Ukweli mchungu kwa timu Simba

Mtoa mada mwenye akili fupi za kufikiri pia kumbuka kuwa Viperz huyo huyo mnayetuaminisha kuwa ni mbovu bila Manzuki na huyo mchezaji mwingine uliyemtaja walimtoa Mazembe kwenye klabu bingwa hadi akashushwa huku kwenye ligi ya waliofeli shirikisho ambapo ndio UTOPWENGA IPO pia
 
Ahueni wale watukana matusi bado hawajauvaumia huu uzi. Na hivyo kutoa nafasi kwa wajumbe kujibizana kwa hoja
 
Umesahau Viper ndio alimtoa Mazembe kwenye mabingwa ndio mkapangwa nae huko kwa waliofeli

Champions League hakuna timu mbovu, timu mbovu zote zilitolewa na kutupwa Shirikisho
Simba hii hii iliyozidiwa PWENTI 8 huku BARA?
 
Najaribu kupitapita mitandao mbalimbali, naona kila mtu anasema Simba itatinga hatua ya robo fainali, huku wakikubali kuwa timu yao ni dhaifu lakini bado wanang'ang'ania eti watafika huko.

Mimi nakataa, namba za kiufundi zinanikatalia kabisa,

Ni hivi, huyu Simba kachukua points sita kwa mchovu Vipers, aliyewapoteza wachezaji wengi msimu huu kama Cesar Lobi Manzoki na Bobos.

Mechi ya kwanza kule Uganda Simba ilishinda kwa kudra za MUNGU tu huku mastraika na viungo washambuliaji wote wakishindwa kabisa kufanya kazi yao,

Tukirudi hapa kwetu kwa Mkapa ile juzi ukweli unadhihirika kuwa kuna wachezaji hawafai hata kuichezea klabu kubwa kama Simba huku likifungwa goli tamu na la kiufundi kwa jitihada za mchezaji mmoja mmoja na si timu.

Mechi inayofuata mnakabiliana na wagumu Horoya huku kiufundi Horoya akiwa anaimudu Simba kwa maeneo mengi, yaani kiufupi Simba anakufa hapa kwa Mkapa na kwenda kuzikwa kwa wababe na maanibiteni
Raja Club Athletic. Huku mkubwa Horoya akijihakikishia points zake Saba na kuwa na uhakika wa kuingia robo final kwani mwisho kabisa atamalizana na wabovu Vipers.

Kwa Yanga hii US Monastir hatoki kwa Mkapa
Ni kweli Vipers ni wabovu na ndo maana wakamtoa TP Mazembe ambayo ndo mbovu zaidi..!!Ramli yako umeipiga vizuri Sana ila kumbuka mpira sio kama kufunga vifungo vya shati kama unavyodhania wewe..!!Huyo Horoya alifanya nini Uganda wakati anacheza na Vipers.? Je alishinda.? Na kama hakushinda iwe awe bora kuliko Simba aloshinda.? Ubora wa Timu ni msimamo wa ligi na si vinginevyo..!!
 
Nyie mmefika mpka mjadili hatma ya mnyama?? Mlishaona wapi mgonjwa anajiombea kifo...iwe isiwe tutapita..
 
Hata mimi nakubali kuwa kikosi cha Simba cha sasa kina matatizo ambayo kimsingi yanawezesha kuita timu ni mbovu. kwa leo siwezi kuelezea, ila timu itatinga robo fainali kwa kutumia jina na uzoefu. hakuna namna nyingine.
 
Kwani hao vipers wamepoteza wachezaji wengi wangapi?, Maana Kila mtu anasema vipers imeuza wachezaji kibao Sasa wangapi?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Ni hivi, huyu Simba kachukua points sita kwa mchovu Vipers, aliyewapoteza wachezaji wengi msimu huu kama Cesar Lobi Manzoki na Bobos.
Yaani wawili ndio wengi, mbona Yanga imewapoteza Makambo, Bigirimana, Yacouba, Kambole, Morrison na Feisal ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom