Ukweli uliojificha, Akina Mama Wailiza CCM Chaguzi ya Udiwani Arusha.

Bado Kidogo 2015

JF-Expert Member
May 24, 2012
207
78
Katika uchaguzi uliofanyika leo tarehe 14 July - 2013 wafuasi wa CCM walikuwa na uhakika wa kuibuka na ushindi hata kama ungekuwa membemba kwa sababu idadi kubwa ya waliojitokeza kupiga kura walikuwa akina mama. Tofauti na ilivyo zoeleka miaka nyuma akina mama au wanawake kwamba ni mtaji wa CCM leo wamegeuka na kupigia kura CDM na kusababisha ushindi wa kishindo kwa CDM!

Utafiti ambao nimeufanya kwa baadhi ya makada wa CDM ambao walikuwa wasimamizi walikosa morali wao ule niliouzea katika chaguzi nyingine baada ya kunijuza kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa ni chache na akina mama walionekana kuwa wengi. Nilipowadodosa zaidi walihitimisha ngoja tuanze kuhesabu hali iliyoashiria hawakuwa na uhakika wa kuibuka kidedea. Kitendo cha kuibuka kidedea ina maananisha akina mama wamefanya kweli.

Angalizo kwa CCM kama mpaka nguzo yenu kuu ambayo ni akina mama wamewakataa mjiandae kushindwa vibaya sana sehemu nyingi kama moyo huu wa akina mama wa Arusha utasambaa mikoa mingine. Kuna baadhi ya watu wanaweza wakabeza lakini wale waliokuwa wanasimamia uchaguzi wa leo watakuwa mashahidi wa hili.

Hongereni akina mama kwa kuitendea haki demokrasia, wale waliokuwa wanasema CDM imezoea kuwapa vijana viroba ili waipende wana swali la kujiuliza na akina mama wamepewa nini???

Natumaini baada ya marekebisho ya daftari la wapiga kura 2015 hali itazidi kuwa tete.

Nawasilisha.
 
Niliwahi kusema kuwa mwaka 2010 asilimia kubwa ya mawakala na walinzi wa kura Rombo walikuwa akina mama... Hawa watu wakushaamua kubadilika huwaelezi kitu...
 
Ukitaka kushinda sehemu yoyote teka kundi hili.
 
Wamelipa kisasi kwa kusumbuliwa na CCM (kupitia Halmashauri ya Wilaya) kwa kuwahamisha huku na huko kwa nguvu, wakiwaharibia biashara, mali na maisha yao. Ogopa kura ya kisasi.
 
this is the wind of change, wanaongangania magamba wanatamani CDM, wanachohofia ni kua hakuna posho CDM, huu ni utafiti
katika kata ndogo ya kaloneni hivi jana, baada ya matokeo, swali ni kua leo magamba wako wapi kwenye forum?
 
Katika uchaguzi uliofanyika leo tarehe 14 July - 2013 wafuasi wa CCM walikuwa na uhakika wa kuibuka na ushindi hata kama ungekuwa membemba kwa sababu idadi kubwa ya waliojitokeza kupiga kura walikuwa akina mama. Tofauti na ilivyo zoeleka miaka nyuma akina mama au wanawake kwamba ni mtaji wa CCM leo wamegeuka na kupigia kura CDM na kusababisha ushindi wa kishindo kwa CDM!

Utafiti ambao nimeufanya kwa baadhi ya makada wa CDM ambao walikuwa wasimamizi walikosa morali wao ule niliouzea katika chaguzi nyingine baada ya kunijuza kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa ni chache na akina mama walionekana kuwa wengi. Nilipowadodosa zaidi walihitimisha ngoja tuanze kuhesabu hali iliyoashiria hawakuwa na uhakika wa kuibuka kidedea. Kitendo cha kuibuka kidedea ina maananisha akina mama wamefanya kweli.

Angalizo kwa CCM kama mpaka nguzo yenu kuu ambayo ni akina mama wamewakataa mjiandae kushindwa vibaya sana sehemu nyingi kama moyo huu wa akina mama wa Arusha utasambaa mikoa mingine. Kuna baadhi ya watu wanaweza wakabeza lakini wale waliokuwa wanasimamia uchaguzi wa leo watakuwa mashahidi wa hili.

Hongereni akina mama kwa kuitendea haki demokrasia, wale waliokuwa wanasema CDM imezoea kuwapa vijana viroba ili waipende wana swali la kujiuliza na akina mama wamepewa nini???

Natumaini baada ya marekebisho ya daftari la wapiga kura 2015 hali itazidi kuwa tete.

Nawasilisha.
Wana hasira kwa kitendo cha mpiganaji mwenzao Judith kuuwa kinyama na lile Bomu na CCM kukaa kimya hata Makinda pasipo hata pole, maana wao waliamini akina mama wako na huruma lakini wamegundua hakuna huruma hata chembe.
 
Back
Top Bottom