFF bali ni Mchezaji Bernard Morrison na Mkataba wake Yanga SC pamoja na Viongozi Wawili wa Simba SC hivyo hata Maamuzi yatakayotolewa hayatoiathiri Klabu ya Simba na Simba SC hapa iko salama tena 100% kabisa.

MAKOSA YA KIUFUNDI YALIYOFANYWA NA YANGA SC AMBAYO YANAIWEKA SALAMA SIMBA SC KUTOPOKONYWA UBINGWA WAKE HALALI NI HAYA
Yanga SC walitakiwa kuachana na Kumshtaki Mchezaji Bernard Morrison na Kuishtaki Simba kama Klabu ili wawe na Hoja nzito kisha hawa akina Hanspoppe na Magori wakawajumuisha pamoja.

Ili Simba SC ipokwe Ubingwa wake Yanga SC walitakiwa Kuishtaki Simba kama Klabu (tena wakati Ligi Kuu ya VPL inaendelea) na siyo Kumshtaki Mchezaji Bernard Morrison ili CAS iihukumu haraka Simba SC wakati Ligi ikiendelea na siyo kwa sasa ambapo Yanga SC wameingia katika Mtego wa Kisheria uitwao 'Time Barred' hivyo hawataweza Kufua dafu.

MAAMUZI AMBAYO HUENDA CAS ITAYATOA BAADA YA LEO KUMALIZA KUISIKILIZA KESI NI KAMA YAFUATAYO
a
) Mchezaji Bernard Morrison ama Kuamriwa kuwa alikuwa ni Mchezaji halali wa Yanga SC kwa Kipindi kile ila kutokana na ukiukwaji wa Mkataba alikuwa na Haki ya Kutafuta Klabu nyingine.

au

b) Mchezaji Bernard Morrison kuwa Huru ila atapigwa Faini kutokana na kuwahi Kwake Kuzungumza na Viongozi wa Vilabu vingine huku akijua Shauri lake lilipelekwa katika Kamati ya Maamuzi.

au

c) Viongozi wa Simba SC Hanspoppe na Magori Kuhukumiwa Kujihusisha na Soka kutokana na Kumrubuni (Kumshawishi) Mchezaji Bernard Morrison kabla ya Mkataba wa Mchezaji kumalizika au Shauri lake kutolewa Maamuzi na Kamati iliyokuwa inasikiliza.

au

d) Mashtaka yote ya Yanga SC dhidi ya Mchezaji Bernard Morrison na Viongozi Wawili wa Simba SC kutupiliwa mbali na Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS) na Yanga SC Kuamriwa kurudi tena upya katika Kamati ya Rufaa ya Tanzania (chini ya TFF) ili Malalamiko yao kupitiwa tena upya.

au

e) Yanga SC Kuonywa na hata Kupigwa Faini kwa Usumbufu na Kukiuka Utaratibu wa Kisheria ambao uliitaka Kwanza kabla ya Kukimbilia kwenda CAS Yanga SC ingekata Rufaa katika Kamati ile ile iliyoamua Kesi ya Mchezaji Bernard Morrison huku Dar es Salaam ( Tanzania ) na kama ilikuwa haina Imani na Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati hiyo husika bado Kisheria Yanga SC walikuwa na Haki ya Kuomba wabadilishwe ili Rufaa yao isikilizwe na siyo kuruka hatua na Kukimbilia CAS.

Baada ya Elimu hii na Ufafanuzi huu ambao GENTAMYCINE nimewapa wana Yanga SC wote Usiku huu nimalize tu kwa Kuwaambia muda wa Maandalizi ya Ligi Kuu ijayo ni Mdogo na Michuano ya Klabu Bingwa inaanza hivi karibuni tu hivyo nyie endeleeni Kupoteza muda na hii Kesi yenu huko CAS kisha mjikute mmechelewa na mkaanza Kuharibu katika Mechi zenu na Simba SC iendelee kufanya vyema kisha muendelee kusema kuwa inabebwa na TFF.

Na Simba SC wala hatusajili kama nyie bali tunajazilia tu (Kufukia Mashimo) tofauti na nyie Wenzetu ambao masikia mmejipanga Kusajili Wachezaji wengi 'Magalasa' kama Kawaida yenu halafu wakija mnajazana JNIA Kuwapokea kwa mbwembwe na baadae Ligi ikiwa inaendelea na kupamba Moto huku Simba SC ikiwa inagawa Dozi zake tu mnaanza Kuwakataa na Kukimbilia ile Kauli yenu mliyoizoea pale mkifanya vibaya kuwa bado mnajenga Kikosi chenu.

Uzi huu uwafikie wana Yanga SC wote!
 
Siku zote Watu wa Simba SC ambao 99.99% si tu kwamba ni Wasomi bali pia tumebarikiwa Akili Kubwa ili tuweze kutoa Elimu kwa Mashabiki wenye bahati mbaya ya kuwa na Upeo mdogo pamoja na Uelewa mbovu kama wa Yanga SC...
Unajua kuandika maneno mengi kama haya,hayakuondoi kwenye ukweli kuwa wewe huwexi kumfikia wakili mgongolwa japo 1%,haya yote uliyoyaandika siku hukumu inatolewa ndio utaujua ukweli

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Siku zote Watu wa Simba SC ambao 99.99% si tu kwamba ni Wasomi bali pia tumebarikiwa Akili Kubwa ili tuweze kutoa Elimu kwa Mashabiki wenye bahati mbaya ya kuwa na Upeo mdogo pamoja na Uelewa mbovu kama wa Yanga SC...
Maamuzi yako wewe GENTAMYCINE ni ya kifever simba na hukumu nyepesi kwa Morrison. Subili hukumu bwashee, usiongeeongee kujifanya mambo kujua kumbe kwa hili na wewe ni mweupe kichwani. Kumbuka kule CAS hakuna Karia, kidau, Jobo Ndugayoo, wala mwakyembe. Yatajulikana tu
 
Unajua kuandika maneno mengi kama haya,hayakuondoi kwenye ukweli kuwa wewe huwexi kumfikia wakili mgongolwa japo 1%,haya yote uliyoyaandika siku hukumu inatolewa ndio utaujua ukweli

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app

Huyu huyu Alex Mgongolwa ambae anagalagazwa na kesi kibao anazozisimamia pale High Court na Kisutu, au Mgongolwa mwingine
 
Hukumu imetoka au bado
Kwa mujibu wa Matangazo ya Mitandao mbalimbali ya Yanga SC na kupitia Viongozi wao hasa Msemaji Hassan Bumbuli Hukumu ilitakiwa iwe Jana na ndivyo walivyotuaminisha na mpaka kututaka tukae tayari na Wao Kujazana Klabuni Kwao wakiwa na Suti pamoja na Tai zao za Mtumba.

Hivyo waulize Wao Mkuu wana Maelezo ya Kutosha ila kwa wenye Akili tunajua CAS watakuja na Hukumu ambayo Yanga SC hawataamini na watajuta Kufungua Kesi huko. Soma vizuri sana hayo Maelezo yangu kwani Hukumu ya CAS haitotoka mbali na Utiririkaji wangu wa Kihoja hapo juu.
 
Huyu huyu Alex Mgongolwa ambae anagalagazwa na kesi kibao anazozisimamia pale High Court na Kisutu, au Mgongolwa mwingine
Ni huyo huyo Mkuu halafu huwezi amini huko Klabuni Yanga nzima ndiyo Wakili anayeaminika na kukubalika nao kuliko mwingine yoyote wakati ukikaa na Mawakili Wenzake wanakuambia hapo hakuna Wakili bali kuna Wakili Msanii na mwepesi katika Mambo ya Kisheria na ndiyo maana Kesi nyingi anazozisimamia huwa zinamshinda na Kukimbiwa mno na Wateja (Watu) wake.
 
Kesi zilizopo ni
1)uhalali wa Mkataba kati ya morisoni na yanga
2) a) simba kumshawishi mchezaji akiwa na Mkataba.
b) simba kumsajili mchezaj wakat shauri lake lipo kwenye kamati ya sheria na hadhi Za wachezaj.

Shauri lá kwanza limefanikiwa ndo mana shauri la pili pia limesikilizwa..
Hivyo wapenda soka tuwe na subira hakuna haja ya kuanzisha thread nyingi wakat muda utaongea..
 
Anaecheka mwisho ndio anaecheka sana
Ni swala la muda tu ila Morrison ni mchezaji ambaye matukio yake anayo yafanya huwa hazingatii future yake na hilo amelithibitisha katika timu alizocheza huko nyuma
 
Ni huyo huyo Mkuu halafu huwezi amini huko Klabuni Yanga nzima ndiyo Wakili anayeaminika na kukubalika nao kuliko mwingine yoyote wakati ukikaa na Mawakili Wenzake wanakuambia hapo hakuna Wakili bali kuna Wakili Msanii na mwepesi katika Mambo ya Kisheria na ndiyo maana Kesi nyingi anazozisimamia huwa zinamshinda na Kukimbiwa mno na Wateja (Watu) wake.

Mkuu upo sahihi kabisa hapo pa “Wakili Msanii” ndiyo maana aliamua kujibrand kwa kila
siku kufanya Interview na Power Breakfast ya Clouds.Ukitaka kujua kuwa ni msanii,mpe kesi asimamie sasa,utaambulia kilio.Nina kesi za watu zaidi ya wanne zote kasimamia na hakuna hata moja aliyoshinda.
 
Masahihisho ya kiuandishi kidogo mkuu, kwa muktadha maridhawa wa msamiati wa kisheria ni "time barred" na sio "time bad" vinginevyo you're out of a classic fallacy...ahsante!
Asante kwa Masahihisho Mwanasheria na Wakili Msomi narekebisha hivi punde tu naomba Radhi kwa Usumbufu ( Ukakasi ) huo kwa Kimaandishi kwa Lugha hiyo ya Kisheria.
 
Mkuu upo sahihi kabisa hapo pa “Wakili Msanii” ndiyo maana aliamua kujibrand kwa kila
siku kufanya Interview na Power Breakfast ya Clouds.Ukitaka kujua kuwa ni msanii,mpe kesi asimamie sasa,utaambulia kilio.Nina kesi za watu zaidi ya wanne zote kasimamia na hakuna hata moja aliyoshinda.
Ukiwa Msomi mkubwa na ukawa ni Shabiki wa Yanga SC tegemea kupata Laana katika Utendaji wako kwani Yanga SC kwa Lugha nyepesi ni 'Nuksi' Mkuu.
 
Kesi zilizopo ni
1)uhalali wa Mkataba kati ya morisoni na yanga
2) a) simba kumshawishi mchezaji akiwa na Mkataba.
b) simba kumsajili mchezaj wakat shauri lake lipo kwenye kamati ya sheria na hadhi Za wachezaj.

Shauri lá kwanza limefanikiwa ndo mana shauri la pili pia limesikilizwa..
Hivyo wapenda soka tuwe na subira hakuna haja ya kuanzisha thread nyingi wakat muda utaongea..
Hapo no 2 Simba wameitwa kutoa ushahidi, au kesi inasikilizwa upande mmoja tu?
 
FIFA Transfer Matching System (TMS) inafanya kazi mara moja tu kila muda wa usajili unapofunguliwa na kufungwa basi, hii ina maana kubwa sana katika kulinda usahihi kwa mchezaji toka sehemu moja kwenda nyingine.

-Morrison msimu wa 2019/2020 (January 2020) alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miezi sita na ndio uliowekwa kwenye TMS hapa ina maana system ilifungwa mpaka dirisha kubwa la June 2020.

-Mkataba wa extension wa Morrison na Yanga ambao ndio unaleta ukakasi na kesi iliyopo CAS haukuwepo kwenye system (TMS) sababu ulifanyika system ilishafungwa, ulikuwa unasubiria mpaka system iwe wazi tena ili uingizwe.

-Baada ya hukumu ya kamati ya hadhi za wachezaji mwezi wa sita (June) Morrison aliweza kuwa huru na kusajiliwa na Simba kwasababu System ilionyesha hivyo kutokana na mkataba uliokuwepo ni ule wa miezi 6 na sio huo mpya wa miaka miwili.

-Simba waliweza msajili Morrison akiwa huru na TMS ilikubali ombi la Simba kuweka data zake kutokana na ukweli huo, kama ingekuwa ule mkataba wa Extension wa Yanga upo kwenye TMS basi Simba walipaswa kuomba kwa Yanga Release letter ya mchezaji au kufanya Transfer (kutoka Yanga kwenda Simba) ambalo ingekuwa gumu sana kukubaliwa na Yanga.

-Kwa Mantiki hiyo suala la Case iliyopo sasa CAS haiwezi kuadhiri chochote msimu wa 2020/2021 kwenye matokeo katika mkataba wa Morrison na Simba ulikubalika kwa TMS, hata hivyo Yanga hawajawahi kuweka pingamizi kuhusu usajili huo popote pale pindi tu Morisson alipotangazwa kuwa mchezaji wa Simba msimu huu.

-Iwapo Yanga ikishinda atakayeadhibiwa ni Morisson na Morisson akishinda itakayoadhibiwa ni Yanga.
 
Back
Top Bottom